Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Hizi ndo sababu za ajali nyingi Kwa Tanzania na Africa Kwa ujumla , magar yanaongezeka kila sku miundombinu Ile Ile ,
 
Kwa maana hyo misiba imekuwa 18 kwa wakt mmoja Mbna hi Ni hatari sana
 
Daaah yaani ni misiba juu ya msiba,poleni sana wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Tunaweza kusema mengi kwa kadri tuwezavyo na tudhaniavyo.
Lakini kuna watu wanapitia wakati mgumu lakini hii familia iliopata msiba natumaini wao kwa sasa wako kwenye wakati mgumu kuliko tunavyoweza weza kusema, pangine wanahitaji faraja ya taifa.

Changamoto za vyombo vya usafiri bado ni kubwa sana huku kwetu, madereva wamekua na haraka kuliko , na bahati mbaya hawafiki wanako harakisha kufika, hebu madereva mtafakari tena juu ya maisha, maisha ni furaha sio huzuni na maumivu, hebu tufanye maisha kuwa mazuri na ya furaha kwa kujali .

Pole nyingi sana kwa wote walio athirika, pole kwa walio jeruhiwa, pole kwa walio fiwa na kufiwa tena.

Wakati ufike watu wa kaskazini na wengineo tufikirie upya kama bado kunaulazima wa kufanya maziko nyumbani tu.
 
Watu 17, ambapo 14 ni wa familia moja, wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magira Gereza, Tarafa ya Mombo wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso iliyoligonga gari aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni wanaume tisa, wanawake sita, watoto wawili mmoja wa kike na mmoja wa kiume.

Majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo kuendelea na matibabu na wawili wamebaki Hospitali ya Wilaya Magunga huku hali zao zikiendelea vizuri.

Mgumba amesema miili ya marehemu ipo katika Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe.

Chanzo cha ajali ni kimeripotiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya fuso kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na ndipo lilipogongana uso kwa uso na Coaster hiyo.

TBCOnline
 
Midereva ya mafuso hata sijui wana matatizo gani? Yaani mwezi uliopita hapa kijijini kwetu bodaboda aligongwa na fuso yaani alichanguliwa changuliwa kulibak kiwiliwili tu.....hawa nahis watakuwa wanavuta bangi na gongo.....then nahis wanaona barabara zimetengenezwa kwa ajili yao tu kwan huwa wanatembea katikati ya barabra hawakai kwenye site zao.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…