TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Soma huu uzi tokea mwanzo.
 
Kumbe wakati wa dikteta magufuli pia umeme ulikuwa wa mgao
 
Tufukue kaburi..

February 2021.
Umeme haujawai kuacha kukatika hovyohovyo hata pindi mwendazake akiwa madarakani.

Wanaopiga kelele sasa ni wajane wa magu wanaotafuta kila aina ya kosa mama aonekani hajui kuongoza huku wakisahau kwamba CCM wote ni walewale tu.
 
Kwa takribani wiki moja sasa imejitokeza tartibu mpya za kufanya matengenezo kwenye njia za umeme na hivyo kupewa taarifa ya kutokuwepo huduma hii kwa muda fulani. Lakini kwa hii taarifa kuhusu upungufu wa umeme sasa tumepata uhakika ni nini kinachoendelea. Ila tukumbuke kwamba hapo awali wenzetu hawa walipewa agizo kwamba sehemu yeyote ambayo umeme utakatika basi wahusika wangefukuzwa kazi, na hicho ndicho kilichofanyika. Kwa kuchelea kufutwa kazi, basi wakaitafuta hiyo mbinu ya kuwepo matengenezo karibia kila siku. Kwa hilo walibana sana lakini imefika wakati sasa wameachia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…