TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Pia kama Tanesco mmeshindwa mseme ili wananchi waingilie kati kununua waya mjemfunge tu.
Tumefatilia zaidi ya mara 15
 
Nguzo ambazo zimedumu kwa miaka mitatu sasa bila waya sijui tatizo ni waya au tatizo ni nini hata sijui.
Kijiji cha kwekitui kata ya Mamba wilaya ya Lushoto.
Zitaliwa na mchwa hizo nguzo kisha mtaambiwa mnunue nyingine
 
Mimi ni mkazi wa kwembe mpakani wilaya ya ubungo
Tuliomba Mradi wa umeme wa nguzo Tisa mwaka 2015 idadi yetu sisi waombaji ni kumi na wawili (12
Tumesubilia Mradi Kwa muda mrefu Sana zaidi ya miaka 2
Mradi umetoka mwezi wa Tano 2017
Nguzo zimeletwa site tokea mwezi wa sita mbaka hivi sasa ninaongea humu nguzo zimetelekezwa chini Sisi Kama Wateja watarajiwa WA Tenesco tupo njia panda atujui ni lini huu mradi utakamilika
hama Tanesco makao makuu mnatushauri tuchukue hatua zipi, ili na Sisi tuupate umeme.
Nakumbushia ombi langu naona sjapewa jibu
 
TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA.

NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
Napenda kuwapongeza TANESCO hasa ofisi ya Kimara kwa response ya haraka unapotoa taarifa kupitia emergency call pamoja na ile customer relations.

Nina tatizo moja, kwanini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara hasa ktk mtaa wa Mloganzila?
Hali hii sasa ina zaidi ya wiki, na huwa hakuna taarifa zozote zinazotolewa kuhusu katizo hili.

Tunapenda kujua tatizo ni nini na litaisha lini?
 
Mimi ni mkazi wa kwembe mpakani wilaya ya ubungo
Tuliomba Mradi wa umeme wa nguzo Tisa mwaka 2015 idadi yetu sisi waombaji ni kumi na wawili (12
Tumesubilia Mradi Kwa muda mrefu Sana zaidi ya miaka 2
Mradi umetoka mwezi wa Tano 2017
Nguzo zimeletwa site tokea mwezi wa sita mbaka hivi sasa ninaongea humu nguzo zimetelekezwa chini Sisi Kama Wateja watarajiwa WA Tenesco tupo njia panda atujui ni lini huu mradi utakamilika
hama Tanesco makao makuu mnatushauri tuchukue hatua zipi, ili na Sisi tuupate umeme.
 
Tafadhali fika ofisini kwa maelezo zaidi
 
Hizi mita zenu mlizofunga kwenye nguzo ni kero sana Mimi Nina saloon huku Bunda hadi nimechoka kuja kuripoti make ile nikipachika drier tu Umeme unakata sasa sijui tatizo ni nini na hata nikiripoti inachukua siku 2 mpaka 3 kufika ofisini Kwangu kunirekebishia!

Inakuaje hapa tanesco hizo mita zenu au zina matatizo???

Wenu mteja
Bunda
 
Hizi mita zenu mlizofunga kwenye nguzo ni kero sana Mimi Nina saloon huku Bunda hadi nimechoka kuja kuripoti make ile nikipachika drier tu Umeme unakata sasa sijui tatizo ni nini na hata nikiripoti inachukua siku 2 mpaka 3 kufika ofisini Kwangu kunirekebishia!!
Inakuaje hapa tanesco hizo mita zenu au zina matatizo???

Wenu mteja
Bunda
Je leo hauna umeme? Kama ndio tunaomba namba yako ya simu na eneo lako
 
Nataka kuuliza je kama umegundua kama kuna ajari ya moto kuunguliwa kwa nyumba na mkajua chanzo ni hitiliafu ya umeme na kampuni yenu ikahusika katika kusababisha tatizo hilo je mtalipa na kama mtalipa kwa kipindi gai na mpo tayri kurekebisha huduma zenu kwa majumbani
 
Je leo hauna umeme? Kama ndio tunaomba namba yako ya simu na eneo lako
Mpaka dakika hii sina Umeme Nina zaidi ya wiki moja nimekata tamaa hata kuripoti
Mita iko nyasura stendi kwa Mzee EMA Jirani na kwa mpyampya.
 
Nataka kuuliza je kama umegundua kama kuna ajari ya moto kuunguliwa kwa nyumba na mkajua chanzo ni hitiliafu ya umeme na kampuni yenu ikahusika katika kusababisha tatizo hilo je mtalipa na kama mtalipa kwa kipindi gai na mpo tayri kurekebisha huduma zenu kwa majumbani
Taratibu unaandika barua huku ukionyesha vitu unavyodai vimeungua kutokana na ubachosema ni umeme kisha timu ya wataalamu itachunguza na kutoa taarifa kuwa nin kimepelekea moto kutokea kisha kama ni sisi utaratibu upo yaani wajibu wa TANESCO kwa mteja
 
Asante vp kuboresha huduma huku mbagala eneo la viwanda
 
Taratibu unaandika barua huku ukionyesha vitu unavyodai vimeungua kutokana na ubachosema ni umeme kisha timu ya wataalamu itachunguza na kutoa taarifa kuwa nin kimepelekea moto kutokea kisha kama ni sisi utaratibu upo yaani wajibu wa TANESCO kwa mteja
Unapoomba umeme kuna masharti kwenye fomu ya maombi sisi tunaita mkataba na mteja wengi wetu hatusomi vile vipengele ikitokea hitilafu vitu vikaungua ndio unakosa haki yako kwa kuwa hukufata mkabata uliosaini
 
Back
Top Bottom