Tanga jiji la kishamba sana, nashindwa kuelewa kwanini mkoa huu ulipewa heshima ya kuitwa Jiji

Tanga jiji la kishamba sana, nashindwa kuelewa kwanini mkoa huu ulipewa heshima ya kuitwa Jiji

Katika historia Tanga ni mji wa pili kuitwa jiji baadavya Dar.
Acha uongo..! Mji wa pili kutangazwa jijij ni Mwanza, Tanga imepewa jiji na mkapa zilitangazwa pamoja na Arusha, mbeya na tanga, badae arusha ikatenguliwa labla ya kurudishiwa hadhi yake.
 
mtoa uzi umekurupuka sioni cha maana ulichoandika hapa, ulitakiwa uje na hoja zilizoshiba ili kuonesha kua Tanga haikustahiki kuoewa jiji lakini kwa hoja za bodaboda kusubiri taa za barabarani na vijumba vya udongo mjini hazina mashiko mana hadi leo kariakoo zipo nyumba za udongo tena si moja wala mbili
 
Tanga ndio asili ya Tanganyika
Tanga na Nyika.
Baada ya kuona histori ya Tanganyika inabebwa na Tanga ikabidi itumike nguvu ya ziada kuufifisha mkoa mzima kielimu,kiuchumi,ki siasa na kimefanyika
Kuna kiongozi mmoja alipata kusema "maji yatapanda Malima"
Akimaanisha kuwa maendeleo ya tanga yote yatakwenda bara na tanga kubaki historia tu.
Baada ya reli ya kati ilifuata reli ya tanga moshi hadi arusha.
Hivyo kuipa jiji ni kujikosha kwa yaliyofanywa.
 
Ni kitu cha kujiuliza, inakuwaje uzi mzima so far hakuna aliyetoa sababu kwa nini Tanga ni jiji au kwa sababu zipi haifai kuwa jiji.
Zaidi tu ya kugeuza hii mada kama personal, mpaka watu wanataka kung'atana.
 
Town center ya Tanga ni bora kuliko mkoa wowote hapa nchini iko kama ile miji ya Europe. Huko msambweni na makorora achana nako.Angalia ofisi ya Rc na mitaa jirani kama raskazone na jirani na hapo ilivyopangwa kwa ufundi mkubwa
Mimi huwa nafanananisha na Glasgow kwa kweli
Ukiangalia mpangilio wa mji na barabara zake ni kama Scotland (glasgow)
 
Kwa hiyo kuvuka red light ni sifa mojawapo ya kuwa mjini au ujinga na kutafuta umauti
 
Wewe muongo Tanga hakuna traffic lights. Nasikia ndio wana mpango wa kuziweka. Jiji ni pamoja na wingi wa watu. Na ndio sababu pekee ya msingi ya Dar kuitwa jiji.
Tayari zipo mkuu, wameweka hapo RAILWAY (eneo linalo onekana kwenye picha) na mitaa ya TOYOTA
 
Hivi dodoma bado haijawa na hadh ya kuitwa jiji tu
Na ndo nashangaa na ndo kuna mpango mji kama huo huo wa Tanga labda kwa kuwa hakuna magorofa mengi [emoji23]
 
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea mji kuitwa jiji ,nitazitaja baadhi
1)Idadi ya watu inapokua kubwa angalau million2
2)fursa za biashara
3)miundo mbinu mizuri ya usafiri kama vile barabara na reli n.k
4)fursa za kielimu
5)ukuaji wa viwanda n.k
6)huduma za kibank na kiuchumi
Pamoja na upatikanaji wa huduma za kijamii. Hizi ni baadhi tu ya sifa ya mji kupanda hadhi na kuitwa jiji na kutokana na sifa hizi Tanga imekidhi vigezo vya kuitwa jiji.
 
Washamba ni kama watu gan hapa Dar, mnapozungumza habari za mikoani huko hua sielew kabisa
 
Back
Top Bottom