Unaona hilo swali la kimtego inamaana Mungu alikua anajua kila kitu maana yeye ndiye mpangaji wa kila kitu kila kilichopo na kilichotokea kilipangwa na yeye mwenyewe Adamu na Hawa wala hawakujua mipango ya Mungu kumbe Mungu alikua amepanga kuwatimua kwa kumtumia Shetani km Chambo ila kila kilichokua kinaendelea alikua anaona lab rat wanavyofanya anawachora tu kashajua huyu panya akipita hata atatokea pale ataenda pale nikimtoa hapa nitamuweka pale umeona hio kitu hapo au bado umefumbwa macho? Mungu mpango mzima alikua anaujua mpaka stage ya kuwatimua itakuaje alikua anajua kila kitu maana alishaandaa kila kitu ukizama deep utaelewa jambo kwamba kila lililotokea lilikua ni mpango wake yeye mwenyewe unakuja kugundua Shetani kasingiziwa yaan Mungu alishindwa kumzuia Shetani pale alikua anamuona au Mungu alienda kwa Mwanamke akiwa kwenye umbo la Shetani? Maswali magumu km hayo unabidi ujiulize kwanza
Ukweli ni kwamba shetani hakusema uongo wowote bali alimwambia ukweli halisi Eva.
Na nukuu halafu tuchambue verse by verse.
Mwanzo 3:1-7, 22-23 (KJV) Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.
UCHAMBUZI KWA KINA.
4* Nyoka alimwambia Kwa kumhakikishia 100% kuwa hakika hamtakufa. Funguka la5 anampata ukweli 100% kuwa Mungu anajua siku mkila matunda hayo mtafumbuliwa macho Nanyi mtakuwa kama Mungu Kwa kujua mema na mabaya.Ni ukweli walifumbuliwa macho na wakajua mema na mabaya.
Funguka la7 linaweka ukweli huo kuwa walifumbuliwaacho "Mara macho Yao yakafumbuliwa" Hadi hapa tunaona shetani hakusema uongo kabisa Bali ukweli wote.
Ukumbuke fungu la 4 shetani alimwambia mwanamke hakika hamtakufa.... Sasa ukweli wa shetani anauthibitisha Mungu mwenyewe kwenye fungu la 22 na nukuu...
Mwanzo 3:22 (KJV) Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Hapa Mungu mwenyewe anakiri wazi kabisa kuwa huyu mtu amekuwa kama yeye(Mungu) Kwa kujua mema na mabaya. Mungu anasema lazima kumzuia huyu mtu kula lile tunda la mti wa uhai(uzima) kwani akilila ataishi milele. Fungu la 23 Mungu anachukua maamzi ya kumtimua huyu mtu Busta Nini. Shetani hakuwa na kosa kabisa Bali aliwaeleza ukweli akiwa hakikisha hawatakufa kama tu wangekula lile tunda la uzima(uhai) maana hatujawahi ona kuwa kulikuwa na tunda la kifo ama mauti halikuwepo hivyo adamu angelikuwepo Hadi Leo kama asingefukuzwa na Mungu mwenyewe.