Tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani, anatumia usafiri wa ndege tu, gharama zikoje hapa

Mtoa mada mimi binafsi natumia ndege kuliko gari sembuse Rais? Tuachane na mawazo ya kifukara nchi iko uchumi wa kati
Uchumi wa Kati uchumi mama leo amesema umeshuka na hataweza ongeza mishahara!!!
 
Itakumbukwa katika awamu ya serkali ya tano kila kitu kilifanyika kwa minajili ya kubana matumizi ya Serikali.

Awamu ya sita chini ya Samia Suluhu imekuwa ya kitofauti kabisa na awamu ya tano hususani katika suala la matumizi ya Rais....
Mwenda zake sio Kama alikuwa anabana matumizi Ila mitikisiko ya angani angeweza kupata heart attack
 
Itakumbukwa katika awamu ya serkali ya tano kila kitu kilifanyika kwa minajili ya kubana matumizi ya Serikali.

Awamu ya sita chini ya Samia Suluhu imekuwa ya kitofauti kabisa na awamu ya tano hususani katika suala la matumizi ya Rais...
Hivi mwendazake alibana matumizi yapi, msafara wake tu,na walinzi,mahelkopita , kwa msafara ule wa mh SSH pamoja na kutumia ndege wenda gharama zipo chini,mtu anakaa chato na watu wake siku kibao alafu mnasema kubana matumizi,ni Mara kumi kikwete akisafili Mara nyingi nje ya nchi
 
Itakumbukwa katika awamu ya serkali ya tano kila kitu kilifanyika kwa minajili ya kubana matumizi ya Serikali.

Awamu ya sita chini ya Samia Suluhu imekuwa ya kitofauti kabisa na awamu ya tano hususani katika suala la matumizi ya Rais....
Acha wivu
 
Kwani mawaziri wanafanya nini,? Urais sio kutumia mabavu na kutafuta sifa Kama mwendazake, Sasa yote kwa yote kafanya nini, kipindi chake ufisadi imekua maradufu tangu nchi imepata Uhuru sema tu sijui alikwisha waroga kila kitu kushangilia, ila tunamshukulu kwa kuacha ametuaribia uchumi, mifumo, na mshikamano Kama Taifa,
 
usafiri wa gari ni rahisi kuliko ndege

shida ni rundo la mawaziri wanaotaka kila rais alipo nao wawepo
 
Tumiaga akili ya kichwani.
Ndege Ni safer, faster and cheaper kuliko msafara wa magari 50 yakiwemo ya kufungua ndege, kusababisha foleni na kuzuia shughuli za kiuchumi kwa eneo husika. Usisahau awamu ya tano helikopta zilitumika Kama sehemu ya msafara.
Au ubongo wako duni umeshasahau?
 
mtoa mada anataka kujua gharama tu, sio kitu kibaya kama mlipa kodi
 
Fikiria msafara wa V8 sitini (60) full tank na ndege moja.. Uone unafuu wa gharama uko wapi...
V8 zinatumia mafuta kidogo sana especially zikiwa zinakwenda bila foleni. Nadhani hilo linafahamika. Ndege inagharama zake ingawa ni nafuu inakwenda na muda sana.

But shida wanatumia lile Airbus ndio tatizo
 
Hili siyo kweli! Huwez kufananisha ule msafara kwa mizania yoyote ya gharama iwe sawa na sasa. That one was more than terrible. Niliona kwenye you tube(sijajua aliiweka nani), Tanzania tulikua ndani ya TOP 5 ya nchi zenye Marais wenye msafara mkubwa na ulinzi mkali. Hatusemi ni jambo baya kua na ulinzi mkali kwa viongozi wetu, ila kwa muktadha wa ulinganifu kati ya mama na mzee(R.I.P), mzee alitisha kwa msafara wenye gharama.
 
Nani kawaambia yale magari ya kifahari hayatumiki sasa hivi? Utofauti ni kuwa sasa hivi yanaenda binafsi bila kuongozana na Rais.
Yanatumika, kwani PM, VP hawatumii au zamani walikua hawatumii kwa kiasi? Jibu ni ndiyo walitumia, kwa sasa ndiyo pia mama anatumia, lakini kiasi kidogo sana. Helicopter haitumiki, convyoy imepungua na ile kusubiri sana misafara kumepungua. Anyway, kila mtu ana style yake ya kuongoza!
 
Uongo mtupu.
Viete 60, chopper, per diem za kundi la watu 200 kwenye hizo gari, usichukulie poa. Pia muda wa watu kusubiri msafara, assuming 2hrs kiuchumi ni loss ya billions of money
 
Hapo sasa! Labda wana miss kupunga mikono, vigelegele na kushinda barabarani au kuwekwa foleni na kufanya siku iende taratibu, labda zile fagia fagia IST barabarani wanazimiss, labda ving'ora na mikogo ya wanausalama barabarani ilikuwa burudani! Au kugawa michuzi barabarani?!
Ila ebu tupate majibu, ipi nafuu? Misururu ya magari na kupotezeana muda mijini au ndege afanye yake fasta bila bugudha kwa wenye vyombo vya moto au watoto kukatizwa masomo wampungue mkono?!
 
Waathirika wa safari za ndege za mama ni wale waliokuwa wanazurula na mwendazake kwenye misafara, wakila mihela ya kodi zetu bila huruma,
Wale waliokuwa wanampangia na kuwapanga wananchi wa maeneo tofauti, tofauti kumsimamisha ili awagawiye mahela.
Hao sasa wanaishi kama mashetani zamu yao. Ndiyo hawa wanaolalamika safari sasa ni za ndege. Wamejazana ofisini wanafuta vumbi na buibui masjala.

Wacha tupumzike, maana ile misafara ya magari akiingia tu kuoga, nyie huku barabarani mnasimamishwa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…