Nataka kuunganishiwa umeme mkoani Kilimanjaro maeneo ya vijijini Marangu
Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
• Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
• Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
• Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
• Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
• Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
• Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/=
Gharama hizi ni kama ilivyoelekezwa na EWURA.
NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 18%
TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU : 0748550000. ^ SK