Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

Pia soma > Watumishi 3 wasimamishwa kazi kwa kusababisha Kifo cha Mjamzito kisa hajatoa Tsh. 150,000
Inaumiza sana [emoji3064]
 
Hata ili KIZIMKAZI litapita bila kuchukua atua yyte. Watanganyika tuamke mm na familia yangu pamoja na ukoo tumeamka. Hakuna anacho weza zaidi y kuteua na kutengua tu. Iyo KAZI Yuko tayri kuifanyia kila wiki,mwezi na mwaka.
 
Ethically hawakuwa Sawa hata thumni ila systematically wako sawa ...

Kwanini kun vitu kuu mbili kubwa hapo Ya kwanza ni ethics Hapo akipelekwa kwenye vikao vya Baraza la Taaluma kafanya Negligence iliosababisha kifo so yuko Hatiani..

Lakini lets Assume alimtibu mgonjwa na hakutoa hela hiyo ni vita nyingine ya Pili ni vita ya kimapato ambayo ndo hiyo vita ya system..
Haya matukio huwa ni magumu sana kuamua ikifika hapa..

Ndo maana kuna muda me nagombana na watu sana ni bora kutoa na kumuombea mgonjwa temporary Exemption hata kama itakucost Posho yako ila sio Kusababisha kifo
Na hiyo ndiyo concern yangu, nchi hii umaskini wa kipato ni mkubwa sana haswa huku vijijini. Serikali inakosea sana na kuwa weka wahudumu wa afya kwenye wakati mgumu sana, uhai wa mtu hauna mbadala, wawe wanatibiwa then wanachi tunaambiwa tuwachangie tu, kama serikali imeamua iwe hivyo.
ndugu yangu hakuna bure
Mkuu wa wilaya akasema ni bure, wewe unapinga
 
Umasikini mbaya sana ,masikini maisha yake ni yakubahatisha Kila nyanja daah so sad [emoji24]
 
Haya majibu YENU

IMG-20231115-WA0000.jpg
 
Wenzao wanaweka kama deni ila wakati tayari amepata huduma asa why hawa walimfanyia ukatili huo kama ni kweli kuna ulazima madaktari kuwajibishwa vikali ila serikali yetu hii utakuta anahamishiwa kituo​
 
Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

Pia soma > Watumishi 3 wasimamishwa kazi kwa kusababisha Kifo cha Mjamzito kisa hajatoa Tsh. 150,000
Kwa upande wa pili, hili tukio ukilisikiliza vizuri, linaonekana kama huyu mama alifanyiwa upasuaji ila wapasuaji wakakosea na kupelekea mama kufariki dunia.

Baada ya hapo watu wakaogopa MURDER CASE wakaona bota iwe ni jinai hiyo angalau wanaweza kuikabili

Ukiwasilkiliza vizuri mashahidi pamoja na mume wa mtu; inaonyesha kabisa kuwa hawa watu hawakuwa willing kumdai mama huyu pesa kabla ya upasuaji

Hili tukio inabidi Serikali walianggalie vizuri na wajiridhishe kama kweli tunachokisikia ndiyo hicho kilchotokea

Kuna uwezekano mkubwa watu wamekwepesha MURDER CASE hapa
 
Na hiyo ndiyo concern yangu, nchi hii umaskini wa kipato ni mkubwa sana haswa huku vijijini. Serikali inakosea sana na kuwa weka wahudumu wa afya kwenye wakati mgumu sana, uhai wa mtu hauna mbadala, wawe wanatibiwa then wanachi tunaambiwa tuwachangie tu, kama serikali imeamua iwe hivyo.

Mkuu wa wilaya akasema ni bure, wewe unapinga
Oooh haya peleka mkeo bure uone
 
Umaskini sio kitu chemaaaa..either una bima au beba helaaa otherwise utaishia kuchukia tu watoa huduma au upoteze uhai.
 
Tatizo lenu mnaendekeza siasa za CCM. Naomba nkueleweshe mkuu.
Ili Cesarean section ifanyike utahitaji vitu vifuatavyo.
1.Madripu ya Maji (Utaandikiwa Idadi)
2.Nyuzi za kushonea (Utaandikiwa Idadi)
3.Gauze
4. Mipira ya kuvaa mikononi
5.Surgical Blade.

Hivyo ni baadhi tu.

Hivyo basi kwa kuwa hizo bidhaa hutolewa bure vituoni,huwa havikidhi mahitaji..mzigo unaweza kuja leo kutoka MSD ambao ukakidhi kwa akina mama watano tu kwa mwezi,hao wengine wakija automatically mzigo umeisha. Hivyo ili afanyiwe Cesarean section anaandikiwa aende dukani akanunue ili afanyiwe. Maana huwezi kufanya bila hivyo vifaa.

Ndo maana nimekuuliza,unataka mtoa huduma afanyaje? Je watoe pesa zao mifukoni?

Serikali yenu inawalaghai kuwa vifaa vipo mahospitalini na nyie mnaamini.lakini kiuhalisia mahitaji hayatoshelezi. Vifaa vinavyo letwa na MSD ni vichache ukilinganisha na mahitaji husika.. na isitoshe hutumika bure hivyo vichache pale vinapo kuja.
Sikitiko kuu ni pale wananchi hilo jambo hawaliamini .

Ukijikita una huruma ndiyo mwanzo wa kusema umehujumu mapato .
 
Back
Top Bottom