TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco Tanesco Kimara Baruti no umeme tokea saa nane usiku vitu vinatuharibikia kwenye friji na sikukuuu hii mnatutia hasara,kuna nn Tanesco?..
Mjomba,tanesco ni shirika la hovyo lililobak la serikal,na wao wanajua hilo.so kiukwel tuwaombee tuu kwa Mungu,

Wengne tumeamuaga ku go with the flow,wakikata tunawasha generator maisha yanasonga,
 
Mjomba,tanesco ni shirika la hovyo lililobak la serikal,na wao wanajua hilo.so kiukwel tuwaombee tuu kwa Mungu,

Wengne tumeamuaga ku go with the flow,wakikata tunawasha generator maisha yanasonga,
Wanachefua sana mkuu,yaani basi tu.
 
Kama tulivyosia umeme umeshuka bei kwa wateja Wa ndani ya mita 30,bei ni 27000.vipi sisi ambao tunahitaji nguzo bei ni kiasi gani ,majibu tafadhali
 
Naomba kujua REA bado ipo au mradi umekamilika?Huku Simiyu wilaya ya Busega kuna maeneo tumeeekewa nguzo za REA tangu mwaka jana ila hadi sasa hatujapata umeme na hatujui kinachoendelea
 
Nahisi huu mradi umekamilika kama siyo kuwa umeisha kabisa maana ni hatari pasua kichwa
 
Du,nadhani tujipe moyo tu mambo yatakuwa mazuri
Ndugu yangu mimi ni mhanga wa kuitafuta REA kwa udi na uvumba lakini naelekea kunyoosha mikono, siku mh Medard Matogolo Kalemani akiamua nitapata tofauti na hapo sina namna.... Tanzania inawenye nayo hakika....
 
Salaam, samahani naomba zile link za whatsapp za Mkoa wa Kagera tafadhali yaani zile zilizo tolewa na tanesco
 
Inahuzunisha Sana mimi nikiwa Mteja tena wa miaka mingi nipo gizani leo siku ya tatu tena hapahapa mjini dar ,ninashida Mita yangu imetemper wakati naingiza token, sipati picha shida hii uipate kijijini nadhani utasahau na umeme wenyewe,naomba Sana tanesco hata kama hamna mshindani muwajali wateja ndio wanawawezesha kufanya mnayofanya,
 
Sector nyeti na mbovu na yenye dharau na wingi wa rushwa ni Tanesco. Pia kwanini Muheshimiwa asiifanyie hii sector ziara za kushtukizia kwanzia aingie mjengoni?
 
Katika kijiji cha Sawala Mufindi tunaomba mtuongezee nguvu ya umeme hasa eneo la Kalinga umeme ni mchache sana vifaa vyetu vinaungua.
 
Tatizo la Kuunganishiwa Umeme Kwa wananchi wa Chanika - Mgeule juu limekuwa ni tatizo la kudumu.

Pamoja na jitihada za ufuatiliaji wa Mara Kwa Mara back jambo hill limekuwa gumu bila sababu yoyote.

Rais aliagiza Managers Msikae to ofisini, tafuteni wateja, limekuwa Ngumu kwenu. Tumetumia Muda na kufufanya ufuatiliaji wa Karibu, badala take ni kugeuza Maneno kila uchwao.

Ngazi inayofuata tusaidieni katika hili.
 
Inabidi uwataarifu kwenye thread yao au uwatag TANESCO walifahamu hili suala
 
Tanesco Kimara jamani Goba hasa Tegeta A kuna nini ???? Mbona umeme unakatika kila siku Mara 3?? Yaani kila siku
 
Naomba kuuliza.
Niliomba kuunganishiwa umeme,na ilichukua muda zaidi ya miezi mitano, ndo wakalietea nguzo.
Sasa ni zaidi ya wiki tatu zimeita, nguzo iko hapo chini hawajaisimamisha, kila ninapo wauliza wananiambia tutakuja kesho au kesho kutwa kuweka nguzo na kukuunganishia umeme.

Je nisubiri mpaka lini?
 
Kusema ukweli TANESCO hamna customer care hata kidogo. Kuna emergences zinatokea kwa mfano Dar es salaam umeme unakatika mtu unapiga simu hazipokelewi na hata wakipokea mafundi hawaji mpaka kesho yake.

Imagine Kinondoni kulala bila umeme na joto la Dar es salaam. Hii namba 0784768584 unaweza ipiga haipokelewi hata kwa masaa. Rekebisheni huu uzembe very seriously.

Hivi mmeshawahi kufikiria ni hasara kiasi gani au ni mapato kiasi gani kwa shirika endapo umeme ukikatika hata saa moja tu tena kwa uzembe tu wa lose connection kwenye nguzo? Badilikeni mfanye kama biashara na msifurahie umeme kukatika kwenu ni hasara kubwa kuliko hata kwa mteja mwenyewe.

Dar tunaishi kwa budget. Tunanunua chakula mara moja kwa mwezi so ukinikatia umeme kwa masaa 20 mpaka 40
umeamua kuniua kwa kuwa chakula changu kinaharibika na sina uwezo tena. Rekebisheni hilo jamani.

Umeme ukikatika basi kiwe na sababu ya msingi na mkiitwa mje haraka siyo baada ya masaa 20 mpaka 40. Response yenu isizidi nusu saa.
 
Back
Top Bottom