Apa ninavyotoa haya malalamiko umeme umekatika tokea jana haujarudi na hiyo ni kawaida ya umeme wa huku yani unakatika masaa 12 unawaka masaa 2 au nusu saa unakatika tena wenyeji wa hapa wanasema tatizo hili lilianza mara baada ya kubadili chanzo cha umeme kutoka wa mafuta na kuanza kutumia umeme wa gesi kuna jamaa yangu yupo UTP(hawa ni km wanawasaidia TISS) anasema aliwahi kwenda ktk ofisi za tanesco kufanya uchunguzi akaniambia pale kuna tatizo sio tu suala la umeme wa gesi lkn hakunieleza kwa undani,
TANESCO Liwale tunaomba mtupe majibu yanayoeleweka kwnn umeme haueleweki huku Liwale kama tatizo ni gesi kwnn msiturudishe kwenye umeme wetu wa uhakika kwnn muingie ktk biashara msiyoiweza ya kutumia gesi ilihali mnajua kuwa hamuuwezi km tatzo ni wafanyakazi au mabosi tunaomba mkuu wa wilaya uliangalie hili kwa umakini kwani tunateseka sn wakazi tunapata hasara mno vitu vimekua vikiungua kutokana na waka zima hii.
Nawasilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app