Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hadi kwa mlompa kura mkulu? Amakweli itafika muda tutashea maumivu tu.Huku Mwanza UMEME hakuna tangu asubuhi na hatujapata maelezo yoyote pia MAJI imekuwa ni kawaida kukatika kila siku wakati Ziwa tunaliona hapo na hakuna maelezo yoyote kwa nini hakuna maji, yaani hizi taasisi mbili ni pasua kichwa sijui hivyo viburi wanavitoa wapi..!!
Pia mtulipe kutokana na huo usumbufu.... Sio kuomba radhi kila siku.... Maana hamkutupa taarifa mapema.... Sisi mbeya ususani kyela umeme unarudi kama tulivyo uzoea yan kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi kuanzia sa moja jioni na mda mwingine sa tano usiku ni mwezi sasa.SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
*TAARIFA YA KUANZA KUREJEA KWA UMEME *
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa umeme umerejea katika Mikoa yote Saa 07:11 Mchana isipokuwa Mkoa wa Mbeya kutokana na hitilafu iliyopo katika njia ya Mufindi.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka
Kwa mawasiliano zaidi
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
01/12/2017
Tuna redio na TV niwajibu wao kututangazia kumbukua hii huduma sio bure tunatoa pesa zetu.... Na tumegharamia na bado pesa zetu wanachukua....Ni taarifa ipi ambayo hujaipata. Tanesco wametoa taarifa za hitilafu za umeme wewe unasema huna taarifa. Jitahidi kufuatilia taarifa sahihi katika ofisi za mkoa wako.
Mheshimiwa Mbunge wa Ilemela huu mgao wa jimboni kwako stuka, iweje buswelu nyamanoro nyakato pasiwe na umeme wiki ya tatu sasa, kila siku mchana hakuna umeme, sasa wachoma mageti waranda mbao wauza juice hawana kazi, zimebaki bar t
hebu dadisi chunguza kwanini ni ilemela tu ha
Ukabila mkuuu na ukwetu kwetu... Si wasukuma hao wanahisi kama umeme ni haki yao pekee maana nchi ni yao.. Wamejisahau sanaa.... Mwambie amfuate kwa office yakeNa wewe Eddy acha ufala, hapa jukwaani kuna post zaidi ya tatu zote zinazungumzia tatizo la umeme nchi nzima, wewe unakuja kumuuliza mbunge kuhusu hizo sehemu tatu?
Suala la umeme si kwamba lipo mwanza tuu ni kwamba kwa mikoa yote iliyounganishwa na grid ya taifa umeme unasumbua hakuna mgao ila ilitokea hitilafu katika msongo mkubwa wa umeme ndio maana umeme ulikuwa unasumbua..!!!
Suala la umeme si kwamba lipo mwanza tuu ni kwamba kwa mikoa yote iliyounganishwa na grid ya taifa umeme unasumbua hakuna mgao ila ilitokea hitilafu katika msongo mkubwa wa umeme ndio maana umeme ulikuwa unasumbua..!!!
Eti matamko ndo yatamaliza matatizo tuliyonayo ikiwemo hili la Umeme? Unaota wewe. Mmebaki kuangalia kila kitu kwa jicho la ushabiki. Na bado, for you deserve all the shit.Mambo kama haya Chadema ndo yalipaswa kuyatolea matamko, lkn kwenye matatizo ya msingi ya watanzania Chadema hujificha, ila akikamatwa Heche polisi, hayo matamko utakayoyasikia sio ya Nchi hii
Masasi laini ya mangaka haujawahi kuwaka masaa 24 hata kwa siku mojaWakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.. Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k
Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?
Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?
nchi ya viwonder