Tanga: Ajali ya Fuso yaua sita wilayani Lushoto, wengine wajeruhiwa

Kwa barabara, njia,miteremko ya huko

Ukienda na gari yenye break za kusuasua

Unajitafutia kifo mapemaaaa

Ova
 
Mwenyezi Mungu sidhani anahusika, accident ni kosa la mtu!,barabara zetu ni mbovu mno, magari yetu lini yalifanyiwa proper roadworthy?major service?,tusimlaumu Mwenyezi Mungu
Tena huko lushoto ni balaa

Ova
 
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 239 AFB walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Jumanne Machi 29, 2022.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.

RPC Jongo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

View attachment 2168006

Chanzo: MillardAyo
Lushoto mabasi na hizo fuso huwa wanashuka kma wehu,mtu unateremka mlima unaskia honi nyuma za kumpa site apite...

Unajiuliza huyu mjinga anaakili kweli,mana breki za upepo sio za kuaminika ukifunga ghafla zinaweza kupasua pipe na ndio hakuna tena breki
 
Mwenyezi Mungu sidhani anahusika, accident ni kosa la mtu!,barabara zetu ni mbovu mno, magari yetu lini yalifanyiwa proper roadworthy?major service?,tusimlaumu Mwenyezi Mungu
Wakati wa JPM barabara zilikuwa nzuri? Mbona ajali zilipungua. Yaleyale ya Tanesco na kukatika kwa umeme.
 
Mwendazake hakupunguza ajali nenda kaangalie statistics, mnampa credit za uongo tu, barabara zetu ni mbovu tuutambue ukweli huu na tuufanyie kazi
 
Madereva wakiwa Soni wanakunywa kutokana na baridi, wakianza kushuka kuelekea Mombo pombe huwa inapanda maradufu.
 
Aise
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 239 AFB walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Jumanne Machi 29, 2022.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.

RPC Jongo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

View attachment 2168006

Chanzo: MillardAyo
Aise nilikuwepo Lushoto mwezi wa pili. Zile Kona kona na yale makorongo. Nashangaa hata hivyo ajari ni chahe aise.
 
Wabongo ni waduanzi tu wakibanwa na Trafiki wanaona wanaonewa ajali ikitokea lawama trafiki nchi ina watu wa hovyo .
 
Daaah ingekuwa wanashtuka mda huu waziri husika angekuwa ameshawaita hao wenye dhamana ya kusimamia hizi barabara na magari na kupeana mawazo yangeyoweza kuzuia au kuzifuta kabisa hizi ajari za kizembe zembe .
 
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 239 AFB walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Jumanne Machi 29, 2022.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.

RPC Jongo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

View attachment 2168006

Chanzo: MillardAyo
Yaani wafuate sheria wasipite barabarani au.
Hivi kuna dereva anaependa kupata ajali?
 
Wiki iliyopita mtu mmoja kama ckosei amekufa baada ya lori scania kuingia nyumba ya mtu.

Jana profesa amepoteza maisha kwa ajali

Leo mbeya wamekufa wanne kwa ajali,

Leo tena tanga watano wamekufa kwa ajali

Kila nafsi itaonja umauti
Na katika utitiri wa ajali zote hizi,viongozi wapo na wamekaa kimya kabisa yani utafikiri ni mambo ya kawaida kabisa.Nasikitika kama Taifa tumerudi nyuma sana,swala la uwajibikaji kwa viongozi limeota mbawa.Huu mwaka mmoja wa mama sijui tunasherekea mafanikio yapi!
 
Roho ya Mauti imeachiliwa panahitajika maombi ya kufunga na kukesha kwajili ya kuvunja hii roho!!!!
Nafikiri vyombo vya moto vifanyiwe ukaguzi na matengenezo wa mara kwa mara, na madereva pia wakaguliwe leseni zao, uzoefu na kama hawatumii kilevi.
Madereva wasibebe mizigo kupita uwezo wa gari, mizigo ipakiwe katika uwiano wa uzito, isiwekwe upande moja zaidi ya upande mwingine, na mizigo ifungwe vizuri, kuepuka kuanguka au kuangukia watumia barabara wengine.
Wakaguzi wa barabara, wafanye kazi yao na kutoa tahadhari kwa watumia barabara, popote penye hitilafu na matengenezo yasichukue muda mrefu.
 
Haya ulioshauri,ni mazuri sana,sema kiuuwalisia hayawezekani,labda ndotoni tu!! Tanzania bado tuna safari ndefu sana!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom