naomba kujua gharama za kuunganisha umeme kwa maeneo ya vijijini kwa umbali usiozidi mita 5-15.
Mpendwa mteja,kwa maeneo ya vijijini ambao yamepitiwa na mradi unaofadhiliwa na serikali vijijini (REA) gharama ni TSH 27000 ndani ya mita moja hadi 30, nje ya mradi wa REA gharama zake ni 320,960/=
 
Mimi sijafanya wiring, ila waliotoa 70000 nguzo inasogezwa karibu na nyumba yako. Ni Kijiji cha Mahorosha karibu na mpakani na Kenya. Mimi nilikataa nikaonekana kama ninapinga maendeleo, wananchi hawajui haki yao. Nikimaliza wiring nitaomba na ninajua ni 27000 tu.
 
Sawa mpendwa mteja, endelea na taratibu zote, kama utapata changamoto nyingne yoyote tafadhali wasiliana nasi kupitia namba 0748550000 TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Binafsi nawapongeza TANESCO MAKAO MAKUU kwa kazi nzuri ya kuhudumia wateja kila napohitaji msaada mnahudumia kwa haraka sana. Pia napongeza TANESCO yenu ya wilaya ya TARIME mkoani MARA nao wapo vizuri wanajitahidi mno

SWALI
Umeme vijijini ni 27,000 kwa upande wa nguzo, mimi nipo kijijini ambako tunalipia 27,000 Service line charge ndani ya mita 30. Nilitaka kupimiwa sababu nahitaji nguzo mbili wakadai nisubiri kwanza huenda kukawa na mabadiliko ya nguzo aidha ibaki hiyohiyo 27,000 kwa nguzo mbili au gharama iongezeke. Leo nimepitia TANESCO Website nakuta gharama ya kujengewa nguzo ndani 90Meters ni 454,654.00 naomba ufafanuzi wa hili tafadhali.
 
Ndugu Mteja!

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

  • Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
  • Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
  • Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
  • Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
  • Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
  • Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
 
Nahitaji ufafanuzi upande wa Rural area kwa hicho kilichopo pichani tafadhali
 
Attachments

  • Screenshot_20230116-093324~2.png
    37.3 KB · Views: 23
Mpendwa mteja,kwa maeneo ya vijijini ambao yamepitiwa na mradi unaofadhiliwa na serikali vijijini (REA) gharama ni TSH 27000 ndani ya mita moja hadi 30, nje ya mradi wa REA gharama zake ni 320,960/=
kama eneo lilipata mradi wa rea kipindi kilichopita nitalipa 27,000/= au nitalipa 320,960/=?
 
Ndugu mteja fanya maombi ya umeme na baada ya vipimo utapata makadilio ya bei sahihi. ^EB
Samahani mtu wa tenesco mimi nipo mkoa wa iringa,wilaya mufindi,mji wa mafinga,kata ya upendo nililipia umeme kwa control number 991033973189 kwa ombi no 131-222-0996 na namba ya ombi 271222-1870 kiasi 515617.52 na recept ikawa 923003150639617 lakin tanesco hapa mafinga mpaka sasa hawajaja na wana longo longo nyingi mpaka kukamilisha malipo naomba msaada nifungiwe umeme maana hali ni mbaya sana
 
samahani kuna ombi nimelituma kule mwisho wa thread
 
Ndugu Mteja
Tunashukuru na kuthamini taarifa yako tumeipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja
JM
 
Nashukuru kwa jibu lako zuri, namba ninayo, nikipata changamoto nitapiga. Sio Mimi tu nipo tayari kuwasaidia walala hoi wenzako ili wajue haki yao. Hao waliopigwa 70000 kuchangia nguzo wengine waliuza mbuzi au mazao yao.
 
Ndugu Mteja
Tunashukuru na kuthamini taarifa yako tumeipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja
JM
Nashukuru sana Tanesco huduma kwa wateja kweli mpo kazini,Meneja wa wilaya alipiga simu ni mtu mzuri sana na ni kwamba alipambania sana eneo tulilopo kuletewa umeme.
Kumbe shida ilikuwa ni taarifa kwamba mwezi huu wa kumi na mbili vifaa havijafika kwahiyo maombi yote ya mwezi wa kimi na mbili hayajafanyiwa kazi vifaa vikifika tutafungiwa na kasema urasimu wilaya nzima ameuondoa kufungiwa umeme ni ndani ya siku saba baada ya malipo.
Namshukuru sana meneja wilaya na ninamtakia kazi njema mungu ambariki apandishwe cheo na vifaa vikifika tufungiwe umeme,lakin pia taarifa ni muhimu ili kuondoa mikanganyiko.
 
TANESCO naomba kujua bei ya kuunganishiwa umeme tayari nimemaliza kujenga nyumba nahitaji kupata umeme haraka.
 
TANESCO naomba kujua bei ya kuunganishiwa umeme tayari nimemaliza kujenga nyumba nahitaji kupata umeme haraka.
Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

  • Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
  • Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
  • Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
  • Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
  • Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
  • Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
 
Habari mimi ni mkaazi wa Moshi- Kilimanjaro sina umeme leo siku ya tatu nilisharipoti zaidi ya mara sita bado tatizo langu halijapata ufumbuzi, hata sasa hivi ninavoandika nimetokea Tanesco wamesema watakuja kutengeneza lakini mpaka sasa sioni dalili ya wao kufika hapa. Mita namba yangu ni 24217992080 (report namba yangu ni 4211). Nahitaji umeme nipo gizani siku ya tatu.
 
Pole kwa changamoto, Tumepokea taarifa kwa ufuatiliaji zaidi ^SK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…