Habari wakuu wa TANESCO hasa idara ya ufundi ,hivi hii laini inayopita hapa kimara baruti kushuka chini kwenda hadi kilungule ,hii laini amewashinda kuirekebisha ? Kama mafundi hakuna Tanzania basi mneleta TX kutoka ulaya maana ni miaka sasa kila siku laini hii haiishi matatizo miaka zaidi ya 10 ,hadi leo umeme ni wa kutosha lakini bado laini hii ni shida ,umeme ni mdogo kuliko kawaida mimi nyumbani kwangu nina ups kifaa kinasapoti tv ili kukinga isiungue maana kuna kipindi umeme unashuka hadi 120 kutoka kipimo cha kawaida cha 220 au 210 angalau hata ukifika 198 utaona umeme umetulia , maswali ninayojiuliza (1) hili tatizo hamuoni? (2)hamna cha kutusaidia?(3)au hamna wataalam?(4)au ni makusudi hamtaki tutumie umeme wenu tununue sola?.
Nakumbuka kuna kipindi ilikuwa kila wiki lazima ukate umeme na tunakaa siku hadi 3 hakuna umeme hata simu tunadhani kwa jirani ambao laini yao inatokea upande wa mbezi ipo vizuri tu haina shida ,sijui malaika aliwatembelea mkaja mkaweka transfoma pale karibu na darajani angalau hali ya kukatika ikaacha sasa ni low voltage taa zinawaka kama vibatari ,tunaomba mtutatulie hili tatizo mimi naamini nikiamua mnaweza kulitatua ,sisi ni wateja wenu hebu tuangalieni kama wateja wenye faida maana hata bili tunalipa,lingine namba ya huduma kwa wateja mbezi ya kimara haipokelewi muda karibia mwingi ipo Bize , yawezekana ni kwasababu ya matatizo mengi katika eneo hilo hebu tuangalie ni hili jambo kwa jicho la tatu ,
 
Tanesco naomba kujua, hivi mkimfungia mtu umeme kisha kukawa na shida mkahitajika kuja kurekebisha je taratibu zinakuwaje

Nauliza hivi maana tangu mwezi wa 12 mtu kafungiwa umeme ukawaka siku tatu tu kisha baada ya hapo ukazima mpaka Leo mwezi wa tano huu. Kila akiwapa taarifa hapewi msaada wowote mara subiri, mara umejipangaje kuhusu sisi kuja mara... Na kadhalika na kadhalika

Ajabu ni kwamba wenye mita zilizokuwa na shida walikuwa wengi lakini wengine wataalamu wenu wakija wanawashughulikia ila huyu anaendelea kuzungushwa tu.
 
Mbona hamtoi majibu tanesco?
 
SMAHAN TANESCO MBEZIBEACH MAKAZI MAPYA KUNA SHIDA GAN MNAZIMA NA KUWASHA MARA YA SABA SASA NDAN YA NUSU SAAAAA??
 
Tanesco Tanzania huku kinondoni kata ya msisiriB mmetukatia umeme usiku huu hivi inawezekanaje mnakata umeme usiku jamani watu tumepumzika nyie mnakata umeme kweli jamani huu ubinaadamu wa wap
 
Tanesco Tanzania kwahiyo kabisa mnatukatia umeme muda huu na mimbu ilivyojaa tuwashieni umeme jamani kuweni binaadamu juzi tuu mlisema umeme mwingi kuliko matumizi sasahiki nini mnatufanyia
 
Juzi mlitukatia saa9 usiku leo mmekata saa7mpaka muda huu hamujaturudishia umeme acheni hizi mateso mnazotupa kwa bei ya promosheni tuwashieni umeme muogopeni mungu
 
Ila Tanesco nyie mmeshashindikana yhn mmeurudisha kisha mmekata tena hivi mtu unafaidika nini kukata umeme mida hii
 
Swali ni lini Bei ya umeme itashuka ,tayari tuna umeme wa Maji gharama nafuu kama tulivyoahidiwa na Serikali ya ccm?
 
Tanesco hivi haiwezekani kununua luku ikajijaza Moja kwa Moja ktk meter yangu maana hizi remote zinategemea mtandao umekaaje siku hiyo ktk eneo nililopo mbona Bado mpo ki kale hivi
 
Tanesco samahani nauliza nataka nijiunge umeme kwa mara ya kwanza na nmeona Huna sehem unaweza kuaply online je hii kwel ipo na munaijua??? Inaitwa nikonect...
 
Mnazindua lini mradi wa umeme uliopo Rusumo border, wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera?
 
Tanesko mkoani Tabora wilaya ya Urambo acheni tabia ya kukata kata umeme kama mchezo. Maana umeme huku imekuwa ni changamoto kila sekunde umeme unakata 🙌
 
TANESCO USA River Arusha. Kuna tatizo la umeme, kata ya Imbaseny, Maji ya Chai, mtaa wa Chemchem, toka jana saa sita mchana. Tumepiga simu lakini mpaka Sasa hamkutokea. Tafadhali ondoeni hii kero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…