Gharama zipi sasa, tufafanulieni tujue
 
Nimezungumzia tatizo la eneo zima yaani kata nzima ya eneo hilo umeme unakatika yaani kila siku unakatika mpaka mara 4 ma hakuna taarifa naomba sana tuwe tunapata taarifa hapa wilaya ya kahama bulungwa mseki naomba sana
 
hello TANESCO
Matumizi yangu hayajawahi kuzidi unit 60 kwa mwezi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, kwa nini msinihamishiwe zero tariff?
Kama kweli mpo kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini; Kwa nini hadi karne ya 21 mumtake mteja masikini asafiri kuja ofisini kwenu kuomba zero Tarriff wakati mna data zote za mita?
Binafsi nafikiri kuna tatizo hapa kwani mtu akitumia unit nyingi hata kama amepta ugeni mwezi huo nasikia huwa mnambadilisha kwenda tarrif ya juu; inamaana mpo kukomoa na siokusaidia???

Kwa nini msiwe na utaratibu kuwa, mtu akitumia uniti za Chini kwa miezi sita mfululizo anahamishiwa zERO TARRIFF na akitumia unit za juu kwa zaidi ya miezi miwli (miezi mitatu mfululizo) anawekwa uniti za juu

Asante
 
Ndugu Mteja!

Tunashukuru kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja, Tunakujulisha kuwa sasa TANESCO imekurahisishia huduma ya wewe kuweze kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa kutumia mfumo bora wa Nikonekt popote ulipo na wakati wowote, Unaweza kufanya maombi kwa njia zifuatazo:

- Nikonekt.tanesco.co.tz

-Nikonekt App (Ipo Play store na Apple store)

- Kubofya *152*00#

-Kwenye ofisi za TANESCO



Kwa Maulizo au msaada wowote tafadhali wasiliana na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa

Simu;0748550000

WhatsApp: 0758346869^EB
 
Habari ya kazi TANESCO . Naomba kufanyiwa key change kwenye mita namba 37209700303. Nyumba ilikuwa inakaliwa na mtumishi wenu, sasa amehama na mita inatakiwa kufanyiwa key change kuja kwenye matumizi ya kawaida na mtumishi wenu kaondoka na unit zake nami nimebaki giza. Msaada jamani. Asante
 
Nimeshafanya online Application na kuprint fomu, na nikapita kwa fundi wiring, nilipopeleka TANESCO waliikataa fomu na kusema kwa sasa hawapokei wateja wapya hadi waishe wa zamani asee! inaboa sana
 
acha unafiki
 
hawa watoa shukran ni dhahiri wamepangwa hakuna mwnancho yoyote anaweza kuwapabshukran Tansco kwa usumbufu wa umeme uliokithiri i
 
Leo tarehe 22/04 saa tano na dakika kumi na tatu baadhi ya maeneo Mbagala hayana umeme tangu jana tarehe 21/04 alasiri, Idd njema Tanesco.
Kiukweli Tansco imewashinda ia kuitoa kuwapa wawekezaji ni dhambi kwao sijui tunakwama wapi
 
Asante kwa majibu mazuri
 
Ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, kwa wateja wa maeneo ya vijijini huwa wanapatiwa huduma kwa kiwango cha 27,000 endapo wapo kwenye mradi wa REA kama ni nje ya mradi basi watapaswa kulipia kulingana na viwango vya kupata huduma ya umeme vilivyo weka wa na shirika.^OK
 
37249129745 we tanesco samahani embu angalia hiyo mita ina deni au maana kila nikitia umeme wanasema haitoshi hela niko miono hapa chalinze
Ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, mita hii ina deni la kodi ya jengo shilingi 12,000 nunua umeme wa zaidi ya kiasi hicho utapata huduma.^OK
 
Ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, mita hii ina deni la kodi ya jengo shilingi 12,000 nunua umeme wa zaidi ya kiasi hicho utapata huduma.^OK
Hii Kode ya jengo mbona kama n Ile service charge mmeirudisha kijanja??
 
TANESCO Mtaa wa Raha/mchikichi na Muhonda kilichobaki ni kuunguza maduka ya watu maana kila baada ya dk 5 umeme unakatika na kurudi maana yake ni nn?

Kila siku mna matengenezo mtaa huu tuu maana kuna nyumba mbili kama sio tatu mtaa wa Raha /Muhonda lazima umeme ukatike muitwe

mbona mnawakwaza sana wananchi na wafanyabiashara wa mtaa huu?

Ifike mahali mutuonee huruma wafanyabiashara na wakaazi wa eneo hili tushachoka sasa
 
TANESCO Kimara mwisho mmeanza tena maswala yenu ya ajabu ajabu.Maisha magumu sana now acheni kukata umeme.Mmekata umeme tangu saa 11 mnategemea nini?!
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tumepokea taarifa ya hitilafu maeneo hayo, wataalamu wetu wanafanya jitihada ili huduma irejee tunaomba radhi kwa adha zilizo jitokeza.^OK
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tumepokea taarifa ya hitilafu maeneo hayo, wataalamu wetu wanafanya jitihada ili huduma irejee tunaomba radhi kwa adha zilizo jitokeza.^OK
Haya,jmosi hii weekend hamjaona mda mwingine kukata umeme zaidi ya weekend,kweli?
Mimi niwashauri jambo,mnapokuwa mnadeal na issues maeneo ya nje ya mji muwe mnafanya katikati ya wiki siku kama za jtano,alhamisi au jnne,mojawapo.
Nje ya mji kunachangamka na kuwa bize weekends hivyo sio muda muafaka kufanya matengenezo yoyote yanayohusisha kukata umeme.Ni kinyume na mjini huko ambako jpili kunapoa.
Nimesoma tangazo lenu kuwa kuna mkandarasi wa treni ya kasi kuna shughuli anaifanya leo na kesho.
Hii sio sawa.Why weekend?
Kwanini isiwe katikati ya wiki ambapo matumizi ya umeme ni madogo na shughuli zetu nyingi zinapoa?
Umeme ni sensitive sana,hata hizo kazi ni bora zifanyike katikati ya wiki na usiku mwingi,mnatutia hasara sana.
 
Habari,ivi ile program ya kuunganishiwa umeme vijijini kwa tshs 27,000 kwa umbali wa nguzo mbili imekwisha? TANESCO
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, huduma hiyo bado ipo, lakini inakuwa chini ya miradi ya REA ambao husambaza umeme kwenye vijiji mbalimbali, kwa walio nje ya miradi au walikosa fursa ya kupata huduma chini ya mradi watalipia bei za viwango vya kawaida vilivyowekwa na TANESCO, gharama halisi mteja atazipata baada ya surveyor kufika na kufanya tathmini kwenye eneo lake.^OK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…