Habari za Leo Tanesco nahitaji kuingiza umeme . Umbali wa kufikia nyumba yangu ni nguzo nne je naweza kulipa Tshs ngapi kwa gharama naomba majibu haraka nahitaji kuingiza umeme kupisha pango la nyumba baada ya siku 3.
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022
• Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
• Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
• Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
• Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
• Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
• Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA
Gharama halisi utazipata bada ya surveyor kufika na kufanya tahmini kwenye eneo lako.^OK