TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Naambiwa 65% ya umeme unaozalishwa Tanzania unatokana na gesi asilia kutoka Kusini, na unazalishwa na mitambo ya gesi ya Ubungo / Songas na Kinyerezi, gesi bado ipo na mitambo inapiga kazi kama kawaida, mabwawa nayo uzalishaji bado unaendelea, sasa tatizo liko wapi hadi mnakata umeme kila siku hovyo hovyo bila ratiba?

Wakati JPM akihutubia bunge kwa mara ya kwanza kama Rais wa Tz aligusia suala la Tanesco kuhongwa na makapuni binafsi ya ufuaji umeme ili kufungulia mabwawa ya maji na kutengeneza uhaba wa umeme, je, mchezo huu umerudi tena?
Soma huu uzi tokea mwanzo.
 
Kwa siku tano mfululizo maeneo haya umeme ifikapo jioni unakatwana bila taarifa kwa sisi wateja labda Kama tangazo Hilo sijalisikia.

Maeneo ya ubungo Mandela Rd kuanzia external, maziwa, hadi darajani unaotazamana na rivaside.

Pamoja na kuwa jirani kabisa na mitambo ya umeme ya ubungo tunakutana na adha hii.

Leo tarehe 26/02/2021 umeme haukarudi mpaka saa 5 za usiku niandikapo taarifa hii na hatujui utarudi saa ngapi.

Tunaomba tutangaziwe kama ni mgao au uzembe au hitilafu.
Kumbe wakati wa dikteta magufuli pia umeme ulikuwa wa mgao
 
Tufukue kaburi..

February 2021.
Umeme haujawai kuacha kukatika hovyohovyo hata pindi mwendazake akiwa madarakani.

Wanaopiga kelele sasa ni wajane wa magu wanaotafuta kila aina ya kosa mama aonekani hajui kuongoza huku wakisahau kwamba CCM wote ni walewale tu.
 
Kwa takribani wiki moja sasa imejitokeza tartibu mpya za kufanya matengenezo kwenye njia za umeme na hivyo kupewa taarifa ya kutokuwepo huduma hii kwa muda fulani. Lakini kwa hii taarifa kuhusu upungufu wa umeme sasa tumepata uhakika ni nini kinachoendelea. Ila tukumbuke kwamba hapo awali wenzetu hawa walipewa agizo kwamba sehemu yeyote ambayo umeme utakatika basi wahusika wangefukuzwa kazi, na hicho ndicho kilichofanyika. Kwa kuchelea kufutwa kazi, basi wakaitafuta hiyo mbinu ya kuwepo matengenezo karibia kila siku. Kwa hilo walibana sana lakini imefika wakati sasa wameachia!
 
Back
Top Bottom