Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

Tanga, Korogwe: Ajali yaua 17 na kujeruhi 12

إنا لله وإنا إليه راجعون

Utaratibu wa kusafirisha maiti ni katika taratibu mbaya zaidi katika kushughulikia mwili wa marehemu, kwanza husababisha huzuni zaidi kwa wafiwa na pia ni kwenda kinyume na mafundisho na maajabu waislamu nao siku hizi wanasafirisha.
Hivi uislam hautakiwi,kusafirisha maiti

Nimeuliza tu

Ova
 
View attachment 2505507View attachment 2505508View attachment 2505511
Picha za Ajali

Ndugu waandishi wa Habari na Ndugu wananchi wa Mkoa Wa Tanga na Tanzania kwa ujumla Nimepokea kwa masikitiko makubwa tukio la Ajali Mbaya iliyotokea usiku wa leo. Ajali hiyo imehusisha Magari mawili na kusababisha Vifo vya watu 17 na Majeruhi 12 Pamoja na Uharibifu mkubwa wa Magari hayo..

Ajali ilitokea Tarehe 03/02/2023 Majira ya Saa 4.30 Usiku Eneo la Magila Gereza Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera - Buiko.

Magari yaliyohusika na Ajali hiyo ni Gari Na T.673 CUC aina Mitsubish Fuso Ikiendeshwa na Dereva ambaye Jina Lake Halijafamika iligonga na Gari T.863 DXN aina ya Coaster Coaster Iliyokuwa imebeba Mwili wa Marehemu n Abiria 26 iliyokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

Ajali hii inasababisha Vifo 17 na Majeruhi 12. Ambao Majina yao wote Hayajafahamika. Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya Ya Korogwe na Majeruhi 10 Wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na Majeruhi 2 wamebaki Hospital ya Korogwe Kwa Matibabu.

Chanzo cha Ajali ni Mwendo Kasi na Uzembe wa Dereva wa Gari Na :T.673 CUC M/Fuso Kulipita gari la mbele Bila Ya kuchukua Tahadhari na kugongana Uso kwa uso Gari Na :T.863 DXN T/Coaster

Tukio la Ajali Baada ya kukaguliwa , Magali yote yameshaondolewa barabarani na Sasa Barabara inapitika.

Mgumba T. Omary
Mkuu wa Mkoa Wa Tanga.
9
Narudia tena Tanzania ni miongoni mwa nchi hatarishi uwapo barabarani.
Ajali za namna hii zinaakisi akili za watu wetu kwamba sisi ni taifa la wajinga wengi.

Siku moja, nimepewa lift na ndugu yangu mtu mwenye elimu yake na kazi nzuri, lakini namna alivyokua anaendesha ovyo barabarani nikasema huyu lazima apate ajali. Wamenishusha zangu Moro, wao wakielekea Dodoma, baadaye napata taarifa wamekula mzinga gari haifai, yeye na mkewe wameumia vibaya.
L
Poleni sana wajomba poleni sana akina Mrema. Hawa waliopata ajali ndiko bibi yangu alikozaliwa. Baba yangu angekuwa kwenye coaster hii aisee leo ningekuw nalia sana. .
Its very sad. Marehemu kafa na watoto wake watatu. Msiba mkubwa Rombo siamanzi kubwa sana ndugu zangu. .
Huwa tunasikia msiba za ajali ila usisikie kwa watu wa nyumbani very sad indeed. .


Raha ya milele uwaangazie ee Bwana. .
Pole kwa wafiwa, inasikitisha sana!!
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Sasa ndio marehemu Aue watu wote.. Hiyo fuso imezingua sana. Madereva wa tz tunatakiwa tupewe course upya
 
Kipande cha Chalinze hadi Segera,
Serikali iangalie uwezekano wa kuweka taa za bara barani za solar.

Pia iangalie uwezekano wa kukata vilima au kujazia mabonde ili kutoa ile migongo inayosababisha magari ya pande mbili tofauti yasiweze kuonana...

Pia iangalie uwezekano wa kuongeza lane ya tatu kwa kipande hiki chote.
 
Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 Ikitokea Dar es Salaam Kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.[emoji848][emoji2827]
Marehemu hakuwa tayari kusafirishwa? Ama kuna mtu hakupenda awepo kwenye msafara?
Kaka sidhani kama ndivyo..ni uzembe tu wa madereva..Sisi wenyewe tuliwahi koswa na fuso mwaka Jana mwezi wa sita MITA kama hiyo tulikuwa tunamsafirisha mwili..pona yetu dereva wetu alikuwa yuko smart na anawafahamu vizuri madereva wa fuso..baada ya kuukwepa huo mtego nilimuuliza alijuaje..
Akaniambia hawa madereva wa fuso wanatakiwa fika sokoni kabla ya saa 11 asubuhi Ili mzigo uuzike..so usiku lazima wakimbie Sana..aliwaona wakiwa wa nafukuzana..wa nyuma alitaka kuovertake hapo maeneo ya korogwe ..kutuona akarudi site yake..ila dereva akasema huyo amerudi tu kwa mshtuko ila najua Hana breki za kumzuia kumvaa wa mbele yake alikuwa yuko kibati..so hatakuwa na jinsi Zaid ya kutoka tena liwalo na liwe..maana ni either amvae mwenzake au atoke upambane nae .ndio maana nikaamua punguza mwendo na kukaa pembeni..Na kweli ndicho kilichotokea.ina maana dereva angejisahau baada ya kumuona amerudi site yake..yangetukuta.
Rai kwa wanaoendesha usiku..jamani kuweni makini sana
 
Hapo lazima kuna ndugu zaidi ya 10
Kwa utaratibu wa Moshi..gari linalobeba mwili wa marehemu ndilo linalobeba ndugu zake wa karibu..kama ni baba basi humo watapakia mke na watoto..kaka na madada ..yaani wa ndugu wa karibu Sana..so waona utakuwa ni msiba mkubwa kiasi gani..yaani ni ukoo umeondokewa na watu waote hao
 
Daah poleni sana ndugu zangu wa Moshi...!! Msiba juu ya msiba yani unashindwa hata kuliaa unabaki unashangaa tuu... Mungu awatie nguvu sana
 
Back
Top Bottom