Usiwe kama Antoniette 1st lady na mama mfalme wa Ufaransa ya kale.
Njaa ilipokuwa imetamalaki nchini mwake, yeye yupo kuwashangaa watu wake masikini wanavyokufa kwa njaa: "kama mikate haipatikani, kwanini wasile keki?"
Ndiyo nawewe akili zako zimeegemea upande wa mawazo kama hayo.
Unashangaa miezi 9 ya mjamzito kukosa hela ya dharula ya kujikimu!
Maisha ya kijijini hata mjini kwa watu walio wengi ni ya dunia nyingine, usije ukawaza kirahisi namna hiyo.
Kuipata tu elfu 10 kwa mtu fukara ni msamiati usio na majawabu.
Aipateje, auze nini mtu asiyemiliki chochote zaidi ya kibanda mbavu za mbwa ama kutokuwa na chochote anachomiliki kabisa?
Kuipata hela ya kula kwa siku moja ni tabu tupu, sembuse kuweka akiba!
Wewe kama Mungu amekujalia maisha mazuri kuweza kula na kujiwekea akiba, shukuru, lakini ukae ukijua kuwa maisha ya waTz walio wengi hasa kipindi hiki, wanaishi chini ya mstari wa umaskini.