TANESCO yatangaza hitilafu ya umeme, mikoa kadhaa kukosa huduma ya umeme

TANESCO yatangaza hitilafu ya umeme, mikoa kadhaa kukosa huduma ya umeme

Huu umeme umeondoka na upatikanaji wa Whatsapp!? Ama MB zangu zijeisha?
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake leo August 22,2023 kuwa kumetokea hitilafu ya mfumo katika kituo cha uzalishaji umeme kwa njia ya gesi cha Ubungo II.

“Hitilafu hiyo imesababisha mapungufu ya uzalishaji wa umeme kwa jumla ya megawati 268 kutokuwa kwenye mfumo wa usafirishaji umeme, hivyo baadhi ya maeneo kwenye Mikoa nchini yanakosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti”

“Jitihada za kurekebisha tatizo hilo zinaendelea na tutawataarifu Wateja wetu kila baada ya saa 4 kadri hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme itakavyokuwa inaimarika”

“Shirika linawashukuru Wateja wake kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme inakosekana”

Muhimu tu iwe ni hitilafu kweli. Maana hamchelewi nyinyi kutengenezea mgao bandia, ili baadaue mpate sababu ya kuwaleta wale ndugu zenu wa IPTL, Aggreco, Dowans, Richmond, Symbion, na takataka nyinginie za upigaji.

Binafsi nitaanza kudunduliza fedha kiasi ili niweke tu mfumo wa solar kwenye kaofisi kangu, kama backup. Maana mpaka muda huu hali si hali.
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake leo August 22,2023 kuwa kumetokea hitilafu ya mfumo katika kituo cha uzalishaji umeme kwa njia ya gesi cha Ubungo II.

“Hitilafu hiyo imesababisha mapungufu ya uzalishaji wa umeme kwa jumla ya megawati 268 kutokuwa kwenye mfumo wa usafirishaji umeme, hivyo baadhi ya maeneo kwenye Mikoa nchini yanakosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti”

“Jitihada za kurekebisha tatizo hilo zinaendelea na tutawataarifu Wateja wetu kila baada ya saa 4 kadri hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme itakavyokuwa inaimarika”

“Shirika linawashukuru Wateja wake kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme inakosekana”

Malizeni bwawa la Rufiji, pumbavu sana
 
[emoji23][emoji23]
Tanesco kwa sasa ni chanzo cha vijana wengi kunyoa vichwa staili za ajabu ajabu

Kijana unakuta ni kondakta wa daladala basi likisubiri abiria anaingia saloon kunyoa ananyoa kichwa robo tu upande mmoja umeme wa Tanesco unakatika na basi linakuwa limeshajaa inabidi aende na robo kichwa kilichonyolewa hivyo hivyo akisingizia fasheni kujitetea kwa abiria wanaomshangaa lakini moyoni anaporomoshea matusi ya nguoni Tanesco kwa kumfanya aonekane kituko kwa abiria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANEANDIKA TAARIFA KAMA MATAHIRA.

ole wake Tanzania Tusipo isaidia.
 
Screenshot_20230822_171930_WhatsApp.jpg
 
'Preventive Maintenance Schedule' isipotekelezwa kwa Wakati tatizo hili halikwepeki
 
Back
Top Bottom