Huku Endabashi Karatu hakuna umeme toka Jana Usiku.Shida nini wakuu?
 
Habari TANESCO , Nimenunua umeme wiki iliyopita, kutoka kwenye namba yangu ya simu kwa kutumia M-PESA App , kwa ajili ya mita no. 43000128942 wa Tshs 10,000 mara mbili, lakini nilipata tokeni mara moja tu. Mnaweza nisaidia ili nipate tokeni zangu zote?
 
Umejaribu huduma ya jihudumie?
Ama haiapply kwa M-pesa App?
 
Surveyor anatusumbua anahitaji 70000 ili aje ku survey kwa ajili ya kuwekewa umeme.
 
Nashindwa kuelewa, kuna kijiji ambacho watu waliambiwa watoe 70000 kila mtu ili wafungiwe umeme, walipotoa wakafungiwa chap chap. Ambae hakuchanga hakufungiwa. Nauliza hii ni haki na najua unalipa 27000?
 
Umeme wilaya ya Newala ni kero jinsi unavyokatika unapelekea shughuli nyingi kusimama, tunaomba mtusaidie
 
Rekebisheni waya zenu zikaze kwenye nguzo
Waya zimelegea na zipo chini hata ukiandika nguo lazima ziburuzike chini
 
Sasa Hii Account Mrudisheni Yule Jamaa Wa Mwanzo Aliyekuwa Anajibu Swali Lolote Analoulizwa Hapa JF
 
Salamu.Huku Endabashi Karatu siku ya pili leo umeme hakuna.Kuna mgao?
 
Wazo kubwa la kiungwana,Mbarikiwe saana!

Hapa Kigoma,Wilaya ya uvinza, Kijijini Cha mwamila jina maarufu kwa mkuu wa mkoa, TRANSFORMER yake Ni pasua kichwa,mashine za kusaga na kukoboa zikiwashwa umeme unakuwa mdogo hivyo majumbani lazm umeme ukate mpk wamalize kusaga ndipo umeme urudi majumbani.....

Kama Tanesco haiwezekan kubadilisha transafo inayoweza kuhimili mzigo na mkawa mmepunguza adha hii kwa wateja wenu???

Naomba kuwasilisha
 
vp nimeomba kuunganishiwa huduma ya umeme,nguzo ipo karibu lakini Sasa ni zaidi ya siku 7 sijaunganishiwa umeme Tanesco nyakato nimelipa kwa control number, mwanza. Naomba msaada au maelekezo
 
UNGENI MFUMO WA MOJA KWA MOJA MTEJA AKINUNIA LUKU KUSIWE NA HAJA YA KUTUMIA MASHINE BALI UMEME UUNGWE MOJAKWAMOJA.
Ahsante
 
WAPENDWA za UZIMA WOTE polen na kazi

KUNA mtr Ina mwezi na mpangaji wangu amejiwekea

Leo asbh ameamka anakuta Nje hamna LUKU

Nawaza huyu mtu nani amewezaje kuitoa hii LUKU

Na JE tumeripoti tanesco ataweza kyitumia??

Na nn kifanyike

Asante kwa mawazo YENU tufanyaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…