Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

View: https://www.instagram.com/p/Cznm2qpiBWZ/?igshid=MXM3Z3RnNmRmcDBkaw==
 
Watoa huduma ya afya wapo sahihi.

Hivi kuna sehemu unaweza kwenda ukahudumiwa bure? .

Wahudumu wa afya ili wapate pesa ni lazima wewe uumwe utoe pesa utibiwe ndipo nao wapate pesa.

Heshimuni kazi za watu acheni kuwakandamiza.
 
Haospitali Zingine wanaweka deni , siku ya kutoka unadaiwa , hapo inabidi wawajibishwe hao wahusika
Kila sehemu na utaratibu wake.

Wagonjwa wakitibiwa bila kutozwa hela na wakafanikiwa kuondoka tabu mnawaachia watoa huduma kulipa madeni yasiyo nakichwa wala miguu.

Wewe unaweza ukamfanyia mtu kazi bila kukulipa?
 
Mungu wangu, chozi limenitoka! Kufiwa kupo ila sio kwa kukosa namna ya kumsaidia mwanao, hasa kifedha!
Mungu ampe mama yake marehemu faraja.

Wahusika wachukuliwe hatua kali kwa haraka!
Hakuna sababu ya kutosheleza ya kusababisha kifo cha mama na mtoto kwa ukosefu wa fedha.
Ficha ujinga na upumbavu wako.

Kumbuka hao wahudumu wa afya nao wana familia zinawategemea.

Wewe unaweza kumuhudumia mtu bila kukulipa?

Tuchukulie mfano mdogo tu ,nenda hata kwa mama ntilie kaombe ugali hata wa elfu 1 uwaambie njaa inakuuma unakaribia kufa na pesa ya chakula huna uone kama utapewa hicho chakula.
 
Mungu wangu, chozi limenitoka! Kufiwa kupo ila sio kwa kukosa namna ya kumsaidia mwanao, hasa kifedha!
Mungu ampe mama yake marehemu faraja.

Wahusika wachukuliwe hatua kali kwa haraka!
Hakuna sababu ya kutosheleza ya kusababisha kifo cha mama na mtoto kwa ukosefu wa fedha.
Wote wachukuliwe hatua akiwemo na mwanaume aliyemtia mimba na nduguze huyo mwanaume wakamatwe.kwa kutia mimba.na kutowajibika hata kutoonekana tu hapo hospitalini wanaachia mama mkwe anahangaika peke yake
 
Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

Makonda huko anapita na kuropoka wakati mfumo hausaidii watu maskini wakati wa uitaji.

Hii nchi ni ya hovyo, na ukipata fursa ondoa kizazi chako wakaishi ulaya au hata Botswana.

Kila siku mambo ya hovyo na ya kishenzy yanaendelea, Makonda anagawa hela huko barabarani.

Msaada wa nchi hii upo kwenye kurekebisha mifumo na sio Bongo movie za ccm.
 
Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo...
Uchunguzi wa nn? Kwani kuna utaratibu serikali imeweka ya kusaidia watu katika haya mazingira,

Nachukia nakuumia mpaka nawaza hii dunia mtu ananyanyasikaje hivyo kwa ajili ya 200,000/-

...hole country, inauma sana, sana haya mambo, kafa, helplessly mtoto wa watu.
 
Back
Top Bottom