Wengine sio kufia hospital wako wanaokotwa wamekufa hawajulikani au ajali ya moto imetokea kama malori ya mafuta yakalipuka kama Morogoro ilivyotokea miili ya watu ikaungua kiasi kuwa haitambuliwi au case kama za MV Bukoba kuna watu meli ilipozama hawakutambuliwa na ndugu wakazikwa na serikali kwa heshima
 
Aise! Hivi Kibiti si iko Mukaranga?
Lakini wakati tunajihoji wale wasio na ajira wachangamkie hii post!
 
ngoja watekaji waje watuambie majibu ya hayo maswali matano

“Baadhi tunazikuta na majeraha makubwa yanayohisiwa ni ya risasi au mapanga hasa vijana wenye kati ya miaka 25 hadi 35,” alisema Lugendo.
 
😆😆😆😆
 
Exquisite [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania tuna low IQ nimekueleza hapo juu kuwa shida ya hili tangazo ni kwa kuwa likewekwa mitandaoni tuu ndio unaona kitu kipya hiki?

Umeelewa niliposema ya kwamba "SHIDA NI KUTOLEWA TANGAZO LA KAZI YA HIYO NAFASI MITANDAONI?"
Nikuulize mwenzetu umezaliwa wapi huenda tukapata majibu mazuri ya kukuelewesha.
 
[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hili lipo miaka mingi ni kweli. Kosa hapa ni namna walivyotangaza nafasi. Kuzika ni moja ya majukumu mengi kuhusu watu wenye nafasi hizi hasa ikizingatiwa kuwa sehemu kama hiyo huwa haina maiti wasiotambulika kwa wingi. Sehemu zenye miili mingi ni mijini.
 
Hawa maiti wanatokea wapi?
Tangazo hili hapa👇
Kwa Maoni yangu, kuna mambo kadhaa ambayo yamesababisha kuibuka kwa sintofahamu au mashaka kuhusiana na tangazo hili la ajira za kuzika maiti za Watu huko Mkuranga, baadhi ya sababu hizo ni:-
1. Udogo wa mji wa Mkuranga na idadi ndogo ya Watu waishio kwenye mji au Wilaya hiyo, sambamba na Hali yake ya kupokea wageni kutoka nje ya eneo Hilo.
2. Kuwepo kwa Historia mbaya ya mji huo kuhusiana na suala zima la Usalama wa Watu. Watu kutekwa, kuuawa na/au kupotezwa.
NB:
Mkuranga ni miongoni mwa miji iliyopo katika 'zone' ya eneo tete la kiusalama la MKIRU (Mkuranga, Kibiti, na Rufiji).
3. Kuwepo au kushamiri kwa matukio ya kutisha ya Watu kutekwa, kupotezwa na/au kuuawa na 'Watu wasiojulikana' hapa nchini kwa sasa.
4. Timing of the Advert,
Muda au wakati wa kutolewa kwa tangazo hili Siyo rafiki Sana kutokana na ukweli mchungu sana kwamba kwa sasa nchi hii inakabiliwa na 'taharuki kubwa' ya Watu kutekwa na kupotezwa au kuuawa.
Jambo hili kwa upande fulani fulani limechagiza pakubwa kuzua taharuki juu ya tangazo hili la ajira za kuzika maiti ambazo hazijatambuliwa na ndugu huko Mkuranga.
 
Ifike mahali tuache upuuzi sasa kuna lipi jipya hapo..... Tunakua wajinga WA uhuru sasa
Tatizo ni hili. Sehemu za vijijini mara nyingi haina miili mingi ya watu wasiojulikana. Hii ni kwa sababu watu wengi wa vijijini wanajuana na siyo kama mjini. Hivyo basi tangazo lingeweka kipengele cha kuzika kiwe kama sehemu ya kazi ya usafi.
 
Kuna baadhi ya watanzania kuna shida mfano kitu hakielewi badala ya kusema jamani hili tangazo sijaelewa kuuliza si ujinga aliyeelewa afafanue anakuja na ujuaji

Watanzania baadhi tujifunze kutumia lugha kama huelewi kitu vizuri unaomba msaada kuwa kuna hiki sikielewi wenye uelewa nisaidieni

Kuliko kukurupuka tu kuwa hao maiti wasiojulikana nawajua na msababishaji namjua

Ndio maana wazungu wako wazi wanasema watu ambao wako tayari kuelimishwa kitu wasichojua ni wazungu,waaasia ,na wajapani wanaamini kuwa waafrika wanakera ni wajuaji na hawafundishiki na wasichokijua wagumu kukubali kuwa hawajui wawe marekani,Afrika au popote

Ndio maana waafrika ni jamii iliyo nyuma mno kimaendeleo kuliko race zingine kisa u much know kiasi wanaojua wanazira ku share knowledge
 
You are a great thinker dear. Nakuunga mkono kabisa. Mimi nimesema kuwa tangazo lingekuwa la mtu wa kufanya usafi na moja kati ya vipengele iwe ni kuzika iwapo itahitajika, basi kusingekuwa na shida sana. Hii ni kwasababu vijijini watu wanajuana na ni mara chache kupata miili isiyotambulika. Mtoa tangazo ni mbulula na hana ujuzi na mawasiliano kwa umma.
 
Amen
 
Huyu bidada alipoteza uwezo wa kufikiri na busara kitambo Sana alipo chagua kuipa siasa kipaumbele kwenye maisha yake.
Maiti zisizotambuliwa na ndugu ni nyingi sana toka miaka hiyo ya zamani.
Huzikwa na manispaa au halmashauri au jiji. Miaka yote angeenda makaburi maarufu angeona mazishi yake yapoje.
 
No, You are wrong. Hoja zake zina mashiko kuhusu suala hili.

Kwa Maoni yangu, kuna mambo kadhaa ambayo yamesababisha kuibuka kwa sintofahamu au mashaka kuhusiana na tangazo hili la ajira za kuzika maiti za Watu huko Mkuranga, baadhi ya sababu hizo ni:-
1. Udogo wa mji wa Mkuranga na idadi ndogo ya Watu waishio kwenye mji au Wilaya hiyo, sambamba na Hali yake ya kupokea wageni kutoka nje ya eneo Hilo.
2. Kuwepo kwa Historia mbaya ya mji huo kuhusiana na suala zima la Usalama wa Watu. Watu kutekwa, kuuawa na/au kupotezwa.
NB:
Mkuranga ni miongoni mwa miji iliyopo katika 'zone' ya eneo tete la kiusalama la MKIRU (Mkuranga, Kibiti, na Rufiji).
3. Kuwepo au kushamiri kwa matukio ya kutisha ya Watu kutekwa, kupotezwa na/au kuuawa na 'Watu wasiojulikana' hapa nchini kwa sasa.
4. Timing of the Advert,
Muda au wakati wa kutolewa kwa tangazo hili Siyo rafiki Sana kutokana na ukweli mchungu sana kwamba kwa sasa nchi hii inakabiliwa na 'taharuki kubwa' ya Watu kutekwa na kupotezwa au kuuawa.
Jambo hili kwa upande fulani fulani limechagiza pakubwa kuzua taharuki juu ya tangazo hili la ajira za kuzika maiti ambazo hazijatambuliwa na ndugu huko Mkuranga.
 
Siipendi CCM lakini CHADEMA ina wajinga wengi kuliko.
Ni kikundi cha wanaharakati uchwara wanaokosa fikira makini kabla ya kufungua midomo yao hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…