Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Huu msafara wa Msiba nilikutana nao Jana Saa 9.05 alasiri pale Madale Kituo Cha Polisi,Kulikuwa na Coaster mbili zimeongozana,hii coaster iliyobeba mwili wa marehemu ilikuwa mbele na nyingine ikifuata nyuma!!,Kiufupi hizi Coaster zilikuwa Spidi Sana!!,
 
Ningekua miongoni mwa mashuhuda na ninamuona huyo dereva wa fuso bado akiwa hai ambaye ndiye aliyesababisha ajali kwa uzembe, ningeenda kumsimanga na kummalizia afe vizuri.
Uzembe wake umegharimu maisha ya watu, lakini tulivyo wajinga ukisoma comments utaona watu wanahusianisha ajali na uchawi, wengine wanachukulia mzaha
 
Poleni sana wajomba poleni sana akina Mrema. Hawa waliopata ajali ndiko bibi yangu alikozaliwa. Baba yangu angekuwa kwenye coaster hii aisee leo ningekuw nalia sana. .
Its very sad. Marehemu kafa na watoto wake watatu. Msiba mkubwa Rombo siamanzi kubwa sana ndugu zangu. .
Huwa tunasikia msiba za ajali ila usisikie kwa watu wa nyumbani very sad indeed. .


Raha ya millennium uwaangazie ee Bwana. .
Pole sana mkuu, hii "RAHA YA MILLENNIUM" ndio Raha gani?
 
Watu 17, ambapo 14 ni wa familia moja, wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magira Gereza, Tarafa ya Mombo wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso iliyoligonga gari aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni wanaume tisa, wanawake sita, watoto wawili mmoja wa kike na mmoja wa kiume.

Majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo kuendelea na matibabu na wawili wamebaki Hospitali ya Wilaya Magunga huku hali zao zikiendelea vizuri.

Mgumba amesema miili ya marehemu ipo katika Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe.

Chanzo cha ajali ni kimeripotiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya fuso kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na ndipo lilipogongana uso kwa uso na Coaster hiyo.

TBCOnline
14 ni familia moja!!??
duuh msiba mzito sana huu
 
إنا لله وإنا إليه راجعون

Utaratibu wa kusafirisha maiti ni katika taratibu mbaya zaidi katika kushughulikia mwili wa marehemu, kwanza husababisha huzuni zaidi kwa wafiwa na pia ni kwenda kinyume na mafundisho na maajabu waislamu nao siku hizi wanasafirisha.
 
إنا لله وإنا إليه راجعون

Utaratibu wa kusafirisha maiti ni katika taratibu mbaya zaidi katika kushughulikia mwili wa marehemu, kwanza husababisha huzuni zaidi kwa wafiwa na pia ni kwenda kinyume na mafundisho na maajabu waislamu nao siku hizi wanasafirisha.
Marehemu kaondoka na roho zingine 17
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Mzee wa utamaduni...tulia basi
 
Back
Top Bottom