Tanesco yatangaza hitilafu, Mikoa iliyoungwa Gridi ya Taifa kukosa umeme

Tanesco yatangaza hitilafu, Mikoa iliyoungwa Gridi ya Taifa kukosa umeme

Kweli..

Sivyo, maana kura za wananchi hazina tija
Wanamharibia ila bado anawaamini.

Huku mtaani raia wanamlalamikia sana tu , kama atakua anajua basi kaamua tu kuwa iwe hivi.

Ila kwa tatizo hili la umeme hana cv nzuri.
 
Hili shirika haliishiwi visingizio, tunaenda mwezi wa mwisho katika ile miezi sita aliyopewa mkurugenzi wa tanesco lakini hali bado ni tete. Hivi mama Samia Rais wetu hsoni huu upuuzi au anachukulia pia tu wananchi wake kuteseka. Tanesco mmekuwa kero kubwa sans kwa watanzania.
 
Shida nini hili shirika kimefichwa watanzania hatujui
Kama unakumbuka miezi michache iliyopita tuliambiwa sababu ya mgao ni kupungua kwa maji
Sababu zimebadilika na zitaendelea kubadilika kadri siku zinavyozidi kwenda. Lengo tuzoee mgawo.
Sababu ya sasa ni maji kujaa na kuharibu miundo mbinu ya uzalishaji umeme.

CCM oyeeee!
 
Sijui maisha haya mpaka lini!

Hii nchi ni nchi ya wavimba macho, hivi siku yakupiga kura umeme ukatike hivi kitatokea nini! Nawaza tu!
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye Mikoa iliyounganishwa na Gridi hiyo.

“Juhudi za kurejesha mfumo zinaendelea kwa haraka ili huduma iweze kupatikana katika maeneo yote yaliyoathirika, Shirika linawaomba uvumilivu Wateja wake wote wakati Watalaamu wetu wakiendelea na jitihada za urejeshaji wa mfumo wa Gridi ya Taifa”

View attachment 2893086
Hivi sisi ni binadamu gani tunaovumilia kila siku? Nashauri wabadilishe lugha na sio hii.

TANESCO wamenisababishia hasara kubwa sana, yani natamani kwenda mahakamani wanilipe.
 
Wamerejesha kwa dakika 20 kisha wamekata tena.

Afu walivyo wehu watarudisha saa 7 usiku ambapo walinzi tu ndio wataoufaidi.

Asubuhi kukikucha tayari washaupiga panga.
 
Au kuna ndugu wa wale wamasai waliofanyiwa mtimanyongo yupo zamu so kaamua kuwaonyesha kuwa nyie si mna utamaduni wenu huko, aya na sisi huu ndiyo utamaduni wetu wa kuishi bila umeme 😂!.

Na hilo joto la bahari mkikaa masaa 12 tu mji wote wa Unguja unajua kitakachotokea 😂 🤣!.
 
Back
Top Bottom