Jina la kwenye mita namba yangu imekosewa herufi 2.na bamba ya simu.nikinunua umeme namba ya simu inakuja ya mtu mwengine.na jina herufi zinakuja zimekosewa.lakini kulipia 27000.na mchakato wa file yangu kilakitu kulikuwa sawa.
 
Tanesco nilituma maombi ya kuunganishwa umeme kijijini nyumba ya wazee wangu surveyor ameenda ameniambia zinahitajika nguzo 5,

Badae akanishauri nimwombe jirani yangu mmoja naye atume maombi ya kuunganishwa umeme , jirani amefanya hivyo , Ila surveyor amekuja Tena anabadilika anasema nyumba zipo karibu karibu Mimi sijamwelewa , maana naona kabisa anatengeneza mazingira ya Rushwa
Namba ya ombi langu 250323-1202
Namba ya ombi la jiran ni hii 260323-0911
 
Tanzania Electric Supply Company Limited Laana mnayoitafuta kwa wananchi mtaipata tu na kama haitowapata ninyi basi hata vizazi vyenu, Kateni umeme kila mnapojisikia.... Mnatesa sana raia ninyi🤬🤬🤬🤬🤬
 
Hili shirika nani alioliloga? Jana mmekata umeme kutwa nzima kwanzia saa moja asubuhi hadi saa 12:30 jioni leo tena mmekata. Hamjui kuna watu tunategemea umeme kuendesha maisha yetu?
 
Hili shirika nani alioliloga? Jana mmekata umeme kutwa nzima kwanzia saa moja asubuhi hadi saa 12:30 jioni leo tena mmekata. Hamjui kuna watu tunategemea umeme kuendesha maisha yetu?
Yaan halafu hawasemi kitu 😡
 
Nimenunua umeme 7.20am Leo 1/4/2023, mpaka sasa sijapata token. Mita 24219770880 shida ni nini?
 
Raia wengi wanaofanya shughuli zao mkoa Dar es salaam wanaishi Mkuranga /pembezoni ,Kupata umeme lazima uombe wilaya Mkuranga .

Nimeomba umeme mwaka jana mwezi wa kumi mpaka leo hata control number sijapata na sijui wataniingizia umeme mwaka gani ?

Tanesco Mkuranga Kuna ujinga na ubabaishaji uliokithiri nafuatilia control number nazungushwa kama Saa tangia mwaka jana.

Kila nikifuatilia , mara subiri wiki ijayo tunatoa control number...nimefutilia mara nne naambulia ujinga wao tu,Cha ajabu Kuna watu wameomba baada ya Mimi kuomba na tayari wameshapata umeme .

Nawauliza mbona hapo kwenye system inaonyesha huyo kaomba nyuma yangu ( tarehe inaonyesha kaomba baada ya Mimi )na tayari ameshawekewa umeme Kwa nini mm nipo pending ? wanakosa majibu sahihi.

Nawauliza wanaohudumiwa na Tanesco Mkuranga mlifanyaje mkapata umeme au mlipata kabla ya hawa watumishi vijana kuajiriwa ? ,Kweli wale vijana ni wababaishaji na wanakera kweli kweli natamani nipigie mtu ngumi ya pua ,control number tu inacheleweshwa hivi ...

Manager wa pale sijui hata kama anafuatilia kituo chake ,kituo kimekuwa na majibu ya ajabu na nyepesi et " Kwa Sasa hatutoi control number " ndani ya mwaka nzima hawatoi control number kweli ?? Kwa nini wilaya zingine unapata umeme ndani ya wiki moja ,Mkuranga Kuna nini??.

Hata kama ni rushwa wanataka ndio uanzie kutoa kwenye control number kweli ? Tanesco Mkuranga tambueni na sisi RAIA TUNAANGAIKA KUTAFUTA MLO KWA SHIDA NA TABU TIMIZENI MAJUKUMU YENU .


Jamani naombeni msaada jinsi ya Kupata umeme Mkuranga nimefauatilia utaratibu nimeishia kubaniwa control number na kupewa bla bla za kijinga.
 
MAOMBI MAPYA YA KUUNGANISHA UMEME MWANZA MJINI
1. ENEO ni Nyerere road karibu na mataa kwa ajili ya ujenzi
2.Mkoa wa mwanza mjini, wilaya ILEMELA, Mjini kati karibu na msua phamacy
3. Tunahitaji umeme kwa ajili ya ujenzi.
 
Naona malalamiko mengi na hakuna majibu kama kipindi cha Magufuli, sioni haja ya kutoa taarifa katika eneo letu sababu najua hamtajibu
 
"Pamoja mvua za masika kuendelea kunyesha nchini, lakini bado mtiririko wa maji kwenye mabwawa ya kufua umeme ya Hale, New Pangani Falls, Kidatu na Mtera ni wa wastani"

Chanzo: TANESCO Mtandao

GENTAMYCINE nilidhani Kaka Mamlaka na Dada walishamaliza Kuyauza Majenereta yao mengi pale Morocco jirani na Airtel Headquarters kumbe bado?

Yaani Mito mikubwa yote imejaa na Mvua huko Mikoani zinapiga ile mbaya halafu leo mnatuambia ( tena bila Aibu ) kuwa Mabwawa hayajajaa.

Hovyooooo....!!!!!!!
 
Napenda kutoa Shukrani zangu za Dhati na kuipongeza TANESCO. Nimekuwa mteja wenu miaka mingi lkn kwa Hili lililotokea WIKI HII ni kubwa. Jumanne tarehe 11/4/2023 nilijaza taarifa za Kuomba kufungiwa Umeme kwa njia ya Mtandao, mchoro ukawekwa. Tarehe 11/04/2023 hiyo hiyo akaja Saveya kukadiria. Tarehe 12/4/2023 nikatumiwa control namba nikalipa bill kwa 320,900/=. Leo tarehe 14/4/2023 asbh saa 3 nishafungiwa Umeme. Kiukweli nimeshangaa sana Utendajikazi huu wa mwendikasi TANESCO.
Nawashukuru sana Hongereni kwa kazi nzuri TANESCO.
 
TANESCO Kidude (kifaa) Cha kuingizia umeme kimekua kibovu, hakibonyezeki, napata shida sana kuingiza umeme. Naomba mnisaidie kutatua hii changamoto.
 
Mpendwa mteja,ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, pole kwa changamoto hiyo, ili tuweze kufungua taarifa yako tafadhali onesha taarifa kamili zifuatazo kwa huduma bora.
1. Jina
2. mkoa
3. Wilaya
4. Eneo
5. Namba ya simu
6. Tatizo
7. Mita namba
8.Kitu maarufu

TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU: 0748550000
WhatApp: 0758346869
^HS
 
Kipekee nawashukuru Tanesco kwa usikivu na umakini wenu hasa kanda ya Makambako.
Kama taasisi tulipata shida ya umeme kukosa nguvu na kushindwa kuendesha moto ya maji na komputa hazikuweza kuwaka kwa siku 4.
Bahati mbaya wasaidizi wangu walipiga simu nafikiri ya wahusika ambao hawakua jirani nasi hata hivyo walikua active kuja kutatua bali msaidizi wangu alipotea hewani ikatokea mis communication.

Baada ya hapo nilipata mawasiliano ya huyu supervisor +255752841417. Huyu bwana ndani ya nusu saa alituma mafundi na wakalitatua tatizo letu.
Kama tunaweza kuwaanika waliotutendea mabaya kwa nini tusiwaanike waliotutendea mema.
Naipongeza tanesco kupitia huyo jamaa mwenye hiyo namba.
Endeleeni na kazi njema nashukuru.!
 
Hahahaa! umetisha ingawa sio poa sana kuweka namba ya mtu kwenye hii mitandao ambayo ni anonymous.
 
TANESCO Kidude (kifaa) Cha kuingizia umeme kimekua kibovu, hakibonyezeki, napata shida sana kuingiza umeme. Naomba mnisaidie kutatua hii changamoto.
View attachment 2589257
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, ili tuweze kufungua taarifa yako tafadhali onesha taarifa kamili zifuatazo kwa huduma bora.
1. Jina
2. mkoa
3. Wilaya
4. Eneo
5. Namba ya simu
6. Tatizo
7. Mita namba
8.Kitu maarufu

TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU: 0748550000
WhatApp: 0758346869
^NM
 
Hahahaa! umetisha ingawa sio poa sana kuweka namba ya mtu kwenye hii mitandao ambayo ni anonymous.
Ni sahihi,

Naomba radhi kama kuna baya litampata lkn sidhani sana, hivyo naomba TANESCO watu hawa muwafikirie kuwapromote na wengine waige mfano huo.
 
Kwenye nguzo ya umeme kuna shoti tangu jana napiga simu ya emmergency tanesco haiiti. Niko morogoro mazimbu road, kibao cha shule. Msaada mnatusaidiajeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…