Kweli Bongo bado muko nyuma sana kwenye suala la Umeme na maji, tunawazidi mpaka sisi huku Mocambique!!

Mocambique umeme haukatiki kipuuzi kiasi hichi.
Kwanza unakataje umeme?
Nawaonea huruma sana.

Tuwape dp world
 
Leo nipo Kilimanjaro najaribu kupiga namba ya makao makuu bila mafanikio na hyo number ya simu waligawa wenyewe, sijui wamezidiwa au shida ni nn.! Ivi kama nna emergency ipi sehem sahihi ya kuwapata?
 
Kwanini mpaka leo mmeacha namba za simu zisizo fanya kazi hapa?
 
Mgao wa umeme umezidi kuwa mkali mpaka masaa 18 na pia hautangazwi?..
Najiuliza hivi nchi hii ni kweli kabisa tumeridhika na hali hii, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na Wizara husika, viongozi wa juu pia kimya.

Mbaya zaidi vyombo vya habari wala havilizungumzii hili tatizo wao wapo bize kusifia tu na mambo ya umbea.

Hakika taifa hili lina safari ndefu sana.

Haya ndugu waangaza giza (taaNosko) endeleeni kukata na kuwasha mnavyojisikia hakuna wa kuwawajibisha, wauza majenereta na wauza mafuta waendelee kupata faida huku wananchi na wanyonge wakiteseka na kushindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi.
 
Kusema ukweli mm umeme wa tanesco upo kwangu just a formality tu kama umeme Kila siku unakatika zaidi ya mara tatu ni umeme au waImi huo.??? Tena saa zingine unakatika usiku kucha na ni hatari kwa usalama wetu zadi ya wezi...achilia mbali hasara tulizopata kwenye biashara.bora mtu ununue solar yako kubwa Moja yaishe...
 
Nina maombi ya kubadilishiwa Tarrif kwa muda mefu mpka nimekata tamaa, maana nauziwa luku kwa gharama za viwandan. Mh!!!!!!
 
Habari Tanesco. Sisi wakazi wa Mikocheni, eneo la Five ways Bar, kuelekea kwa Daffa, tunapata changamoto ya umeme mtaani kwetu, kwanza kulitokea shoti ya umeme ambayo iliunguza vifaa kwenye kaya nyingi hapa mtaani, na umeme uli[porudi haukuwa na nguvu ya kutosha. . Pia tangu tarehe tarehe 22/10, hadi leo hii, tumekatiwa umeme kila siku kasoro ijumaa tarehe 27 na jumatatu tarehe 30. Jana umeme ulikuwa unawaka na kuzima, na tukitoa taarifa tanesco tunaambiwa ni mgao tu.
Tatizo la kukatoka kwa umeme liko kwenye nyumba chache tu mtaani, nyumba nyingine hazikatiwi, Tunaanza kuona wimbi la nyumba moja moja kuhamishwa line, mfano bar ya 5 ways na MRC.
Ningependa kujua kama tatizo la mtaa huu ni nini.
Kama line ina shida na haiwei rekebishwa, basi tunaomba nyumba zote hizi zihamishwe line, na si nyumba moja moja, kwa usalama wetu sote.
Asante, tunatarajia ufumbuzi wa kudumu, kwani kukosekana kwa umeme kunaashiri sana shughuli za kiuchumi za wakazi wa mtaa huu.

Wahudumu wenu wa simu hawajawa msaada wa kutosha kwetu. Tumeomba ratiba, tukaambiwa inapatikana magroup ya whatsapp. tunaomba pia namba ya admin, au link ya whatsapp ya eneo la Mikocheni ili nasi tuingine kwenye group.
N.B muda huu bado haujakatwa, but mioyo inadunda!
 
Tanesco kwa sasa mnatuonea baadhi ya wateja

Tokea mmebadilisha mita za ukutani kwenda za juu ya nguzo imekuwa kero

Umem ukirudi jioni..huwa unakatika kila saa, yaani mpk kero....
Unakuta mpk ifike saa 4 umeme umekatika zaidi ya mara 6.

Baadhi ya nyumba umeme unawaka zingine hamna
Tumeshapiga simu tanesco mara kibao lkn hamna msaada wowote.

Basi muamue moja tu km umeme hautoshi mje mtoe mita zenu
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tafadhali tupatie taarifa zifuatazo kwa msaada zaidi,
Jina
Mkoa
Wilaya
Eneo
Namba ya simu
Mita namba
Kitu maarufu karibu na wewe
Namba ya nyumba
TANESCO Huduma Kwa Wateja
SIMU: 0748 550000
WhatApp: 0758346869.^OK
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tunaomba namba ya simu kwa usaidizi zaidi.^OK
 
TANESCO habari yako....unajua kuna mambo unafanya yanakuwa hadi aibu....nipe point ya kukata umeme mara zaidi ya tano ndani ya saa moja ..ni marekebisho ya aina gani haya.....yaani mtu na akili zako kweli kila baada ya dk kadhaa unazima unawasha...kwa nini kusiwe na ratiba maalum ( ilala, msongola,kidole kwa jongo) imegeuka kuwa kama eneo la majaribio...ratiba ilikuwa jummanne, ikaongezwa na jumamosi now ni kila siku...yaani j4 na jmosi...ni zaidi ya masaa 16 no power...then siku nyingine ni washa zima...ifikie hatua jiongezeni....hii ndio inafanya ngozi hii iendelee kuonekana ya kitumwa....hakuna kinachofanyika kwa ufasaha....kifupi mnakosea sana ...ni bora msingekuwepo kabisa tukajua moja...kuliko mpo halafu ni kama hampo...!
 
Habari Tanesco polen na majukumu
Fault;
Region: Kilimanjaro
Manispaa ya Moshi kata ya kariwa mtaa wa njiapanda kcmc,Kuna itilafu ya umeme tangu juzi hakuna umeme,tafadhali tunaitaji Msaada wenu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…