Tanesco yatangaza hitilafu, Mikoa iliyoungwa Gridi ya Taifa kukosa umeme

Tanesco yatangaza hitilafu, Mikoa iliyoungwa Gridi ya Taifa kukosa umeme

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye Mikoa iliyounganishwa na Gridi hiyo.

“Juhudi za kurejesha mfumo zinaendelea kwa haraka ili huduma iweze kupatikana katika maeneo yote yaliyoathirika, Shirika linawaomba uvumilivu Wateja wake wote wakati Watalaamu wetu wakiendelea na jitihada za urejeshaji wa mfumo wa Gridi ya Taifa”

View attachment 2893086
Matatizo ya Tanesco tatizo ni Wizara na waziri wake au tatizo ni Malkia wa Puerto Rico na genge lake?
Je Tanesco ni janga la taifa?
Je Waziri kahujumiwa kwenye hili ili kumchafua na km ambavyo waziri yule alivyohujumiwa mfumo wa malipo ya Luku 2021 hadi ikawa sababu ya kutumbuliwa?

Je kumtumbua Waziri mwenye dhamana ndiyo suluhisho?
Au Malkia Mu Puerto Rico na genge lake wanastahili kutumbuliwa?
Huku nilipo kisiwa cha Lampenduza hadi mda huu hamna um umeme.
 

Attachments

  • 1706866390274.mp4
    375.5 KB
Nafikiri hili Shirika tungelibinafsisha na kuwapa private company waliendeshe nasi kama Nchi tuwe tunapokea gawio tu Kila Mwaka.

Maana hichi kinachoendelea ni as if Nchi haina Waziri Mkuu/Makamu ama Rais.

Haiwezekani Umeme ukosekane wakati Maji yamejaa kwenye mabwawa hadi yanaleta mafuriko 🙌
Hawawezi, wenyewe wanasema ndipo “usalama wa nchi ulipo” by usalama wanajua wanachomaanisha…..

Walau basi waipe sekta binafsi baadhi ya operation, ili tupate wakum-hold accountable. Serikali yenu haina jadi ya kuwajibika, tutaendelea kulalamika hadi Masiah arudi.

Btw, Babu ile nyumba yetu ya wageni usisahau kutuwekea generator.
 
Wafanyakazi wa shirika hili wanapaswa kufikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi kwa taifa
Wafanyakazi wa TANESCO nahisi walifukuzwa kimya kimya wote. Waliopo kazini ni wanafunzi wapo field.
Yaani,hii wiki ya pili sasa.

Af unanunua umeme, eti Debt Collected: 1500
Mtunyime umeme,af na hela zetu mchukue
 
Hivi hawa jamaa wanaijua PPM
PLANNED PREVENTIVE MAINTENANCE?
Wanaifanya?
Wana kitengo mahususi kwa ajili ya hii PPM?
 

Sijui ukiacha umbea, wivu, uzembe na ufisadi ni kitu gani kingine watanzania tunaweza.

Mashirika yetu kuyaendasha hatuwezi, tupo kama vilema wa fikra.
 
Tanesco kwa ujumla wake ni shida kabisa, taifa litafute mwekezaji mwenye teknolojia pevu ya kisasa asiwe Mwarabu awe Muingereza marekani au Mjerumani, akomeshe ujinga huu, zaidi ajenge mfumo mwingine mpya, taifa liwe na alternatives national grids, ziwe zinasaidiana.
Mwarabu tu ndio ndio anaweza hizi changamoto. Mmarekani aliisha weka mitambo yake hapa lakini shida iko palepale. Hukumbuki Obama alipokuja alifungua mradi wa kuzalisha umeme?
 
Hawawezi, wenyewe wanasema ndipo “usalama wa nchi ulipo” by usalama wanajua wanachomaanisha…..

Walau basi waipe sekta binafsi baadhi ya operation, ili tupate wakum-hold accountable. Serikali yenu haina jadi ya kuwajibika, tutaendelea kulalamika hadi Masiah arudi.

Btw, Babu ile nyumba yetu ya wageni usisahau kutuwekea generator.
Na hivi Sheria ya Usalama wa Taifa imefanyiwa mabadiriko ndiyo balaa 🙌

Ingekuwa Umri haujasogea sana ningeomba ridhaa Wananchi ili niwaongoze japo Kwa miaka 5 tu, changamoto ni kuwa nimezeeka.

Watanikuta nimelala Ikulu ama kwenye hafla za Kitaifa, katikati ya Hotuba wanakuta Kizee miye nauchapa Usingizi 😜

--------
Kule nimeweka Mjukuu, Kuna Vijana wakiingiaga mule huwa na kazi Moja tu ya kutoana Jasho hivyo ilikuwa considered awali kabisa 🤗
 
Back
Top Bottom