Tanga: Ashikiliwa kwa tuhuma za kuua baada ya kumfumania mkewe

[emoji2][emoji2]dah inauma kiukweli
 
Nakazia
 
ndio amchakatie kwangu kwanini wasifanye gesti huko ambako sitaona.
 
Akipata wakili mzuri mahakamani anachomoka, labda sasa huko uraiani ndugu wa marehemu wa'take revenge..
Kama hakufanya maandalizi kwa ajili ya kuua na ameua pale pale na muda uleule,atapatwa na manslaughter kwa defense ya provocation lakini mvua kadhaa zitamuhusu.
 

Limetimia lile andiko la Kazi ya ibilisi ni kuchinja na kuharibu
 
Tanga kunani pale?

Nakumbuka enzi hizo kuna mchezaji mpira maarufu sana wa Coastal Union ya Tanga wana Maangush tulikua tukiaa nae jirani, katika mojawapo ya barabara za Tanga

Siku moja alirudi nyumbani kwake ghafla na akamkuta mkewe yupo na njemba na wakiwa chumbani kwake, kwenye kitandani chake, wakiwa uchi wa mnyama! Inaelekea walipomaliza mambo yao usingizi ukawapitia

Alichokifanya yule jamaa baada ya kuona hali ile na akahakikisha wahusika wamemuona akafunga mlango taratiibu na kutokomea nje ya nyumba

Yule mwanamke hakuondoka pale nyumbani kwa mumewe na katika kipindi cha mwezi na nusu jamaa mwenye mke akawa anaishi hapohapo na mkewe maisha ya kawaida kama hakuna kilichotokea(details kama walikua wakipeana unyumba au laa sina maana jamaa hakusema na Baba yangu Mkubwa hakumuuliza)

Siku moja anarudi nyumbani hakumkuta yule mkewe! Alikua kaondoka na kafungasha kila kilicho chake!

Yule mchezaji akaja kwa marehemu Baba yangu Mkubwa ambaye tulikua tunakaa nae pale home

Akamueleza kua “Mzee kuna watu wana maisha marefu. Leo nilikua nifanye mauwaji ya kikatili sana”

Akamueleza Mzee wangu kisa kizima na mimi nikiwa pembeni nikijifanya sina habari na mazungumzo yao!!!!

R. I.P the then Liberal wa Coastal Union.
 
baada ya kuua , unakwenda Jela maisha au kunyongwa ......huku mkeo anaendelea kugegedwa na jamaa kuhamia kabisa nyumbani kwako..sasa hapo umepata au umepatikana?
 
😂
 
mkuu kuchakata mbususu nyumban kwa mwanaume kunahitaji moyo sana japokuwa nilishapiga matukio ya aina hii Mara kibao ila umakini unatakiwa kwanza usilale na ukiingia hakikisha umekagua siraha zote zilizomo ndani za kukuokoa ikitokea gafla ukapata uvamizi pia tafta chemba za kujificha kama kujiokoa hamna namna
 
baada ya kuua , unakwenda Jela maisha au kunyongwa ......huku mkeo anaendelea kugegedwa na jamaa kuhamia kabisa nyumbani kwako..sasa hapo umepata au umepatikana?
Hii hanyongwi mtu... jamaa anachomoka mchana kweupeeee.. kama vile kuuwa jambazi tu... kuna njia nyingi za kujitetea kwenye hili..
 
Marehemu alimzarau sana jamaa asee
Ukale tunda lake tena ndani ya boma lake ni mbaya sana
 
Nakubaliana na wewe mkuu,lakini huoni kuwa mgoni alikuwa na kosa,haiwezekani uende kwa familia ya mwanamme mwenzako kufanya ufusika na mke wake,Hilo Ni kosa kubwa sana,lakini tambua kuwa mwenye mke angezembea kidogo angeuliwa na huyu mgoni,maana kufikia hatua ya kwenda kwa mwanamme mwenzako unakuwa umejiandaa,sidhani Kama utaenda mikono mitupu utadhani unaenda kupeleka injili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…