Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanesco huku chalinze tangu jana jioni mpaka sasa hatuna umeme simu zinaishiwa chaji vitu kwenye friji vinaharibika tatizo ni niniView attachment 498143
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.
Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;
1. ENEO HUSIKA
(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)
2. NAMBA YA SIMU
(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)
3. KARIBU NA NINI
(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)
4. JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO
(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)
5. MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI
(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)
6. KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME
(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)
7. KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI
(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)
TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.
ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO
Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;
Poleni sana, robot litawajibu sasa hivi, uko wilaya gani, tupatie namba yako ya simu.😅Tanesco huku chalinze tangu jana jioni mpaka sasa hatuna umeme simu zinaishiwa chaji vitu kwenye friji vinaharibika tatizo ni nini
Ndugu mpendwa Mteja wetujamani mimi ninashida kwenye mita yangu ni siku ya tano leo hakuna umeme,lakini kwenye king'amuzi unit zipo za kutosha sasa sielewi shida ni nini.
Acha kupotosha tafadhali wanaotoa taarifa kamilo watakuwa mashahidi wanapata hudumaPoleni sana, robot litawajibu sasa hivi, uko wilaya gani, tupatie namba yako ya simu.[emoji28]
Everyday is Saturday................................[emoji41]
Mteja hanunui CIU maarufu kama remote bali atawajibika kuilipia kama ameiharibu yeye mwenyeweNaomba kufahamu, je rimoti ya kuwekea luku inapochakaa au kuharibika, mteja anatakiwa kununua mpya?
View attachment 1749362
Ahsante, nimekuelewa. Yangu haikuharibiwa imetokea tu ile screen yake haioneshi maandishi, ingawa inawaka.Mteja hanunui CIU maarufu kama remote bali atawajibika kuilipia kama ameiharibu yeye mwenyewe
Hivi tanesco siku 30 za kufungiwa umeme huwa ni za nini? Ni kweli upatikanaji wa vifaa unaweza chukua huo muda wote? (Just meter tu) mtu unaamka unaangalia nyaya zimepita bati lako lakini wewe huna nishati ya umeme, mbaya zaidi majibu yenu ni yale yale vifaa bado hatujapata, zikiwa tayari mtajulishwa, ukifatilia sana hujibiwa kabisa, namba za simu mnazoziweka kwenye maofisi hazipokelewi, hata ikitokea ukapata namba ya muhusika nae hakupokelei imekuwa vita sasa.Mimi ni Mkazi wa eneo la mwembe mtengu mkokozi maeneo ya kanisa la kkkt,
Napenda kutoa dukuduku langu leo maana tumeshakaa na kuvumilia muda mrefu sasa bila jawabu kutoka kwa wahusika,
Eneo tuliopo ni muda sasa hakuna nishati ya umeme, licha ya wenzetu waliotuzunguka pande zote nne wanawekewa umeme na hadi hivi sasa naandika hapa wameshawashia hapo juzi, lakini sisi hakuna hata procedure zinazoendelea,
Miezi mitatu iliyopita tulipeleka maombi ya kuhudumiwa Tanesco ya mkuranga, walituahidi mwezi unaoanza (September) wangekuja kufanya survey wajue nguzo ngapi zinatosha kutokea umeme ulipokomea, licha ya kuwajibu kuwa kuna nguzo mbili tu kutoka umeme ulipo na Nyumba ya kwanza kwenye eneo letu, na hadi umeme ufikie Nyumba zote zilizoeneo letu (jumla nyumba 20 tu) ni nguzo saba 7 pekee kuanzia na Zile mbili za njiani.
Hadi hivi leo ninavyoongea hakuna kilichofanyika tumeshafanya juhudi za kurudi kufatilia atleast wangekuja tu kutupa tu nguzo chini kungekuwa na ahueni Kuna jambo limetendeka,
Hili eneo jeografia yake sio nzuri, ni mwisho wa eneo hili la mkokozi tumezungukwa na bonde hivyo inapelekea hakuna eneo la makazi tena ukitoka kwetu , wezi na vibaka wanachukua advantage hiyo kutoka kwenye mabonde huko kuja huku kwetu kufanya uhalifu kwa sababu hakuna umeme ni giza totoro ikifika saa moja tu,
Hata ukichukua boda boda usiku hakufikishi hadi kwako kwakuhofia usalama wake anakuachia hapo kkkt kanisani palipo na umeme,
Tunaomba mtusaidie tuna jitahidi kujenga kupendezesha mji na kuleta maendeleo lakini serikali yetu inatukwamisha.
Namba zangu ni
0768900531
Johnson Mgaya.
Mkazi wa mwembe mtengu, mkokozi , kkkt kwa diwani.
Ndugu mpendwa Mteja wetuUkipiga simu hawapokei simu kwa wakati inaita tuuu, ikitokea wamepokea ukieleza shida yako wanakwambia mafundi wanaohusika watakuja kushughulikia tatizo. Shida inakuja ukiomba namba ya taarifa hawakutajii wanakwambia system ipo chini. Utaendelea kufuatilia kuwapigia simu kuwakumbusha wanakuuliza nipe namba ya ripoti nawaambia sikutajiwa niliambiwa system ipo chini na kazi haitafanyiki tena.
Inaonekana hukutoa taarifa kwao juu ya tatizo lako, kuna wakati mh mkuu wa wilaya ya Kisarawe aliwahi kuwaweka ndani baadhi ya wafanyakazi kwa utendaji mbovu wa kazi na aliwataka kila mtu mwenye shida yake akiwapigia Tanesco watoe namba ya taarifa. Wahusika tafadhali fuatilieni utendaji wa wafanyakazi kituo cha Gongo la mboto ni wa hovyo
Tafadhali tuonyesha namba ya taarifa na mwezi uliotoa taarifa tuifanyie kaziUpo sahihi, mimi nina namba ya taarifa tangu mwezi 3, 2019 tena niliifuata mwenyewe ofisini lakini tatizo langu halijatatuliwa. wananiambia tatizo lako tunalipeleka kitengo cha mita. Kila nikipiga simu nikiwapa namba ya taarifa wanashangaa hujahudumiwa. Yaani wenyewe wanajiogopa.
Ndugu mpendwa Mteja wetuHivi tanesco siku 30 za kufungiwa umeme huwa ni za nini? Ni kweli upatikanaji wa vifaa unaweza chukua huo muda wote? (Just meter tu) mtu unaamka unaangalia nyaya zimepita bati lako lakini wewe huna nishati ya umeme, mbaya zaidi majibu yenu ni yale yale vifaa bado hatujapata, zikiwa tayari mtajulishwa, ukifatilia sana hujibiwa kabisa, namba za simu mnazoziweka kwenye maofisi hazipokelewi, hata ikitokea ukapata namba ya muhusika nae hakupokelei imekuwa vita sasa.
Tusaidieni jamani mtu umeshalipa kila kitu, saveyi imeshafanyika kuja kufungiwa tu nayo iwe big deal?
Biashara gani mnafanya hamjali wateja wenu? Mtu analipia apate huduma mwisho wa siku inapita miezi hakuna bidhaa aliyolipia?
Binafsi nimeshachoka kulalamika, kufanya kazi kwa shinikizo sio vizuri.
Tafadhali tuonyesha namba ya taarifa na mwezi uliotoa taarifa tuifanyie kazi
Ndugu mpendwa Mteja wetuNamba ya taarifa sikutajiwa niliambiawa systeam ipo chini
Adelina JonasNdugu mpendwa Mteja wetu
Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako
Jina
Eneo
Wilaya
Namba ya simu
Tatizo
Toka lini
Ahsante sana
TANESCO Huduma kwa Wateja
Majibu yenu ni hivyo hivyo siku zote, nimereply post yangu ya nyuma ambayo mliniuliza the same qns na nikawajibu.Ndugu mpendwa Mteja wetu
Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako
Jina
Eneo
Wilaya
Namba ya simu
Tatizo
Toka lini
Ahsante sana
TANESCO Huduma kwa Wateja
Tunafatilia taarifa zako kwa hatua zaidi tafadhaliMajibu yenu ni hivyo hivyo siku zote, nimereply post yangu ya nyuma ambayo mliniuliza the same qns na nikawajibu.
Any way
Jina: Johnson mgaya
Simu: 0768900531
Eneo: mkokozi
Wilaya: mkuranga
Tatizo: kuungaishiwa umeme
Muda: siku 30 zimeshapita tangu nilipie umeme
Mazingira: nguzo ipo mlangoni kwangu.