Kwa Maoni yangu, kuna mambo kadhaa ambayo yamesababisha kuibuka kwa sintofahamu au mashaka kuhusiana na tangazo hili la ajira za kuzika maiti za Watu huko Mkuranga, baadhi ya sababu hizo ni:-
1. Udogo wa mji wa Mkuranga na idadi ndogo ya Watu waishio kwenye mji au Wilaya hiyo, sambamba na Hali yake ya kupokea wageni kutoka nje ya eneo Hilo.
2. Kuwepo kwa Historia mbaya ya mji huo kuhusiana na suala zima la Usalama wa Watu. Watu kutekwa, kuuawa na/au kupotezwa.
NB:
Mkuranga ni miongoni mwa miji iliyopo katika 'zone' ya eneo tete la kiusalama la MKIRU (Mkuranga, Kibiti, na Rufiji).
3. Kuwepo au kushamiri kwa matukio ya kutisha ya Watu kutekwa, kupotezwa na/au kuuawa na 'Watu wasiojulikana' hapa nchini kwa sasa.
4. Timing of the Advert,
Muda au wakati wa kutolewa kwa tangazo hili Siyo rafiki Sana kutokana na ukweli mchungu sana kwamba kwa sasa nchi hii inakabiliwa na 'taharuki kubwa' ya Watu kutekwa na kupotezwa au kuuawa.
Jambo hili kwa upande fulani fulani limechagiza pakubwa kuzua taharuki juu ya tangazo hili la ajira za kuzika maiti ambazo hazijatambuliwa na ndugu huko Mkuranga.