Maneja wa TANESCO kibaha.tunaomba utuanganzie wakazi zaidi ya 15 wa eneo la Mwanalugali,hisia kali. Karibu na eneo inapojengwa zahanati
-Wananchi wa eneo hili kila tunapofutilia umeme tunaambiwa zinatakiwa nguzo Kati ya tano na kumi kuwafikia Wananchi wote.(Kwa hiyo Ni mradi).
-Huu mradi umekuwa unazungumziwa tangu mwaka 2015 mpaka leo.
-Tanesco ni shirika la kuwaangazia wananchi maisha na siyo shirika la kuwaweka wananchi gizani.
-Mradi unakuwa na timeframe,ni mradi gani hauma timeframe (haukamiliki tangu 2015 mpaka 2022).
-Sisi wakazi wa Mwanalugali tunaamini TANESCO Kibaha wanazo nguzo za umeme za kutosha.
-Viwanja vya Mwanalugali Wakati vinapimwa 2006 Serikali ilisema kutakuwa na huduma ya maji, umeme, zahanati,soko nk.
-Tunashukuru Serikali imeleta mradi wa maji na zahanati inajengwa.
-wananchi wenye Viwanja wameanza kuendeleza baada ya kuona huduma ya maji na zahanati inajengwa.Wananchi wengi watakuja kujenga na kuishi Mwanalugali kama huduma ya umeme itafika.
Ushauri
1). TANESCO Kibaha ifikishe nguzo eneo hilo,ili sisi wananchi tulipie service line ya shs320,960
2). TANESCO Kibaha itume wapimaji wake kuja kuhakiki na kufanya makadirio ya hizo nguzo ili kuomba fund TANESCO makao makuu.Mkurugenzi Mikuu wa TANESCO ni kijana safi na result oriented,hawezi kushindwa nguzo 10 za umeme-kibaha Town Council.
3). Kama TANESCO haina fedha wakazi wa tunaweza kuchangia gharama kwa pamoja, badala ya kumwambia mteja mmoja kulipia nguzo tatu zaidi ya milioni Saba,ili kupata huduma.
4). TANESCO iwe inatembelea au inapeleka miundo mbinu ya umeme maeneo yote yaliyopimwa,ili kuleta chachu ya Maendeleo endelevu na kuongeza kanzidata ya wateja.
5). TANESCO Kibaha wanaweza kupeleka/kujenga nguzo za umeme Mwanalugali, wakati wanasubiri vifaa vingine vya umeme,wakishafikisha nguzo karibu na wateja ndiyo waanze kutoa control number kwa wateja ,kwa kufanya hivi shirika litaongeza idadi ya wateja na mapato kwa shirika
Mwisho tunaomba Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, kutatua changamoto ya umeme Mwanalugali Kibaha Township.