Siku hizi mbona mnakata tu umeme jamani kama leo kutwa nzima daa!
Ndugu Mteja!

Tafadhali onesha taarifa zifuatazo kwa wepesi wa kufanyia kazi swala lako:

Jina

Wilaya

Tatizo

Simu

Namba ya Mita

Namba ya taarifa/Ombi kama ipo

TANESCO Huduma kwa Wateja

0748550000

Makao Makuu
 
Ndugu TANESCO. Umeme kwangu umekatika ila nyumba za jirani unawaka.

Nikazani luku ila remote yake haionyeshi unit inasoma no 8888888888 zinakuja na kujifuta.

Nikijaribu kuingiza no yeyote inajifuta so nimelala gizani hata sielewi namna ya kuangalia unit wala kuingiza token maana hakiandikiki linasoma 8888888 tu
 
Ndugu Mteja
Tumekupigia simu kwa namba iliyopo kwenye taarifa yako haipatikani, Tafadhali tujulishe namba ya kuwasiliana na wewe kwa huduma bora
Ahsante

TANESCO nasikitika tatizo nililoliwasilisha bado halija tatuliwa kikamilifu takribani mwezi mmoja sasa. Kilichofanyika ni kusimamisha nguzo mpya, kunikatia bomba langu la maji na kuondoka.

Nilipiga tena simu baada ya kuona mafundi hawarudi kumalizia kazi, nikaambiwa kua kuna nguzo nyingine tatu kwenye hii line zimeoza kwahiyo wataleta nguzo nyingine pia inabidi wasafishe njia kwa kupunguza miti na matawi ndio wafunge waya, niliwaelewa vizuri sana nikiwa najua itawachukua siku mbili au tatu kukamilisha kazi.

Mwezi sasa unaisha bado tupo kwenye hatari ya kuangukiwa na waya za umeme. Tafadhali TANESCO naomba tena msaada wako kulifikisha hili swala panapo husika.
Namba ya taarifa ni ileile 0707 kituo cha huduma ni Nyakato Mwanza.


TANESCO asante sana kwa kushughulikia swala langu! leo mafundi wenu wamenipigia na wamekuja kubadilisha nguzo japokua bado hawajafunga waya ila nina matumaini kesho watakamilisha kazi.
Nafuta hii comment yangu ya kutoa shukrani kwasababu mmenikera.
 
@TANESCO hili ombi langu
Mmeliffikia wapi jaman

696000 pesa nyingi Sana hii
Nililipa Lakin hata hamshuhulik
Tangu mwez wa 3 seriously?
 
Nilitaka kumnunulia mteja wangu umeme badala ya 1000 nikamnunulia 10,000 naomba kujua kama naweza kubadilisha hizo token kwenda kwenye mita nyingine au kurudisha pesa.
 
Nilitaka kumnunulia mteja wangu umeme badala ya 1000 nikamnunulia 10,000 naomba kujua kama naweza kubadilisha hizo token kwenda kwenye mita nyingine au kurudisha pesa.
Hii n kama kubadilisha vocha iwe
Pesa uitoe ngumu Sana Kwa hawa jamaa
 
TANESCO Je Kesho mtakata umeme huku Mvuti kama ilivyo kawaida yenu

Naomba nijibu ili nione na-adjust vipi ratiba yangu
 
Shirika limeoza , yaani huduma mbovu kabisa , customers care mbovu kinyamaa , mwaka huu tutaisoma
 
Shirika limeoza , yaani huduma mbovu kabisa , customers care mbovu kinyamaa , mwaka huu tutaisoma
Ndugu mteja, Tafadhali tujulishe tatizo ni nini, Wilaya gani na namba ya ombi/simu kwa hatua zaidi
 
Kuna tetesi kuwa kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 10/9/2022 bei itakuwa 800,000/=. Kuna ukweli wowote?
 
TANESCO Kibaha, bado tunasubiri nguzo Mwanalugali
 
Kuna tetesi kuwa kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 10/9/2022 bei itakuwa 800,000/=. Kuna ukweli wowote?
Kama ulivyosema hizo ni tetesi na zitaendelea kuwa tetesi, Bahati nzuri Juzi saa3 kamili nilifuatilia hayo mahojiano, January Makamba alikuwa anafafanua anasema kwamba serikali kwa wastani inamgharamia kila mtu sh. Laki8 kupata umeme, yani ukiona umeme umewaka kwako ujue serikali imetumia laki8 ili wewe kupata umeme, alivyochanganua hiyo laki8 alisema kwamba ule waya ambao unafungiwa kwako kwa mita moja serikali inaununua 15,000 na minimum akasema wengi ni mita30 ina maana 30×15,000=450,000.

Akasema ile mita ya LUKU gharama yake ni laki1 hadi laki2, na akasema kwa bahati mbaya hivyo vifaa kila wanapoagiza bei hupanda ila ni ngumu kuwabadilishia wananchi bei, akasema pia hapo kuna gharama za mafundi wanaokufungia wewe umeme, kuna gharama za usafiri hadi kuja home kwako.

Na pia akasema ile 321,000 unayolipa ni just a part of total cost, the rest wanagharamia wao. Ila serikali inanufaika na wewe pale utakapoanza kununua LUKU. Ignore tetesi hizo.
 
Ndugu mteja, Tafadhali tujulishe tatizo ni nini, Wilaya gani na namba ya ombi/simu kwa hatua zaidi
Kweli TANESCO mwezi wa tatu huu nasubiri control number nilipie na nikipata control number kuna miezi mingi tu ya kusubiri kuwekewa umeme uwake.
 
Kweli TANESCO mwezi wa tatu huu nasubiri control number nilipie na nikipata control number kuna miezi mingi tu ya kusubiri kuwekewa umeme uwake.
Ndugu Mteja, Tafadhali onesha namba ya ombi au namba ya simu uliyofanyia maombi ya kuunganishiwa umeme kwa hatua zaidi
TANESCO
 
Kuna tetesi kuwa kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 10/9/2022 bei itakuwa 800,000/=. Kuna ukweli wowote?
Tafadhali zipuuze tetesi husika, Bei ipo palepale kwa huduma bora
 
Tanesco muleba kagera mnazingua saa 24 hmna umeme tunalala giza kazi zinakwama jitafakalini wakuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…