Tanganyika na Tanzania ya ovyo ni zao la Hayati Mwalimu Nyerere

Huyu jama kapokelewa na waislamu wa pwani wakamuamini wakamsaidia kwa harakati zote alivyo pata uraisi akaanza kubaguwa waislamu kisiasa na kielimu, kafiri ni kafiri ata umsaidie je atakuja kukupenda
Hili sio kweli ni propaganda, Nyerere alirithi legacy ya wakoloni ambao walijenga shule kwenye maeneo yaliyokua na wakristo wengi kwa kutumia wamisionary, then pia utamaduni WA kusoma secular education haukuwa muhimu kwa waslam kutokana na mapokea ya dini yenyewe ambayo iliwekwa zaidi kwenye elimu ya dini .
Ingekua Nyerere ana ubaguzi basi pia angekua mbaguzi WA kikabila au kikanda, maana mara haukua mkoa ambao una shule nyingi .
Waislam wanalalamika walifanyiwa ubaguzi lakni hawaelezi huo ulifanyikaje, yaani hawatoi ushahidi.
 
Kwamba miaka 24;ya utawala wa Nyerere Haina athari kwa Tanzania?!..kufukia shimo la miaka 24 so kazi ndogo, ujerumani ilichakaa WWII,Leo uchumi mkubwa ulaya,ilichukua miaka mingapi?..unajua nchi aliyorithi mwinyi!?..hovyo,raia viraka tu,njaa,shule hakuna,hebu fikiria mwinyi angerithi nchi kiuchumi imechangamka Kama kipindi Cha jakaya,Leo tungekua wapi?..scent ya Nyerere itakuwepo walau kwa miaka 30 ijayo
Uko sahihi kabisa ila kinachoharibu Watanzania wengi ni mapenzi tu kwa mtu wanayemwamini.
Nyie ni wavivu na wazembe wa mabadiliko ndio maana hii Tanganyika bado iko hapa, wavivu wa kifikra na kiutendaji.

Siwezi kupoteza hata sekunde moja kumlaumu Nyerere aliyeondoka duniani zaidi zaidi ya miaka 20 iliyopita, na madarakani zaidi ya miaka 30 iliyopita, kwa matatizo yanayonikuta leo?

Ukijumlisha hiyo miaka tangu Nyerere aondoke madarakani, na duniani, ni zaidi ya miaka 50, sasa iweje kwa miaka yote hiyo bado tusiweze kurekebisha makosa yake na kuishia kumlaumu?!

Nyie ni wajinga wapuuzi msio na aibu.
Tunakubali kuwa sisi ni wajinga na wapuuzi kama unavyotuita lakini kumbuka kuwa huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaolalamikiwa kila siku na Watanzania wengi chimbuko lake ni Nyerere.Madini au migodi mingi tuliyonayo Tanzania kutowasaidia au kuwanuufaisha Watanzania sababu ni fikra za Nyerere.Hiki Chama Cha Mapinduzi ufedhuli wake sababu ni Nyerere aliounda Sera ya ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CCM.
Leo Mwenyekiti wa CCM amesaini Mkataba wa DP World unasemaje mnufaika wa mambo ya Nyerere?
 
Mimi najiulizaga hata huo Muungano wa ASP + TANU = CCM.... yaani hapo hizo C, C na M wamezitoa wapi?
C-Chama + C-Cha + M-Mapinduzi.
ASP iliendelea kuwepo baada ya mapinduzi, TANU inaonekana kushirikishwa katika kuunda chama kimoja. Swali ni Je, TANU ilishiriki kufanya mapinduzi ? 🤔
 
Hili sio kweli ni propaganda, Nyerere alirithi legacy ya wakoloni ambao walijenga shule kwenye maeneo yaliyokua na wakristo wengi kwa kutumia wamisionary, then pia utamaduni WA kusoma secular education haukuwa muhimu kwa waslam kutokana na mapokea ya dini yenyewe ambayo iliwekwa zaidi kwenye elimu ya dini .
Ingekua Nyerere ana ubaguzi basi pia angekua mbaguzi WA kikabila au kikanda, maana mara haukua mkoa ambao una shule nyingi .
Waislam wanalalamika walifanyiwa ubaguzi lakni hawaelezi huo ulifanyikaje, yaani hawatoi ushahidi.
Uko sahihi na leo Palestina ni marufuku kwa Wanawake kusuka nwele,kuwa na saloon pamoja na kusoma shule.
 
Nyie ni wavivu na wazembe wa mabadiliko ndio maana hii Tanganyika bado iko hapa, wavivu wa kifikra na kiutendaji.

Siwezi kupoteza hata sekunde moja kumlaumu Nyerere aliyeondoka duniani zaidi zaidi ya miaka 20 iliyopita, na madarakani zaidi ya miaka 30 iliyopita, kwa matatizo yanayonikuta leo?

Ukijumlisha hiyo miaka tangu Nyerere aondoke madarakani, na duniani, ni zaidi ya miaka 50, sasa iweje kwa miaka yote hiyo bado tusiweze kurekebisha makosa yake na kuishia kumlaumu?!

Nyie ni wajinga wapuuzi msio na aibu.
Wawalaumu pia waarabu waliowatawala miaka 1,000
 
C-Chama + C-Cha + M-Mapinduzi.
ASP iliendelea kuwepo baada ya mapinduzi, TANU inaonekana kushirikishwa katika kuunda chama kimoja. Swali ni Je, TANU ilishiriki kufanya mapinduzi ? 🤔
Wazenji kwa kudeka na kujidai mnaonewa hamujambo.
ASP alianzisha Nyerere usiku wa tarehe 5/2/1957 mtaa wa Kariakoo Michenzani Zanzibar.
Nyerere alianzisha akiwepo msaidizi wa Katibu wa Tanu Zubeir Mtemvu.
Mwalimu Nyerere aliwaajiri Mmalawi Abeid Karume aliekuwa anatetea wafanyakazi weusi wakati wa unyanyasaji na alitumia tawi la Tanganyika African Association ya Nyerere (Zanzibar yeye na Nyerere walikiita simple tu AFRICAN ASSOCIATION).

Mbinu za Zanzibar kujiondoa CCM ilikuwa ajenda ya Amani Karume Rais wa Zanzibar 2000 hadi 2010, sasa ajenda hiyo ipo kazini sana, ili Zanzibar iwe na Mamlaka kamili juu ya siasa. Hili ndio kosa halisi lililomfukuza Ali Karume kulikataa na kulipigia kelele kuwa sio jama jema Zanzibar kujitoa CCM taifa. (Ali Karume ndio kati ya watoto wa hayati Karume ndie anopenda Muungano) Amani hapana hata kidogo.
 
Kama Nyerere alikosea wewe unashindwa nini kurekebisha makosa yake?

Wewe ndie mjinga zaidi ya Nyerere, kwasababu tatizo unaliona, lakini umeamua kuliacha hivyo hivyo huku ukibaki kumlaumu Nyerere.
Sasa mkuu,

Kwa mifumo iliyopo ya wanasiasa na viongozi wakubwa kuwa na kinga kubwa ya kuto kukosolewa una anzaje kurekebisha makosa?
 
Uko sahihi kabisa ila kinachoharibu Watanzania wengi ni mapenzi tu kwa mtu wanayemwamini.

Tunakubali kuwa sisi ni wajinga na wapuuzi kama unavyotuita lakini kumbuka kuwa huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaolalamikiwa kila siku na Watanzania wengi chimbuko lake ni Nyerere.Madini au migodi mingi tuliyonayo Tanzania kutowasaidia au kuwanuufaisha Watanzania sababu ni fikra za Nyerere.Hiki Chama Cha Mapinduzi ufedhuli wake sababu ni Nyerere aliounda Sera ya ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CCM.
Leo Mwenyekiti wa CCM amesaini Mkataba wa DP World unasemaje mnufaika wa mambo ya Nyerere?
Bora usiandike kitu, hujielewi kabisa.

Umefikia mpaka stage ya kumlaumu Nyerere kwa madini tuliyonayo kutolisaidia taifa.!!

Hujui Nyerere alisema hayo madini yaachwe huko ardhini mpaka watanganyika watakapokuwa na uwezo wakuyachimba ndio wayachimbe?

Kitu gani kilifanya ushauri wake usifuatwe? hilo ni kosa la Nyerere?! Stop this please.

Mambo ya muungano na kero zake, nimeshakuonesha na wenzio miaka zaidi ya 50 tangu Nyerere atupishe, kitu gani kinatushinda kuuvunja, au kuurekebisha huo Muungano?

Nawaita wajinga for a reason, siwaonei, mnaonesha kabisa hamjielewi, wala hamkielewi hiki mnachokitetea hapa.
 
Sasa mkuu,

Kwa mifumo iliyopo ya wanasiasa na viongozi wakubwa kuwa na kinga kubwa ya kuto kukosolewa una anzaje kurekebisha makosa?
Upelekwe muswada bungeni kurekebisha hiyo sheria, mbona simple tu. Nyerere anahusika nini hapo?
 
Kambona baada ya kuleta upinzani Mchonga akaanza kumwita Malaya..

Kambona angetupaisha sana kuliko tulivyo sahivi.
 
Bora usiandike kitu, hujielewi kabisa.

Umefikia mpaka stage ya kumlaumu Nyerere kwa madini tuliyonayo kutolisaidia taifa.!!

Hujui Nyerere alisema hayo madini yaachwe huko ardhini mpaka watanganyika watakapokuwa na uwezo wakuyachimba ndio wayachimbe?

Kitu gani kilifanya ushauri wake usifuatwe? hilo ni kosa la Nyerere?! Stop this please.

Mambo ya muungano na kero zake, nimeshakuonesha na wenzio miaka zaidi ya 50 tangu Nyerere atupishe, kitu gani kinatushinda kuuvunja au kuurekebisha huo Muungano?

Nawaita wajinga for a reason, siwaonei, mnaonesha kabisa hamjielewi, wala hamkielewi hiki mnachokitetea hapa.
Hasira ni hasara ndugu yangu kama kuna sehemu tunakosea sahihisha kwa vigezo yakinifu vijembe havijengi hata sisi tuna maneno ya shombo vile vile na ukumbuke duniani hakuna malaika na hata wewe kwenye familia ukiwa na watoto watano pamoja na kuwahudumia kila kitu usifikiri wote watakupenda lazima wawepo ambao wewe ni kero kwao.
 
Nonsense.

Chukia mtu for a reason, sio kwa vijisababu vya kipuuzi.

Bahati mbaya sina kipaji cha kubembeleza wajinga, sorry.
 
Ujumbe wa siku
bbe5a0d4da184a9e88ec7e95a76b21f9.jpg
 
Nonsense.

Chukia mtu for a reason, sio kwa vijisababu vya kipuuzi.

Bahati mbaya sina kipaji cha kubembeleza wajinga, sorry.
Uliwahi kumuona Lissu akimtukana Nyerere live? Jionee.

Siku nilivyomuona Lissu akisema hivyo nikasena huyu sasa kajichoka.
 
Back
Top Bottom