Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Kwa hakika pesa imefanywa kipaumbele kwenye vituo vya huduma za kijamii. Yaani badala ya kuwa na roho ya utu na ubinadamu watu wanatanguliza maslahi. Kwa hakika wote waliohusika katika hili nafsi ya huyo mama itawatesa mpaka wanaondoka duniani.
Hakuna sehemu ambapo pesa haipewi kipaumbele, ndio maana kila kukicha watumishi wanalia lia wapandishiwe mishahara.

Tuje kwako, unaweza kufanya kazi bure kisa tu huruma?
 
Hakuna sehemu ambapo pesa haipewi kipaumbele, ndio maana kila kukicha watumishi wanalia lia wapandishiwe mishahara.

Tuje kwako, unaweza kufanya kazi bure kisa tu huruma?
Unaweza kumuacha mtu afe kisa pesa na una uwezo wa kuokoa uhai wake?
 
Huyo ni mmoja aliyekufa kwa kusoma huduma sababu ya kipato ila wapo wengi sana wanaokufa sababu kama hizo.
Ukitaka kujua hospitali zetu zina mifumo ya hovyo umwa serious

Jamani maskini wenzangu tuzichunge sana afya zetu maana zikitetereka kidogo tu tumeenda na maji.
Ilinde afya yako kwa gharama yoyote.
 
Huyo ni mmoja aliyekufa kwa kusoma huduma sababu ya kipato ila wapo wengi sana wanaokufa sababu kama hizo.
Ukitaka kujua hospitali zetu zina mifumo ya hovyo umwa serious

Jamani maskini wenzangu tuzichunge sana afya zetu maana zikitetereka kidogo tu tumeenda na maji.
Ilinde afya yako kwa gharama yoyote.
Nyie kwenye fields zenu huwa mnatoa huduma bure kisa huruma?
 
Ujauzito sio Dharura, Huyo mjamzito alikua ana Miezi 9 ya kujiandaa kifedha.
Haya ni maelezo ya mtu aliyeshiba, au mtoto au hajawahi kukumbwa na majanga.

Kuna wakati inatokea unakosa hiyo pesa na huwezi kuacha kutengenezea familia.

Watu wa zamani wangekuwa waoga wa haya mambo tusingezaliwa.
 
Wote wachukuliwe hatua akiwemo na mwanaume aliyemtia mimba na nduguze huyo mwanaume wakamatwe.kwa kutia mimba.na kutowajibika hata kutoonekana tu hapo hospitalini wanaachia mama mkwe anahangaika peke yake
Mkuu uko serious kweli? Hosp sio shughulini watu mkajazane, na pia mama mtoto hakuwa na shida yoyote zaidi ya kucheleweshewa kupatiwa huduma.

Kama mwanaume hujui kuna utafutaji? Unajua vipi kama baba mtoto alikuwa anahaha kusaka namna ya kumsaidia mkewe?

Kwa jinsi habari ilivyo ningeshangaa kama mwanaume nae angekuwa hospitali badala ya kutafuta.
 
Ni huzuni sana jamani yani sasahivi watu hawaangalii utu kabisa!
Si wangemsaidia kama wanavosaidia wengine jamani Nimeumia sana!
 
Watashikana tu uchawi kinafiki.
Sera za serikali upande wa afya ni mbovu. Masikini hana thamani nchi hii.
Pole mama yangu Mungu akutie nguvu kulihimili hili.
 
Madaktari walisharuhisiwa kupiga kazi private ndani ya kituo cha kazi eti baada ya muda wa kazi.
Inawezekana mama marehemu aliingia muda wa private.
ummy Mwalimu
 
Ila watu nao wapunguze kuzaa hovyo bila kujipanga watu wengi wanazaaa hajali ana pesa ya kujikimu au la
Madaktari nao wana makosa kwanin wasimfanyie upasuaji akipona alipe hiyo pesa ubinadam kwanza pesa baadae
 
Mwanaume tafuta pesa umhudumie mkeo ipasavyo, Kwani mumewe yupo wapi coz naskia tu mama. Inaumiza lakini.
 
Hilo linawezekana pasi na shaka.

Huko ni kwa Mheshimiwa waziri wa afya, ngoja tusikie atasema nini.
Gharama za matibabu Tanzania ni ghali mno na sishangai kusikia hivi maana hospital ni biashara TU kama biashara zingine hapa nchini
 
Kazi za utabibu zinahitaji watu wenye mioyo sana, sasa unakutana na lijitu limaskini lina madeni ya kausha damu, mwingine kazalishwa kaachwa yaani lazima roho iwe usugu wa kuzoea kuyaona maumivu ya wengine.
 
Back
Top Bottom