Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Kizazi Cha ovyo sana hiki, kunyimwa utelezi, kuambiwa ujifunze kupika na uanze kufua unapatwa na makasiriko hivyo ? Take easy bro maisha ni mapambano .

Fuata ushauri huu.

Kwanza kubali kuwa uko kwenye kipindi Cha mpito kinachobadiri mtazamo wako juu ya maisha na ndoa. This season utajua nini maana ya kuomba kuwa na make supportive in this life na umhimu wa kuwa na uchumi imara.

Dharau zote unazohisi unafanyiwa ni mtazamo tu , potezea , kuwa positive, msaidie mkeo , Huku daily ukijipanga.


Utaona na kusikia mengi ila jipe moyo kipindi hiki kitapita. Omba Mungu tu wife akianza kukazwa nje asikuonyeshe waziwazi coz kwa hasira zako hizo unaweza kujitia kitanzi.

Mwisho , usiache kumpa Yesu maisha yako , atakuwa Mungu wako msaada utakaokusaidia upitapo kwenye bonde la uvuli wa mauti
 
Mke asie na kazi tofauti na mume asie na kazi, mke akiwa nyumbani kuna kazi nyingi atafanya sasa mume anaeshinda nyumbani kwamba afue, apike, afanye usafi, aoshe watoto si ndio kelele zitazidi mwanaume anadharauliwa kisa hana kazi wakati kwa mwanamke ni kawaida tu.
Kabisa yaan
 
asante mkuu nmefikiria kuondoka mimi sababu tunaishi nyumba ya kupanga kuna kiwanja nilinunua kwa ajili ya ujenzi ila nmeishia kumwaga tofali tu kwanza
Pambania Mjengo wako kwanza,atakuja mwenyewe baada ya Mjengo kuisha! Si anapenda kamselelekoo!? Wwe mwachee atalipata analo litafuta!!!
 
Hakuna mwanamke wa kukaa mahali ambapo hapana uhakika hata ukaoe mzaramo wa Samvula Chole eti dela la shughuli hana kisa anakuvumilia *****.
Ebu msome tena mleeta maada, kasema "Mahitaji ya Nyumbani kwake anatimiza, yeye japokua Mke wake ana mshahara Mkubwa sana!!!"
 
Habari za jioni wanajukwaa wa MMU, ikiwa mmetoka katika mihangaiko akili na mwili vimechoka nawaletea jambo jingine hili tupate kulijadili.

Mimi na mke wangu ni waajiliwa yeye ni mtumishi wa umma na mimi ni mtumishi wa sekta binafsi, ndoa yetu ina miaka mitatu sasa na tuna mtoto mmoja (asante sana MUNGU kwa hili).

Shida iliyonileta kwenu ni kuwa hapa karibuni nimepata matatizo ya kikazi sasa imenibidi niwe nashinda nyumbani kwa sababu mimi siyo mtu wa kukaa nje sana nahisi ndipo matatizo yalipoanzia. Tangu nipatwe na hii hali mke wangu amebadilika tabia sijui kama ni makusudi au lah.

Niwe muwazi kuwa mke wangu amenizidi mshahara lakini pamoja na hayo sijawahi kuona tabia hizi kwake hadi hapo nilipopatwa na hizo shida kazini.

Tabia zipo nyingi ila naleta tatu zilizonishitua;

~ Kwanza amekuwa hataki kushiriki nami tendo.

~ Pili sababu huwa nashinda na mtoto huwa napika kwa ajili yangu na mtoto ambapo ye akirudi anapika kwa ajili ya wote kwani anasema sijui kupika. Sasa hapo juzi kati alinambia itabidi nijifunze kupika kama nataka kuendelea kuwa naye.

~ Tatu ni kuwa tuna machine ya kufulia sasa imeharibika, nikamuomba kuwa nikipata hela tutafanya matengenezo akanijibu kama ni hivyo basi niwee namfulia nguo zikiwemo chupi zake daah.

Mimi nimefikiria uamuzi wa kuachana naye licha ya kuwa na mtoto naye, kwani sina mpango wa kumpiga na hiyo juzi ilibaki kidogo nipige arudi kwao Vunjo Mashariki na ulemavu wa uso alivyosema niwe namfulia.

Nauliza tu wanawake wa humu haya anayofanya mwenzenu ni halali kweli?
Hapo dharau imezidi Mpige chini tu,

Kinachofuata hapo ni kuchapiwa
 
Tatizo ulilikaribisha mwenyewe ulipo oa mchaga wa Vunjo. Mimi huwa nawauliza Sana vijana.
Kwenu hakuna warembo mpaka mkaoe kwa watu?
Ukiwa msambaa, oa msambaa mwenzio hata mbondei, mdigo na mzigua usiguse.
Ukiwa mpare wa usangi, kaoe usangi achana na dada zetu wa Same.
Usioe kwa sababu ya tako. Oa asiye na yako lkn mwenye busara.
Wenye mijitako wako tele Dar. Unajipigia mwenye tako mchana jioni Benet na wife flat screen.
Hahahahaaa..... Jf sitoki.
 
asante mkuu nmefikiria kuondoka mimi sababu tunaishi nyumba ya kupanga kuna kiwanja nilinunua kwa ajili ya ujenzi ila nmeishia kumwaga tofali tu kwanza
Panga vitofali hapo site ziba tiribai anzia hapo,usikubali kuwa mtumwa
 
Kuondoka sio solution mkuu. Cha msingi kaa nae umwambie kama mume kila mtu abaki na majukumu yake. Wewe kama mume utaendelea kuprovide matumizi na yeye kama mke aendelee na majukumu yake haijalishi unashinda nyumbani au vipi as long as matumizi unatoa.
Na inabidi usimame kama mume kipindi hiki maana ukitetereka kidogo tuu utaonja joto ya jiwe mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa anatakiwankazi yake online aiganyie away from home,then ajifanye kazini karudishwa kila kitu kitakuwa shwari
 
Back
Top Bottom