Tangu asubuhi sijauza hata Tsh. 100 aisee

Haya maisha bhana! Biblia inasema Njia za Mungu hazichunguziki! Sielewi kabisa

Kuna watu nawajua walikua wanatoa fungu la 10, kanisani kwa sana, Maombi kabla na baada ya biashara lakini biashara zao zilifirisika mitaji ilikata na walikua na huduma nzuri kwenye biashara.

Mbona naona wanaofata kanuni za Kimungu ndio maskini? Mambo yao hayaendi?

Huu ushauri wako ninaukataa sababu nimeona haujafanya kazi kwa watu wengi.
 
Sikia ndugu...

Achana na yote ya JF, kaa ndani jifungie piga magoti, muombe Mungu kwa imani kuu, naye atakufungulia vyema.

Waganga sikushauri, unless kama una imani ya waganga toka mwanzo.

Asante!!!
 
Mkuu jichunguze ,,,vipi katika harakati zako ulishawahi kumuacha mkeo kwenye biashara yako aendeshe hata mara moja iwe kwa dharura au iwe ndiyo kawaida yenu ?

Nb. Wanawake wana midomo michafu na maringo ya kipuuzi kwenye biashara za waume zao kiasi cha kuwakwaza wateja.
 
Haapana mkuu its only me i swear
 
Mwisho kaomba ushauri! Ongea maneno ya kumtia moyo kama huwezi pita hivii..!

Hakuna kitu kibaya kama kukosa ridhki, sasa unavyosema neno kama hili unakua unamkosea mleta mada.
Acha tu mkuu , maumivu ni ya mtu anayoyajua 😭
 
NAKUPA HII, NAOMBA MREJESHO BAADA YA SIKU 7

Loweka Karafuu kwenye maji" mwagia kwenye mlango wa kuingilia dukani kwako au uchome kama vile udi asubuhi na mapema unapoingia dukani kwako au loweka kwenye maji kisha siku inayofuata unanyunyizia yale maji mbele ya duka lako.

MREJESHO TAFADHALI SANA.
 
Mwisho kaomba ushauri! Ongea maneno ya kumtia moyo kama huwezi pita hivii..!

Hakuna kitu kibaya kama kukosa ridhki, sasa unavyosema neno kama hili unakua unamkosea mleta mada.
Mbona unapenda kuniandama? Mimi nimeuliza. Lakini unawezaje kumshauri mtu bila kuwa well informed? Hajasema hata anauza nini na wapi
 
Hii nafanya kwa siku saba. Au ni mara moja tu mkuu wangu?
 
Hardware ya vifaa vidogo vidogo

Zamani nishawahi kuuza kwa boss fulani.

Sekta ya hardware huwa inategemea hali ya hewa na hali ya hela na ushindani
Kama kuna ushindani wape ganji mafundi wakileta wateja wa kununua vitu vingi unawapa hela. Pia hardware msimu wa mvua biashara huwa inasizi hadi mvua ziishe kuanzia mwezi wa saba na wa nane


Wazo lingine
Pia ongea na watu wa malori na matipa wakupe location wanakopeleka mchanga,kokoto,tofali kwenye njia panda ya mitaa hiyo ambako watu ndio wanaanza kujenga ndio ukaweke hardware huko.


Biashara ambazo hazina msimu ila faida ni ndogo mno ni bidhaa matumizi ya nyumbani, ngano, maji, juisi,soda, sembe, Dona, mafuta ya kula, mchele, maharage, sabuni ya kipande, sabuni ya unga, sukari, chumvi, pedi za wanawake na pampas za watoto
 
Hii nafanya kwa siku saba. Au ni mara moja tu mkuu wangu?
Fanya siku 7 mfululizo, kisha utafanya hii kwa ajili ya ulinzi wa biashara yako

Tumia Chumvi nyeusi ni mchanganyiko wa chumvi hii ya ungaunga pamoja na vumbi la udi, nikisema vumbi la udi namaanisha lile vumbi linalobakia baada ya udi kuungua, vumbi lake lile sasa lichukue uchanganye na chumvi ya unga ili kutengeneza chumvi nyeusi ambayo inaweza kutumika kwa ulinzi nyumbani kwako, chumbani kwako, kazini kwako, kwenye biashara zako n.k. pia inasaidia kuondoa nishati (energy) mbaya inayozunguka maeneo hayo niliyoyataja. Weka sehemu ya chini ya mlango wako yaani unyunyizie chini ya mlango wako ili kuzuia wavamizi, nikisema wavamizi nafikiri umenielewa?

Udi ni wowote unaweza kutumia ila ikiwa utapata udi Basil, Cinnamon, Rose Geranium, au Gingeroot itakuwa nzuri zaidi, hizi unazipata duka la dawa za asili.

Naomba ulete mrejesho hapa hapa kuanzia tarehe 8 mwezi huu
 
πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿 Ahsante mtaalamu wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…