TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mkoa
Wilaya
Eneo
Namba ya simu
Namba ya mita
Jinsi ya kufika kwako

Tunaomba hizo taarifa mpendwa mteja
Nimetuma in private message. n nyie mnaweza kuwa kama Tigo, mtu akiwa na tatizo kama hili mkaingiza namba huko kwenu? ili tusilale giza. Nimetum hadi namba za token
 
[HASHTAG]#Tanesko[/HASHTAG]
Naomba kuuliza ni WAKATI gani MTEJA anazuiwa kupatiwa Huduma ya umeme kabisa,hali ya kuwa amelipia kila kitu?
 
Naomba kujua utararibu wa kuvuta umeme kwa eneo linalo itaji nguzo 5
 
Kale kadude ka kuingizia umeme kama kamegoma nichukue hatua gani? Unatoa taarifa unaambiwa kesho na kesho zinakua nyingi, sio hasara kwa shirika?

Ninalala kwenye giza na huku Tanesco wanapata hasara ni uungwana? Mtega akitoa taarifa mshughulike mapema kwa faida ya taifa. Mimi ni mlala hoi mzalendo
 
Naomba umeme wa Rea nguzo tsh ngapi maana niliyotajiwa had i naogopa
 
Kale kadude ka kuingizia umeme kama kamegoma nichukue hatua gani? Unatoa taarifa unaambiwa kesho na kesho zinakua nyingi, sio hasara kwa shirika? Ninalala kwenye giza na huku Tanesco wanapata hasara ni uungwana? Mtega akitoa taarifa mshughulike mapema kwa faida ya taifa. Mimi ni mlala hoi mzalendo
Kwanza hakikisha kana betri na umekiweka kwenye soketi ya imeme na soketi umeiweka ON postion na main switch iwe imewashwa. Hapo lazima umeme uingie
 
Nataka kujua gharama za nguzo umeme wa REA eneo Bukeile Buyango Misenyi maana nimeombwa nitume kila nguzo tshng 350000 nahitaji nguzo zaid ya tatu
 
Kadude kanagoma baadhi ya no haziingii, umeme upo wa kutosha tatizo ni kidude, ukiripoti unaambiwa subiri nikae gizani? Waseme tu nitafute fundi wa kidude.

Samahani nasema kidude na sio dude, sijui jina lake ila Tanesco walinipa bila ya kuniambia jina. Wanipe jibu kwani nipo gizani, au niibe, sijasoma ila potelea mbali naunganisha kivyangu
 
Tanesco siwaelewi kabisa, mbagala wiki hii tu umeme umekatika kuanzia asubuhi kurudi jioni zaidi ya Mara tatu. Tatizo ni nini?. Muda huu Leo tayari wameshakata, hivi kweli sisi wajasiliamali tunaotegemea umeme kusukuma maisha tutajikwamua kweli kwa mtindo huu?. Tafadhalini rekebisheni hizi kasoro.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya matengenezo ya njia ya ya msongo mkubwa wa 132kv kutoka Kurasini-Mbagala na kutandaza mifumo ya udhibiti wa umeme kwenye kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha chang'ombe, iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme Siku ya Jumamosi, tarehe 23 Sept,2017 kuanzia saa 02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 jioni

Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Mbagala yote, mkuranga yote, baadhi ya maeneo ya yombo, baadhi ya meneo ya chang'ombe, temeke, Kimbangulile, Kiburugwa, kilungule, Kingugi, maeneo yote ya Chamazi, Mzambarauni,kijichi, Nyumba nyeupe, Mbande Kiponza, Mbande Bamia, Zakhem, Kizuiani, Rangi tatu, Mbande Kisewe, Nzasa, hospitali ya Rangi tatu, hospitali ya temeke, kituo cha polisi cha cha'ombe, serengeti breweries, Tanzania distillers, CI group, bora industry, TCC, TTCL-Nyerere road, MCL, kiwanda cha Dar steel, kiwanda cha maji poa, ukumbi wa Darlive, Am steel, karibu textile mills, East afrc polybagy, avant industry, camel cement, SD plastic Epz ltd, Maweni industry.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu
 
Tumeiyona mkuu tunaifanyia kazi
Wakati mnaendelea kufanyia kazi, mita imeamua kufanya kazi leo. 'Fundi Mbao' mmoja kaniambia kumbe inaweza kuwa ni tatizo la unyevu kutokana na mvua za juzi juzi hapa.

NA nijaribu tena ikiwa imewakiwa na jua. Mngeweza kuniambia hili . Maana bila fundi mbao wangu, ningeendelea kusubiri tu leo, miendelea KUFANYIA KAZI. Pia mtupe ushauri kama mita za nje zinapata unyevu na buttons kugoma tufanyeje?

Pia kuweni kama wenzenu wa mitandao ya simu, kama nimeshindwa kuingiza namba, basi toeni msaada immediate ili niendelee kutumia umeme na kuwapa pesa. maana nikilala giza, mnapoteza pesa. Uzalendo uanzie TANESCO kwa kweli!
 
Wakati mnaendelea kufanyia kazi, mita imeamua kufanya kazi leo. 'Fundi Mbao' mmoja kaniambia kumbe inaweza kuwa ni tatizo la unyevu kutokana na mvua za juzi juzi hapa. NA nijaribu tena ikiwa imewakiwa na jua. Mngeweza kuniambia hili . Maana bila fundi mbao wangu, ningeendelea kusubiri tu leo, miendelea KUFANYIA KAZI. Pia mtupe ushauri kama mita za nje zinapata unyevu na buttons kugoma tufanyeje? Pia kuweni kama wenzenu wa mitandao ya simu, kama nimeshindwa kuingiza namba, basi toeni msaada immediate ili niendelee kutumia umeme na kuwapa pesa. maana nikilala giza, mnapoteza pesa. Uzalendo uanzie TANESCO kwa kweli!
Mafundi wetu watakufukia mkuu
 
Mafundi wetu watakufukia mkuu
Kwa mara ya kwanza naisifia Tanesco. Mafundi wamekuja na kubadilisha mita. bila sisi kuhitajika kutoa Hata Senti Moja. Hongereni sanasana. mmenifanya ni regret my earlier sacarsm. Nadhanj tutafika sasa.
 
Kwa mara ya kwanza naisifia Tanesco. Mafundi wamekuja na kubadilisha mita. bila sisi kuhitajika kutoa Hata Senti Moja. Hongereni sanasana. mmenifanya ni regret my earlier sacarsm. Nadhanj tutafika sasa.
Tunashukuru sana mpendwa mteja.sio taratibu wala ruhusa kwa mteja kufanya malipo yoyote kwa fundi anapofanya kazi yake kwani anafanya kwa mujibu wa sheria
 
[HASHTAG]#TANESKO[/HASHTAG]
NILILETA LALAMIKO HAPA KUHUSU NGUZO TULIYO ILIPIA KWA HUDUMA YA UMEME KUNG'OLEWA NA KUSIMIKWA NJIANI NINAPO PITIA.
SASA WAHUSIKA NILIO WATAJA WAMEMDANGANYA MFUATILIAJI MLIYE MTUMA KUWA ILIKUWA YA WIZI ,NA UMEME ULIKUWA WA WIZI.
NDO MAANA WAKA NG'OA NGUZO.

AFISA UHUSIANO UKO WAPI ,MTU AMELIPIA UMEME ANABAMBIKIWA KESI KISA TU NGUZO HAIKUSIMIKWA NDANI YA MITA HAMSINI.
Documents za malipo mnazo,jalada la MTEJA mnalo ,masurveyor wote walio shiriki kazi wapo, MTEJA WENU yupo,figisu za nini kama kunauzembe ulifanyika au watufulani hawaku wajibika kwanini msiwa kemee?

#NYAKATO#TANESKO.
SRMENI TENA NIMEWACHAFUA KWENYE MITANDAO.
MTANIONYESHA.
MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
 
Back
Top Bottom