HILI JUKWAA BADO LINAFANYA KAZI AMA NDIO WALEWALE TUOMBE WALITOE KABISA MAANA NAONA KAMA WANAISHIA KUSOMA SHIDA ZETU WANACHEKA
 
Kwanini maeneo ya Temeke , Keko, Changombe na Tandika tunakatiwa umeme kila nara na hakuna sababu wala notification.
Tatizo hili ni la muda mrefu kwa zaidi ya miaka 5 hatuna umeme wa uhakika
 
Kijiji cha kwasekinga kata ya miamba wilaya ya same ,tangu mwaka jana mwezi wa tisa mlileta nguzo na nakuziweka kweny mashimo nakufunga nyaya ,ila hadi leo nikama mradi wakuunganishiwa majumbani imekua ngumu,tukiuliza tunaambiwa mradi ulikuja kisiasa kwajili ya uchaguzi wa serekeli za mitaa ,hamuoni kua mnaichonganisha serekali na wanachi ,? Tunaomba muwangizie wananch umeme majumbani ili kuondoa kero hii,
 
Imekuwa ni kawaida kila siku kuanzia saa moja usiku, umeme Huwa unakatwa eneo la Maji Matitu, TANESCO kuweni wawazi mtupe maelezo kwa Nini kila siku tatizo husika linatokea?
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.​
Nendeni mkajibu thread huko

 
Hatutaki umeme kutoka Ethiopia wala Kenya, Tunataka Umeme wa Bwawa letu.
 
Nyie Tanesco Geita Dc kama mnakata umeme kateni tujue moja habari za kukata kurudisha dakika moja mnakata hata mara mbil au tatu na kurudisha siyo poa
Kama mnakata kateni tujue umeme umekata siyo kukata kurudisha kukata kurudisha haijakaa poa
By the way:kuanzia mwezi wa 12 hadi huu wa 3 hapo nyuma mmefanya vizuri na nimepata faida ya kutumia umeme wenu hongereni kwa hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…