TANESCO yatangaza hitilafu ya umeme, mikoa kadhaa kukosa huduma ya umeme

TANESCO yatangaza hitilafu ya umeme, mikoa kadhaa kukosa huduma ya umeme

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake leo August 22,2023 kuwa kumetokea hitilafu ya mfumo katika kituo cha uzalishaji umeme kwa njia ya gesi cha Ubungo II.

“Hitilafu hiyo imesababisha mapungufu ya uzalishaji wa umeme kwa jumla ya megawati 268 kutokuwa kwenye mfumo wa usafirishaji umeme, hivyo baadhi ya maeneo kwenye Mikoa nchini yanakosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti”

“Jitihada za kurekebisha tatizo hilo zinaendelea na tutawataarifu Wateja wetu kila baada ya saa 4 kadri hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme itakavyokuwa inaimarika”

“Shirika linawashukuru Wateja wake kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme inakosekana”

1692691783876.jpeg
 
Tanesco kwa sasa ni chanzo cha vijana wengi kunyoa vichwa staili za ajabu ajabu

Kijana unakuta ni kondakta wa daladala basi likisubiri abiria anaingia saloon kunyoa ananyoa kichwa robo tu upande mmoja umeme wa Tanesco unakatika na basi linakuwa limeshajaa inabidi aende na robo kichwa kilichonyolewa hivyo hivyo akisingizia fasheni kujitetea kwa abiria wanaomshangaa lakini moyoni anaporomoshea matusi ya nguoni Tanesco kwa kumfanya aonekane kituko kwa abiria
 
Back
Top Bottom