TANESCO mimi ni mkazi wa mwanza wilaya ya nyamagana mtaa wa mwananchi nahudumiwa na kituo chenu cha nyakato.
Tangu tarehe 5 June nimetoa taarifa ya emergency ya nguzo iliyooza na imedondoka, bahati nzuri ipo karibu na mti kwahiyo imeegemea mti ndio maana haijafika chini, namba ya taarifa ni 0707.
Mafundi walikuja tarehe 8 June wakaiangalia angalia then wakaniambia wataibalisha, ila ikipita wiki kama itakua bado hawajaibadilisha niwakumbushe kwa kutoa tena taarifa.
Bahati mbaya kweli wiki ilipita na nguzo haikubadilishwa nikatoa tena taarifa tarehe 18 June, simu alipokea mdada akaniambia taarifa imefika na itafanyiwa kazi.
Tangu siku hiyo sijaona fundi yeyote wa tanesco na nguzo bado inaning'inia.
Tarehe 6 August nikatoa tena taarifa kwenye banda la tanesco nanenane, nikiwa hopo bandani wahudumu walipiga simu kwenye kituo chenu na kuulizia taarifa yangu. Taarifa yangu ilikuepo na taarifa ya mafundi waliokuja kuiangalia nguzo pia ilikuepo, nikaahidiwa tena kwa mara ya tatu kua tatizo litashughulikiwa leoleo.
Hadi nimeamua kupost hapa kwenye thread yenu ni kwamba tatizo halijashughulikiwa na mbaya zaidi nguzo inazidi kuinama. Maybe hadi patokee janga ndio mtaibadilisha.
Ni kitu cha ajabu sana mtu unatoa taarifa ya emergency mara zaidi ya tatu halafu inapita miezi almost miwili bila tatizo kutatuliwa.
Tafadhali
TANESCO kuweni wawajibikaji shughulikieni hili swala.