TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Vishoka Tanesco Dar es salaam (Kituo husika nakihifadhi kwa sasa) wanasumbua wateja. Huwezi kumpata surveyor bila kupitia kwa kishoka. Control number bila kupitia kwa kishoka utaambiwa mtandao unasumbua, ukipitia kwa kishoka ni siku moja tu unapata. Kuunganishwa umeme kawaida inachukua 30 hadi 60, ukipitia kwa kishoka siku mbili tu. Hivi huu mchezo mtaundekeza hadi lini?
Tunaomba namba yako ya simu inbox kwa hatua zaidi tafadhali
 
Naomba msaada nimefungiwa umeme siku tutu zimepita nikitaka nunua umeme naambiwa hii namba ya mita haipo nifanyeje?
 
Tunaomba namba yako ya simu na namba ya mita, wilaya tafadhali
 
Hallow Tanesco Njombe,Hivi kwa nini mipango yenu ya matengenezo ni siku ya Jumamosi tu?
Ndo kusema mmelenga kutupa taabu sisi watumishi wa umma tunaopata nafasi siku ya Jumamosi kufanya shughuli zetu za uzalishaji?
 
Hallow Tanesco Njombe, hivi kwa nini mipango yenu ya matengenezo ni siku ya Jumamosi tu?
Ndo kusema mmelenga kutupa taabu sisi watumishi wa umma tunaopata nafasi siku ya Jumamosi kufanya shughuli zetu za uzalishaji?
 
Jamani mpaka inaboa, umeme wanakata masaa 20 ukipiga nguzo imeanguka, haya mara kuna tatizo linashughulikiwa . Haiwezekani maeneo hayohayo yakapata matatizo ndani ya wiki moja. Vitu vyetu vinaharibika.

Lazma kuna uzembe. Tunaomba Manager wa kituo cha TANESCO Tegeta ajitafakari.

Miundombinu ya umeme maeneo ya Boko, Ununio sio mibovu hivyo kusingizia kwa ndiyo sababu.

Manager fanya kazi yako. Kama sio wewe, supervisors wako wanakuangusha, tena wa shift za usiku. Kwa nini matatizo yanatokea usiku tu?
 
Tunashukuru kwa taarifa mpendwa mteja wetu tunaifanyia kazi
 
Wadau mtu ambaye ameandika barua inayohusu jinsi ya kulipia service line nguzo mbili anicheki inbox ili na mm nidese barua hiyo nimfuate manager wa eneo langu. Maana huku nilipo kunapigo za kishamba, ambao hatupo kwenye mradi wa REA hatupati umeme hii siilewi kabisa yani tunabaguana hata kama unahela ya kulipia umbali wa nguzo mbili, yani bora nilipie majirani waingize umeme kuliko kununua misola hii.
 
Tanesco mnanikwaza sana..mlinibadilishia mita mkaweka luku ..sikua na deni zaidi ya billi za kawaida na nikalikipa.mwaka mzima napata umeme safi ..mwezi wa kumi na moja mwaka huu mmeanza kunikata 5000 kila ninapo nunua umeme..yaan ilo deni linatoka wap??yaan mnanikara na ukipiga simu unaambiwa una deni.kwa nini hamkunipa taharifa kamanina deni na kwa nini muanze kunikata mwezi huu kama kuna deni??ina maana bili tulizokua tunalipa kila mwezi kwenye crdb na zile control number zilikua feki??
 
Tunaomba namba yako ya simu inbox kwa hatua zaidi tafadhali
Hapa nimeandika ili mpeane tahadhari nyinyi kwa nyinyi kabla hamjakutana na vichwa maji wakawaitia takukuru. Pesa yenyewe hata haizidi Tzs 50,000/, sijui wanagawana bei gani na hao vishoka. Yaani msomi mzima anageuka mtumwa wa kazi za kishoka zenye tip ya Tzs10,000?
 
Tunaomba ushirikiano wako kwani kutoa tuhuma bila ushirikiano ni kushindwa kusaidia kutatua tatizo.Tunaomba taarifa kamili maana wakati mwingine mnakutana na vishoka mtaani mnaandika na kutuchafua kwanini usiwe muwazi hatua zichukuliwe?
 
Habari ya jpili ndugu watanzania wenzangu?
Ni kipindi sasa, tangu Tanesco waanze kutoza gharama nafuu za kuingiziwa umeme kwa vijijini REA.
Vijijini wanatoza Tshs. 27,000 tu. Hoja inakuja wa mijini.
Gharama ni kubwa sana. Zaidi ya ×25 ya wale wa vijijini.
Watanzania wote ni sawa.
Kwa nini kuwe na utofauti wa gharama kubwa kiasi hicho.
Sawa tunajua mradi wa Rea umefadhiliwa na wazungu .
Kama ndio hivyo,kuna haja serikali iwafadhili wa mijini nasi tuweze kuingiza umeme japo kwa elfu 27 pia.
Au sisi tuishio mijini sio watanzania?
Wananchi tunatakiwa tuwe pamoja kwa hili.
Tupaze sauti iwafikie wahusika.
Wangapi wanaunga mkono hoja?
 
Tunapenda kukujulisha kuwa miradi ya REA inawesezeshwa na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, pili maeneo yote ya vijiji iwe REA au vingenevyo wateja wote wanalipia tsh 27000 tu.
 
Hoja yangu ni kuwa kwa nini mijini gharama zipo juu.
Mfano, bila nguzo ni laki 3.21 lkn kama kuna nguzo 1 ni laki 5.21
Je hamuoni huo ni ubaguzi kati ya watanzania wa mijini?
 
Nipende kutoa masikitiko makubwa kwa shirika la Tanesco kanda ya kusini, hususani mkoa wa Mtwara.

Kwa takribani wiki ya pili sasa umeme umekua ukikatika kila mara, kwa siku waweza kukatika hata zaidi ya mara 20.

Kusema ukweli mna katisha juhudi zetu wananchi katika kujikwamua kiuchumi. Pia, mnakwamisha juhudi na mipango ya rais wetu kufikia uchumi wa viwanda.

Mana kazi zote zinazotegemea umeme ili kufanya uzalishaji zimesimama. Watu wanaunguza mshine na vitendea kazi vyao. Hivi mnatutakia nini sisi wana kusini?

Cha ajabu hata taarifa hamtoi kwa wananchi, kama umeme unashida si mzime moja kwa moja mpaka utakapo tengamaa ndipo muwashe kuliko hii zima washa.

Najua waziri wa nishati upo humu tunaomba utembelee Mtwara ili uone shida nini hasa ikibidi utumbue majipu. Wananchi tunateseka, umeme Mtwara imekua kerooooooo.

#MaendeleoHayanaChama
#TanzaniaYaViwanda.
#RaisWaWanyongeSikiaKilioChetu.
 
Naona mods mmeamua kuunganisha huu uzi..haya TANESCO mje mjibu.

Mitaa yetu ya Msasani Kila siku umeme unazimika

Juzi umeme umerudi saa tisa usiku jana saa 10 jioni leo asubuhi hii saa tatu umezimwa

Kwa mfanyakazi wa tanesco ambae anasoma uzi huu kama anamajibu basi atujulishe
 
Me mwenyewe nko mitaa ya General tyre hapa nashangaa ni majenereta tuu Yana nguruma ....dah Yan cyo pouwa
 
Back
Top Bottom