Nguzo Moja laki tatu?
Ulilipa kwa control namba au ulimpa mtu mkononi akurahisishie upatikanaji maana mie najua kihalali bei ya nguzo ni laki Tano +
 
Naomba mnijuze (yeyote mwenye kujua aseme siyo lazima TANESCO)

Hivi nikihitaji umeme kijijini na nguzo haijanifikia bado je ninaweza kutuma maombi? Na nasikia nguzo inahitajika kulipiwa je nitahitajika kulipia kiasi gani ili niwekewe nguzo (maana nimeambiwa mpaka niwe mita 30 kutoka ilipo nguzo sasa mimi nilipo ni mita wastani wa 60-70, hazizidi mita mia moja)
 
Maombi kutuma ni Bure
Ukishatuma watakuja surveyor ata survey Bure
Ndani ya mita 30 kwa kijijini ni 27,000
(Ndani ya mita 80 ) inamaana nguzo Moja mita 50 + waya kutoka kwenye nguzo kuja kwako 30m inagharimu 519000 itategemea ila isikate kiwanja Cha mtu
 
Nashukuru sana, hivi hiyo nguzo nikishailipia itakuwa hakuna mtu mwingine kuchukulia umeme hapo kwenye nguzo yangu au watanirefund au ndo basi tena watapata mserereko?
 
Nashukuru sana, hivi hiyo nguzo nikishailipia itakuwa hakuna mtu mwingine kuchukulia umeme hapo kwenye nguzo yangu au watanirefund au ndo basi tena watapata mserereko?
Hakuna utaratibu wa kumchangisha jirani
Kwa mfano Kuna Mzee mmoja kikiji Fulani kanunua transfoma yake kwa ajili ya kuazisha mashine na ghala la nafaka lakini jirani yake akavuta kwa hiyo hiyo transfoma kwa 27000
Sembuse na wewe nguzo Moja
USHAURI
Mshirikishe jirani mpige hesabu mgawe kwa idadi yenu then mmoja mumpe hiyo Hela aesabike kama kailipia yeye ili mzani uwe sawa asionekane wa kulaliwa na wengine mnalipia gharama ya meter
 
Kuna swala la kubadilisha mita Dareslam,,,,,
Inaonekana mafundi wenu wanafanya ni mradi sasa wa kuwatishia watu kwa kuwaeleza mita zimechezewa na wanaomba wapewe pesa ili wafunge mpya la sivyo wawapeleke watu mahakamani!!
Na wanawatisha watu bila huruma!!
Pitieni maeneo ambayo mita zilitakiwa kuweka na hawajaweka siku ya leo kisa wanalazimisha wapewe pesa!!
Dau lao ni milioni moja na nusu Hadi laki nane!!
Tanesco fanyieni kazi hilo ,,, watendaji wenu wanamchafua mama
 
Hawa TAANESIKO walisema ikifika Julai wataweka mfumo wa ukilipa bill inaingia moja kwa moja
 
Tanesco ni majizi
Ni baadhi ya watendaji wasio waadilifu,,,, kama siku ya tarehe 08/07/2024 maeneo ya Kimara walifanya vitu visivyo vya kiungwana na vya hovyo sana!! Wanawachekecha watu wasio na uelewa kwenye madude yao na kuomba wapewe 1.5mil, laki 8, laki 3 n.k so shame!!
Na baadhi ya nyumba hawajaweka mita wakisubiri pesa walizoomba!!
Watendaji wachache wasio waadilifu huchafua hizi taasisi!!
Watendaji mlioko maofisini fatilieni nyumba ambazo hawajawekewa mita, na waulizeni kwa nini hawajatolea taarifa ijapokuwa changamoto nyingine ni kubebana kwenye maofisi!! Ila wanachafua serikali kwa ujumla pamoja na taasisi yenu Tanesco-meneja Kimara na maeneo mengine tazameni hawa vijana wenu!!!
 
Kuunganishiwa umemw ni bei gani ? Kwa vijijini na mijini pia umeme unatarajiwa kupanda garama za kuunga au kupungua?
 
Halafu mbona kama mmeanzisha mgao wa kimya kimya? Au mabwawa mmeyatoa maji tena.

Hii nchi ngumu jamani, kila kitu hakiendi. Tuko kama jehanamu
 
swala la POWER-CUT kwenye metre za Wasion.LUKU haiingii.
Suluhisho lake ni nini?Kwanini msituelekeze tunarestet vipi--mpaka tuwapigie kila saa
 
Tanesco imekua kero sana kwa wateja wenu. kuanzia tarehe 1 mpaka 7 July 2024 kumekua na sintofahamu kubwa sana unaponunua umeme unapewa nusu ya ile pesa ulionunua, yaani mfano ukinunua umeme wa ths 5000/= ambapo ulitakiwa upate unit 14 utapata nusu yake yaani utapata unit 7. Ukiwasiliana na huduma kwa wateja wanakwambia kuna tatizo(error) katika mita yako ambayo inaonyesha kua mita yako imechezewa hivyo imesababisha deni lisilopungua chini ya tsh 1,000,000/= na kuendelea. Leo tarehe 15 July 2024 hata kama kweli mteja ulichezea mita katika matumizi ya kawaida ya yumbani kweli unaweza ukatumia umeme wa kiasi cha tsh milioni na ushee kwa muda wa siku 10 mpaka 15?.
Wanasema kuna wakaguzi wa mita/luku walipita na kuacha barua inayoeleza juu ya deni hilo ilihali wakaguzi hao hawajonekana wala barua hazijapokelewa kutoka Tanesco.
Operation kama hii kutoka Taasisi kubwa kama hii Tanesco inatekelezwa vipi bila kutoa taarifa wa wateja weke?

Note: Hili tatizo limekua kubwa hasa mkoa wa kinondoni( Kawe, Kijitonyama makumbusho N.K....) Tanesco pitieni Mifumo yenu vizuri, tunaamini mpo katika maboresho ya mifumo na lengo ni kweli 'KUANGAZA MAISHA YA WATANZANIA' ila kwa mabambiko haya ya madeni kwa wananchi ni kama mnaenda kinyume na kauli mbiu yenu.
NAWASILISHA...
 
swala la POWER-CUT kwenye metre za Wasion.LUKU haiingii.
Suluhisho lake ni nini?Kwanini msituelekeze tunarestet vipi--mpaka tuwapigie kila saa
Suluhisho la wassion jitahidi usiishiwe kabisa umeme hasa wassion toleo la kwanza linasumbua sana
Maana ukiishiwa umeme Kuna kuwa na changamoto ya kupoteza mawasiliano kati ya meter juu ya nguzo na remote Yako JITAHIDI USIISHIWE UNIT
 
Je TANESCO huwa mnapokea pesa bila kutoa risiti? Kule Wilaya ya RUNGWE,mkoa wa mbeya,kata ya Kiwira ,kijiji kinaitwa ilundo,kuna eneo linaitwa ISOKO,wananchi wanachangishana shilingi laki 5 tano,wanapewa jamaa wa TANESCO wanapeleka nguzo na umeme unaunganishwa! Hizo pesa wanasema ni za nguzo,lakini hawatoi risiti! Hebu tupeni maelezo kamili! Kwani nasikia mtu wa kule kama hakuchanga hiyo laki 5 hawezi unganishiwa umeme hata kama nguzo ipo nyumba ya jirani,masharti kwanza apeleke laki 5 kwa balozi ndipo aunganishwe umeme
 
Hizi mashine za kuwekea umeme ukishanunua zinasumbua sana wakati unaweka nielekee wapi kupata msaada zaidi niko ilala
 
Naona TANESCO wenyewe wako Bize wanakula kvat tu! They are not up to date! Ngoja tuendelee na maisha mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…