TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Bora wasiurudishe kabisa tu kama lengo lenyewe ndo hilo angalau kama akili zinaweza kuwarudia japo kidogo!
 
Ndugu mpendwa mteja
Tunakuomba radhi sana pamoja na hayo tunakujulisha kuwa kuna kipindi cha mvua hivyo hitilagu zikiwa nyingi tunahudumia kwa kwanza kutoa taarifa wa kwanza kufanyiwa kazi

Mjifunze customer care. Jitahidini kumlizisha mteja kwa kauli na ahadi mnazompa pia mtambue kila mteja wenu kwenu ni muajiri.

Lakini pia ukishakubali kuwa Meneja wa kituo jaribu kupokea simu na kumuattend mteja inawezekana hakulidhika na majibu ya vijana wako. Unapoona hilo ni gumu kwako omba kupumzika au kufanya kazi chini ya mtu. Cheo ni dhamana.

We need good service, make sure we get the real value of our money.
 
Mgao upo jamani, hali ya maji mtera, kidatu, kihansi si nzuri na production imeshuka sana. Private sector ndiyo hivyo tena serikali imeipiga kibuti, hakuna Symbion wala IPTL. Nchi haina reserved power sources, load kila siku inaongezeka na vituo vingi vya thermal (Gasi na mafuta) na kile cha Nyakato-Mwanza vinazalisha chini ya uwezo wake sababu ya ukosefu wa vipuri. Tuna kazi kubwa kweli.
Vipi Arusha hali ikoje uko??
Tatizo ni umaskini jeuri wetu! Tuwapatie mkataba mpya IPTL, Symbion, mgao utaisha!
 
Poleni kwanza kwa magumu mnayopitia ktk kuhakikisha mnawapatia nishati ya umeme watanzania.

Tangu nimeanza kupata akili mpaka sasa naufukuzia muongo wa tatu ktk maisha yangu sijawahi kuona mwaka umepita bila matatizo ya umeme nchini kwetu hii nadhan sabab za msingi mnazo wenyew maana mara nyingi huwa znafanana sasa sijui kwanini hamzitibu kikamilifu.

Kuanzia mwisho wa mwezi wa 11 tumeshuhudia kukatikakatka kwa umeme katika maeneo mengi sana kupelekea wananchi kupata hasara kwa namna moja au nyingine.

Ninachowashangaa sana ni kwanini hamtoagi taarifa ya kueleweka kwamba tatizo liko hivi na litatuliwa baada ya muda kadhaa kiasi kwamba mkatufanya wananchi tuwe aware na huo usanii wenu. Wiki iliyopita nimeenda ferry nimechukua misamaka kibao kutia kwenye friji ili inisukume sukume leo hii imeshaoza maana umeme hamna na ukirud unakuja lisaa limoja unakatka.

Ukiachilia samak wangu vitu vingi vilivyokua kwenye friji vimeharibika dah. Sio mimi tu watu wengi wanalia the same issue. Badiliken mnatuumiza jaman dah!!!
 
Kama mtaalamu wa Mambo ya technology leo nimekuja na Ushauri Huu kwa Tanzania electrical supply company(TANESCO)
Umeme sio luxury miaka hii, Umeme ni hitaji la lazima la binadamu kwa sasa yani basic need, Tunahitaji Umeme kusonga mbele kuendesha Viwanda, Kuhifadhi vyakula na Asilimia kubwa ya biashara kama sio zote zinahitaji umeme, Tunahitaji umeme kuwasiliana,Tunahitaji umeme Kuwa updated Yani umeme ni hitaji ambalo tunalihitaji moja kwa moja bila Ubabaishaji.

Shirika letu TANESCO linazalisha wastani wa MW 1740 Kwa sasa kupitia Thermal na Hydro na Heavy fuel Oil, MW hizi si toshelezi sana ila zinatufaa huku tukisubiri project kubwa kama za singinda Wind na ingine uko ruvuma ya hydro. Umeme unapitia stage tatu mpaka kumfikia end user yani consumer kuna Generation, Transmission na Distribution kati ya hao watatu mwenye shida sana ni Distributor watu wa Generation na Transmission wako firm sana kuanzia miundombinu, Nikisema Transmission hapa nazungumzia Grid yani interconnection kati ya mikoa na mikoa kupitia msongo wa kuanzia 66kv mpaka 220Kv, Hao unaona ata usafirishaji wao wa energy hii hutumia Metal tower kitaalamu tunaita Pylons hizi nguzo za Chuma ni very strong na ni ngumu kupata Breakdown kwenye hizi grid.

Distributor hapa ndio unawaface zaidi wale local tanesco wa wilaya wao wanachukua power kutoka ktk substation na kutupa sisi end user hawa wana miundo mbinu mibovu mno Line zao huanzia 33 na 11 Kv na ni za mbao, kweli kabisa tunasafirisha umeme na nguzo za mbao??? Unafukia mbao kwenye udongo nini unategemea ni bora tuingie gharama kubwa ya Kujenga nguzo za Zege kwa line za 11 na 33kv kwanza pia 11kv kwa sasa tuziache hazina efficiency tutumie 33kv tupu kwa local feeders na Ziwe structured na concrete yani Zege Hii itaondoa Temporary breakdown na replacement tunazofanya frequently kwenye Wooden pole,

33kv zikishakuwa scattered kwenye lets mkoa au wilaya basi LV line tutumie Insulated cable na mtaani zikatize Metal Pole yani Viguzo vidongo vya Chuma kwa ajili ya kubeba LT cables huku tukiangalia future ya underground ambapo ndio inatumika ktk developed countries kwa miji iliyopangika basi tuanze ku implement Underground system kabisa nakumbuka former Minister of Energy and minerals Hon Sospepter muhongo alisema kufikia kipindi fulani hatutaona cable hata moja Juu kwa Dar es salam all electrical system will be undergrounded hii alitamka waziri alietoka hivo hali iendelezwe na aliyopo sasa.
 
Tanesco kulikoni mlifika Eneo la Igombe B mkagungua Eneo kubwa la Mtaa huu hatujafikiwa na huduma ya umeme ,Mkaanzisha kanda Igombe c mkadai tutapata huduma ya umeme sio mda mrefu yapata mwaka na miezi kimya umetuachaje gizani hatujaletewa huduma ya umeme?
 
Hadi muda huu @19:18
Tanesco wamegoma kurejesha umeme wao yaani vurugu tupu sijaingiza hata 100 tangu asubuhi

Ifike muda sasa TANESCO waweke mikataba baina ya wateja na wao
Nimelipia units za kutosha kwenye mita yangu nikiamini sasa kazi tu nisidaiwe na TANESCO kumbe wameniingiza mkenge

OMG
 
TANESCO , kwa hivyo umeme tutegemee kurudi saa ngapi(nipo Dar)? Mngeweka utaratibu wa kutoa updates mara kwa Mara ili mtuwezeshe wateja wenu ku plan shughuli zetu.
 
Kama mtaalamu wa Mambo ya technology leo nimekuja na Ushauri Huu kwa Tanzania electrical supply company(TANESCO)
Umeme sio luxury miaka hii, Umeme ni hitaji la lazima la binadamu kwa sasa yani basic need, Tunahitaji Umeme kusonga mbele kuendesha Viwanda,Kuhifadhi vyakula na Asilimia kubwa ya biashara kama sio zote zinahitaji umeme, Tunahitaji umeme kuwasiliana,Tunahitaji umeme Kuwa updated Yani umeme ni hitaji ambalo tunalihitaji moja kwa moja bila Ubabaishaji. Shirika letu TANESCO linazalisha wastani wa MW 1740 Kwa sasa kupitia Thermal na Hydro na Heavy fuel Oil, MW hizi si toshelezi sana ila zinatufaa huku tukisubiri project kubwa kama za singinda Wind na ingine uko ruvuma ya hydro. Umeme unapitia stage tatu mpaka kumfikia end user yani consumer kuna Generation, Transmission na Distribution kati ya hao watatu mwenye shida sana ni Distributor watu wa Generation na Transmission wako firm sana kuanzia miundombinu, Nikisema Transmission hapa nazungumzia Grid yani interconnection kati ya mikoa na mikoa kupitia msongo wa kuanzia 66kv mpaka 220Kv, Hao unaona ata usafirishaji wao wa energy hii hutumia Metal tower kitaalamu tunaita Pylons hizi nguzo za Chuma ni very strong na ni ngumu kupata Breakdown kwenye hizi grid.

Distributor hapa ndio unawaface zaidi wale local tanesco wa wilaya wao wanachukua power kutoka ktk substation na kutupa sisi end user hawa wana miundo mbinu mibovu mno Line zao huanzia 33 na 11 Kv na ni za mbao, kweli kabisa tunasafirisha umeme na nguzo za mbao??? Unafukia mbao kwenye udongo nini unategemea ni bora tuingie gharama kubwa ya Kujenga nguzo za Zege kwa line za 11 na 33kv kwanza pia 11kv kwa sasa tuziache hazina efficiency tutumie 33kv tupu kwa local feeders na Ziwe structured na concrete yani Zege Hii itaondoa Temporary breakdown na replacement tunazofanya frequently kwenye Wooden pole,

33kv zikishakuwa scattered kwenye lets mkoa au wilaya basi LV line tutumie Insulated cable na mtaani zikatize Metal Pole yani Viguzo vidongo vya Chuma kwa ajili ya kubeba LT cables huku tukiangalia future ya underground ambapo ndio inatumika ktk developed countries kwa miji iliyopangika basi tuanze ku implement Underground system kabisa nakumbuka former Minister of Energy and minerals Hon Sospepter muhongo alisema kufikia kipindi fulani hatutaona cable hata moja Juu kwa Dar es salam all electrical system will be undergrounded hii alitamka waziri alietoka hivo hali iendelezwe na aliyopo sasa.
Shukrani
 
Naomba mawazo yenu kwa tatizo hili: natumia unit 8 kutwa.

Nina frigdge moja ndogo, taa energy saver kama 5 zinawaka saa 12 a day, tv mbili zinatumika kama saa 5 a day, . Nadhani unit 8 a day huu ni umeme mwingi ninao tumia.

Tatizo linaweza likawa wapi? Nimeleta fundi akacheki wiring akasema iko vizuri.

Ushauri tafadhali.

Asante

Utakua umelogwa! Mtafute mtaalamu wa kimila
 
Nimenunua umeme lakini sijapata token:-

Namba ya simu :- 0765371753
Namba ya mita:- 54130511071
Kiasi:- 9100/=
Tarehe 03/12/2017
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MAENDELEO YA MATENGENEZO YA DHARURA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KINYEREZI I

Tunawataarifu Wateja kuwa Wataalamu wetu bado wanaendelea na kazi Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Kinyerezi I.


Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

31/10/2017

Hivi shinyanga tatizo ni nini mgao au maana imekuwa too much
 
Daaah!!! Hakuna kitu mnakera kama kukata umeme vyuoni na mkiwa mnajua hakuna kazi inayoandikwa na mkono huwa mnatuumiza sana na huku mmeptia badliken bhana
 
Back
Top Bottom