Mbona mnakata sana umeme hadi kero au ndo mama yenu anawatuma mkate umeme hovyo??
 
Naomba kuuliza swali mimi nakaa kwenye nyumba ya taasisi ila nyumba yangu ina umeme ya jirani yangu ipo kama mita 70 hivi haina umeme ila nataka kutoa waya kutoka kwenye extension yangu mpka kwake ili aweze kutumia kwa matumiz madgo madgo kama kuchaj simu n.k

JE, HII INARUHUSIWA MAANA NI NYUMBA YA SERIKALI NA MITA INASOMA JINA LA TAASISI?
Ndugu mteja pole kwa changamoto, tunaomba namba ya simu kwa usaidizi tafdhali.^OK
 
Kila mwaka Tatizo la mgao hutokana upungufu wa maji kwenye Hydroelectric Reservoir dams zinazotegemewa, sasa kwa kuwa shida inajulikana ni upungufu wa maji, na kwa kuwa msimu wa mvua huwa maji mengi yanapotea kwa kuelekea baharini na maziwani kwa speed ya mkupuo, kwa nini Shirika lisijenge water reservoirs nyingi kwenye mabonde yenye kingo kila upande ili kuhifadhi maji mengi yatumike katika kuzalisha umeme nyakati za kiangazi kuliko kuyaachia yaende Baharini na maziwani?

Kwanyongeza;

Njia hii pia husaidia kuzalisha mvua za mara kwa mara katika ukanda wa nchi kavu kama zilivyo mvua za ziwani na baharini.
 
Pamoja na kuwa kuna mgawo wa umeme hapa Mwanza ni zaidi hasa maeneo ya Nyakato National, Mahina, Mwananchi. Kila siku umeme unakatwa tangu saa 12.30 asubuhi na unaporudi saa 1.00 jioni pia kufika saa 4.00 usiku tena unakatwa mpaka saa 8.00 usiku ndipo unarudi na kuzimwa tena saa 12.30 asubuhi. Nilitembelea Shinyanga siku saba mfululizo hawajakatiwa umeme. Nawauliza ndugu zangu waTANESCO Mwanza hasa maeneo ya Nyakato National, Mahina, mwananchi tumewakosea nini?.
 
Jiranii ni kweli nyakato wamezidi kutukatia umeme
 
Kama Meneja TANESCO KWIMBA upo hapa Mungu akulipe unachostahiki na kiukweli Huyo aliekuteua laiti Angelina ungepewa hata ufagiaji tu Maza raia umeniozeshea samaki wangu nyau wewe
 
Kama Meneja TANESCO KWIMBA upo hapa Mungu akulipe unachostahiki na kiukweli Huyo aliekuteua laiti Angelina ungepewa hata ufagiaji tu Maza raia umeniozeshea samaki wangu nyau wewe
Mim pia nipo kwimba huku kata ya mhande ,umeme una siku 3 haujarudi ,Bora nihamishe biashara zangu wilaya ya kahama tu,mashine haifanyi kazi bila umeme
 
Tanesco Temeke kituo Cha yombo sigara.tupatiene ratiba ya mgao wa umeme,ili wateja wenu tuwe tunajua.Kwa mfano leo ni African super league day,mnyama anakiwasha na Al Ahaly huko Lupaso, lakini umeme umekatwa,wapenda soka wanashindwa kufuatilia.acheni kiburi na jiongezeni Bwana,
 
Halafu kuna machizi kwenye uchaguzi bado yatachagua ccm

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Hii ni Kero isiyoelezeka kabisa.
Kila wiki tanesco wanakata umeme mtaani kwetu na inaathiri nyumba takribani kumi.
Utakuta mtu umepigika na mgao wa siku nzima alafu jioni umeme umerudi mnakula mgao mdogo wa nyumba kumi.
Mara nyingi tukiwapigia tanesco kwenye customer care line yao 0748550000 huwa wanatupa namba ya taarifa na mafundi huwa hawaji kabisa au wanakuja usiku sana saa 6 ,7 au 8..
Tumeshawauliza mara nyingi Je hili tatizo hawawezi kuli fix???...mana kila wiki umeme unakatika kwa hizi nyumba chache??

Leo wamekata tena .....ngoja tuone watachukua muda gani kufix maana tushawapigia simu.

TANESCO badilikeni.

Mkazi wa Mbagala Kipati ,Mangaya Street.
 
Mimi naishi simiyu nina tatizo la umeme nyumbni kwangu tokea jana limoti yangu inaandika 000000000 kama vile umeme haupo ila kwa majirani upo kwangu tu ndo haupo nimejaribu kuwapigia wa emergency katika mkoa wangu sijafanikiwa kuwapata namba zao zote hazipatikani. Je kwa ili tatizo nitumie njia gani ili niweze kupata umeme tena. Nakumbuka kwa kipindi cha nyuma lilijitokeza tukawapigia emergency wakaja wakatengeneza leo limejirudia tatizo ni nini nisaidieni
 
Ndugu mteja pole sana kwa usumbufu huo, tafadhali tupatie majina yako, namba ya simu, wilaya , kata na eneo unalopatikana kwa msaada zaidi ^EB
 
Mimi nafikiri tanesco wafanye innovation jamani,ingieni ubia na veta,DIT and costek,tuna jua almost 95% ya mwaka mzima,tuna upepo binde la ufa/baharini wawezesheni or ingieni ubia vijana watengeneze umeme huo tuondokane na story za kina cha maji kimepungua tangu nazaliwa mpk umri huu
 
TANESCO mmekata umeme nikiwa nanyolewa, kinyozi alikuwa ameshanyoa tu pembeni katikati ndo zimebaki nimekuwa kama jogoo, najiuliza nafikaje nyumbani tena ni mchana?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…