Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Poleni sana wajomba poleni sana akina Mrema. Hawa waliopata ajali ndiko bibi yangu alikozaliwa. Baba yangu angekuwa kwenye coaster hii aisee leo ningekuw nalia sana. .
Its very sad. Marehemu kafa na watoto wake watatu. Msiba mkubwa Rombo siamanzi kubwa sana ndugu zangu. .
Huwa tunasikia msiba za ajali ila usisikie kwa watu wa nyumbani very sad indeed. .


Raha ya millennium uwaangazie ee Bwana. .

Aisee,ni wa Rombo sehemu gani mkuu?
 
Tuwaulize nyie wa Rohoni ambao mna dunia nyingine mnayoijua , hao watu waliokuwa wanasindikiza walitakiwa kufanyeje ..... Mana sa hv inasingiziwa maiti , kana kwamba Magari ya maiti hayatakiwi kupata ajali

Take it easy....

Gasp some water and gargle for a while...

It's a free world 🙂.
 
View attachment 2505507View attachment 2505508View attachment 2505511
Picha za Ajali

Ndugu waandishi wa Habari na Ndugu wananchi wa Mkoa Wa Tanga na Tanzania kwa ujumla Nimepokea kwa masikitiko makubwa tukio la Ajali Mbaya iliyotokea usiku wa leo. Ajali hiyo imehusisha Magari mawili na kusababisha Vifo vya watu 17 na Majeruhi 12 Pamoja na Uharibifu mkubwa wa Magari hayo..

Ajali ilitokea Tarehe 03/02/2023 Majira ya Saa 4.30 Usiku Eneo la Magila Gereza Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera - Buiko.

Magari yaliyohusika na Ajali hiyo ni Gari Na T.673 CUC aina Mitsubish Fuso Ikiendeshwa na Dereva ambaye Jina Lake Halijafamika iligonga na Gari T.863 DXN aina ya Coaster Coaster Iliyokuwa imebeba Mwili wa Marehemu n Abiria 26 iliyokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

Ajali hii inasababisha Vifo 17 na Majeruhi 12. Ambao Majina yao wote Hayajafahamika. Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya Ya Korogwe na Majeruhi 10 Wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Majeruhi 2 wamebaki Hospital ya Korogwe Kwa Matibabu.

Chanzo cha Ajali ni Mwendo Kasi na Uzembe wa Dereva wa Gari Na :T.673 CUC M/Fuso Kulipita gari la mbele Bila Ya kuchukua Tahadhari na kugongana Uso kwa uso Gari Na :T.863 DXN T/Coaster

Tukio la Ajali Baada ya kukaguliwa , Magali yote yameshaondolewa barabarani na Sasa Barabara inapitika.

Mgumba T. Omary
Mkuu wa Mkoa Wa Tanga.
Nakumbuka walipiga marufuku kusafiri usiku imekuaje tena? Usiku risk ni kubwa sana na madereva weng wanalala
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Hahahahaha wewe, Mshana Jr, Kila kitu unataka kukitafsiri na kuleta maelezo ya kidadisi.
 
Poleni sana wajomba poleni sana akina Mrema. Hawa waliopata ajali ndiko bibi yangu alikozaliwa. Baba yangu angekuwa kwenye coaster hii aisee leo ningekuw nalia sana. .
Its very sad. Marehemu kafa na watoto wake watatu. Msiba mkubwa Rombo siamanzi kubwa sana ndugu zangu. .
Huwa tunasikia msiba za ajali ila usisikie kwa watu wa nyumbani very sad indeed. .


Raha ya millennium uwaangazie ee Bwana. .
Poleni sana ndugu yangu, poleni mno .
 
Madereva wa mafuso ni wana matatizo na gari zao zenyewe zile siyo za kuziamini hata kidogo na bado wanaenda hovyo njiani. Kuna natoka Tanga kuelekwa Dodoma njia inaruhusu kuovertake, dereva wa basi kakoleza mwendo anataka kumpita. Jamaa si kasogeza gari kati kuzuia halafu anaenda mwendo mdogo, ikabidi apigiwe honi nyingi ndiyo akarudi upande na hii wametufanyia madereva zaidi ya watatu njiani.

Hayo mafuso hata ukiwauliza madereva wa malori makubwa wanakwambia hayo magari siyo yangekuwa binadamu wangesema yana tabia ya kupoteza kumbukumbu. Yanahitaji umakini mkubwa kuendesha kuliko hayo malori ila wao wanayachukulia poa.
 
Back
Top Bottom