TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kwa zaidi ya miezi miwili sasa tumekuwa na shida ya Umeme kwa baadhi ya nyumba katika eneo letu la Jogoo, Mbezi Juu. Maeneo ya jirani na shule ya Kimataifa ya Breiburn Mtaa wa Mkapa. Umeme unapatikana chini ya masaa saba kwa siku na ukipatikana huwa unakatika na kurudi hadi imepelekea kuunguza vifaa vyetu. Tunahudumiwa na Ofisi ya Tanesco Mbezi Beach na tumekuwa tukitoa taarifa kila mara mafundi wanafika kurekebisha ila tatizo bado halijaondoka. Tumejaribu kutaka kumuona Meneja wa hapo ila anaonekana ana kiburi na hataki kuonana na sisi wananchi ili kujua hatima ya upatikanaji wa huduma katika eneo letu.
Kuna Kijana kafungua studio inaitwa Pluto yupo maeneo hayo nae amekuwa na wakati mgumu kufanya shughuli zake maana huduma ya umeme imekuwa ni changamoto kubwa. Na kibaya zaidi watendaji wa Tanesco hawasemi tatizo ni nini. Tunaomba msaada wenu.
 
TANESCO,Kuna mdau katoa Uzi kulalamikia ufungaji ovyo wa umeme katika Kijiji Cha Hasengo,Shibolya wilaya ya mbeya vijijini.
Hembu fuatilieni muone kazi ilivyofanyika.
Hiyo thred iko huku Ila sijaweza kuiweka hapa.
Hayo tuu
 
Tanesco Kinyerezi Kifuru kuna tatizo gani umeme unakuja na kukata kila baada ya sekunde kumi….shida ni nini? Na hii imeanza tangu asubuhi
 
Hizi mita.zenu mpya za edmi zinakula umeme haraka.sana. ni.kwanini unit moja yaumeme inafikia shs 329 hapa dsm shida iko wapi.

Nani anafanya pricing huko Tanesco. Wananchi tunaumia.sana.chini.ya.tanesco ccm
 
Na

MITA huwa ni muda gani kuletewa baada ya kuharibika ? Nimetoa taarifa ina siku 9 Sasa ..na bado hawajaletwa..kwani ni siku ngapi kuletewa kwake? Wapangaji wananisumbua sana
 
Na

MITA huwa ni muda gani kuletewa baada ya kuharibika ? Nimetoa taarifa ina siku 9 Sasa ..na bado hawajaletwa..kwani ni siku ngapi kuletewa kwake? Wapangaji wananisumbua sana
Habari octavier, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tupatie namba ya taarifa/tiketi kwa msaada zaidi. ^GK
 
Habari, hii imenishangaza, umeme umepanda?

Nina luku ya kawaida, umeme wa 1000 nilikuwa napata unit 8.1, Leo (muda huu) nimenunua mmenipa unit 3.7 how?

24315688788
9002243662059221437
3.4KWH

0857 3904 0936 7749 3263

Cost 819.68
VAT 18% 147.53
EWURA 1% 8.20
REA 3% 24.59
TOTAL 1,000.00

Cc TANESCO
 
Tanesco hoja.yangu ya.umeme kwenda.haraka.na kuisha kupitia mita mpya mnazolamisha kuwafungia watu mbona haijibiwi.

Hizi mita za.dmi zenye box linakaa nje na remote ndani. Mnapunguza kura kwa.ccm.

Tulidhani bwawa la mwl Nyerere likiisha bei ya umeme na.kasi itapungua kuleta.ahueni kwa.wateja.

Nafikiria kuongea na mwabukusi kuhusu hili kisheria nililazimishwa kungolewa mita bila ridhaa yangu. Mita yangu ya.mwanzo niliridhika nayo kabisa.
 
Nilichofanya kiongozi ni kuwapa taarifa kuwa MITA namba flani maneno flani.. wakasema wataleta mda si mrefu
 
TANESCO MTAA WA RAHA NA MUHONDA KARIAKOO TUMEWAKOSEA NN KIKUBWA HIVYO TANGU TRH 14 DEC 2024 KILA SIKU LAZIMA MKATE UMEME HAMJUI TUNATESEKA?
KAMA KUNA JAMBO LILITOKEA TUJULISHENI ILI TUELEWE NAMNA YA KUJITETEA NDG ZANGU!
 
Umeandika kwa hisia Sana.
 
Back
Top Bottom