Wakuu.

TANESCO KASULU hawa jamaa hawafai toka nimefika huku kwa siku umeme wanakata hadi mara sita na hawatangazi kwa wananchi kiasi ya kwamba wanapelekea vyombo vinavyotumia umeme kuungua ni hatari kua na watendaji wabovu wao wanachoangalia ni rushwa tu, binafsi nimekuja kutembea lakini nitawamulika vizuri madudu yenu halafu mtajua kama mnafaa au hamfai.
 
Kasulu umeme mnakata mnavyojisikia tena bila taarifa sijui mnakua na maana gani sasa.
 
Eneo la madale - kubali ya ishe umeme mnatuletea lini maana mara kwa mara mnakuja kufanya survey lakin hamna hatua za kuleta umeme wakati eneo la jirani tu mbopo Umeme umefika
 
Hivi tanesco mna mini na wana nnchi wa Chanika na pugu mbona kila siku kero ya kukata umeme tumechoka
 
TANESCO Eneo la Mikocheni baadhi ya maeneo ya umeme mdogo na mengine yako gizani. Taarifa tunaambiwa ati mafundi wanabadilisgani 'shift' tangu saa 11 jioni mpaka muda huu naandika hivi, hawabadilishana tu!! Hapa kazitu kweli?
 
Nafasi za kazi au ajira mbona limekuwa tatizo sugu? Jamani tunaomba mtazame na kero ka hizi@ tanescomwanza
 
TANESCO mnapaswa kutoa taarifa kama kuna mgao wa umeme, au mtoe sababu ya kukatika kwa umeme katika maeneo mengi kwa muda mrefu kwa takribani siku ya NNE leo hii.

Hali hii inarudisha nyuma maendeleo ya wajasiriamali wadogo wadogo katika mkoa huu hasa katika kipindi hiki ambapo uchumi umekuwa ukiporomoka kwa kasi.
 
Kwa taarifa tu zilizopo hali ya umeme itakuwa bora kuanzia mwakani mwezi machi kwa sasa endelea kuvumilia tu mdau mambo mazuri yaja
 
Kweli mtwara kumebadilika huo mji kipindi hicho kuna jamaa wa Umoja light umeme hajuwahi kukatika mtwara hapa naongelea 2013 ,2012 na 2011 umeme ilikuwa 24 hrs, Perhaps mji umekuwa mkubwa sasa supply ni ndogo kuliko demand au Majengo marefu yameongezeka nasikia kuna Tiffany hotel na BoT huko siku hizi
 
Nipo Wilaya ya nyamagana kata ya Butimba,hv karibun umeme umakatwa bila hataa taarifa,ni kama vile mgao ambao haujatolewa taarifa yeyote, Watenda wa siku hizi wanashindwa kusema ata kama kuna tatzo,Wanamuogopa mkuu, kwa taarifa tunaomba mkuu usikie kilio chetu,umeme unakwa hovyo hovyo,nasema ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…