Tanzania bado ni salama sana na tunapaswa kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama

Ndugu zangu Watanzania,

Pamoja na matukio machache yaliyojitokeza hapa katikati,lakini haiondoi ukweli kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kubwa sana iliyotukuka ya kuhakikisha kuwa Taifa letu linaendelea kutamalaki kwa amani, Utulivu na usalama wa hali ya juu sana kuanzia mipakani hadi ndani ya Nchi,kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanafanya kazi zao katika mazingira ya amani na utulivu pasipo hofu wala wasiwasi.

Embu fikiria leo hii katika Historia ya Taifa letu tunashuhudia magari ya abiria makubwa kwa madogo yakisafiri usiku kucha katika mikoa mbalimbali yakipita katika misitu ya kila aina bila shida wala kutekwa wala kitisho cha kutekwa .hii yote ni kutokana na kuwepo kwa usalama wa kutosha Nchini unaotokana na kazi nzuri na iliyotukuka ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Kumbukeni ya kuwa suala la ulinzi na usalama ni suala gumu , zito na lenye kuhitajaji nguvu kubwa sana ya uwekezaji katika kupambana na matukio yote yenye kuhatarisha usalama.embu fikiria Taifa kama Marekani lenye teknolojia ya hali ya juu kabisa,vifaa vya kisasa ,watu wenye ujuzi wa kila aina pamoja na kamera kila kona,lakini Dunia nzima kwa macho yake ilishuhudia mgombea Urais na Rais wake mstaafu Donald Trump akipigwa Risasi ya sikioni akiwa jukwaani.

Nchi Kama Tanzania yenye watu zaidi ya Millioni 61 na yenye kuzungukwa na nchi takribani 7 na ikaendelea kuwa katika usalama kama huu tunao ushuhudia pasipo matukio makubwa yenye sura ya kigaidi au wahalifu kuvuka mipaka na kuja kufanya matukio hapa nchni ,ni lazma tuvipongeze sana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kuwalinda watanzania na mali zao pamoja na mipaka ya Nchi yetu.

Ni lazima tufahamu kuwa hali ipo hivyo kwa kuwa vyombo vyetu vipo macho saa 24 usiku na mchana,doria zinapigwa muda wote.ni kwa kuwa wapo askari wetu waliojitoa sadaka ya damu yao kwa ajili yetu watanzania ili tuishi kwa amani.ni kwa kuwa wapo askari wetu wanatokwa jasho ,machozi na damu kupambana na kila aina ya uharamia na uhalifu .

Tuwapeni moyo na kuwaunga mkono askari wetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.tusiwakatishe tamaa wala kuwatukana matusi wala kuwatolea maneno machafu.haya matukio machache ya watu kupotea naamini kuwa na sote tuamini ya kuwa vyombo vyetu vipo kazini kufanya upelelezi ili wote wapatikane wakiwa hai kabisa .kikubwa tutoe ushirikiano na tujue sote ni walinzi wa Taifa letu.

Tambua ya kuwa wewe ukiwa umelala usingizi chumbani kwako na mkeo au mume wako vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinakuwa macho kukulinda wewe na mali zako.ndio maana unaamka ukiwa salama wewe na mali zako.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
kichaa wewe
 
kwanza hongera kwa kutuonesh watanzania kuwa bado kuna watu wanaishi mapangoni!
Wengi huwa tunazungumza mada kwa utashi wetu endapo tu jambo hilo halijatokea kwenye maisha yetu directly. Mfano, Tunawea kusimulia kuwa wananjeshi wanakufa vita ili kulinda mipaka na nchi yetu ila siku mtoto wako ambaye ni mwananjeshi amepoteza maisha kwa hakika hii kauli huwezi kuisema! utabakia kujutia na kujilaumu kuwa kwanini haukumzuia asiende jeshini.
Siku ukipoteza member wa familia yako kwa tukio lenye mfanano huu huu! Njoo utupatie mrejesho!
Tanzania sio salama hata kidogo! Ni salama tu endapo ukijitoa akili na kujifanya mpumbavu tu! kama ......e vile!
 
Inakuwaje mtu mmoja tu ashambulie watu na kuwajeruhi mbele yenu?
Unapouliza hilo jiulize...ilikuwaje mtu ashushwe kwenye Basi Kwa nguvu, Kisha aonekane amefariki siku ya pili? Pia huyo mtu aliye jeruhi raia kwanin aachiwe na polisi alipokamatwa? Kisha kuendelea kutoa vitisho Kwa raia?
 
Yuko jamaa mmoja anaitwa Risasi Mwaulanga. Huyu alikuwa mbwekaji kweli hasa kwenye tv kuitetea ccm. Siku hizi meneja hoteli ya dada yake hapo Morocco maghorofani. Ni sawa na huyu Mwashambwa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Pamoja na matukio machache yaliyojitokeza hapa katikati,lakini haiondoi ukweli kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kubwa sana iliyotukuka ya kuhakikisha kuwa Taifa letu linaendelea kutamalaki kwa amani, Utulivu na usalama wa hali ya juu sana kuanzia mipakani hadi ndani ya Nchi,kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanafanya kazi zao katika mazingira ya amani na utulivu pasipo hofu wala wasiwasi.

Embu fikiria leo hii katika Historia ya Taifa letu tunashuhudia magari ya abiria makubwa kwa madogo yakisafiri usiku kucha katika mikoa mbalimbali yakipita katika misitu ya kila aina bila shida wala kutekwa wala kitisho cha kutekwa .hii yote ni kutokana na kuwepo kwa usalama wa kutosha Nchini unaotokana na kazi nzuri na iliyotukuka ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Kumbukeni ya kuwa suala la ulinzi na usalama ni suala gumu , zito na lenye kuhitajaji nguvu kubwa sana ya uwekezaji katika kupambana na matukio yote yenye kuhatarisha usalama.embu fikiria Taifa kama Marekani lenye teknolojia ya hali ya juu kabisa,vifaa vya kisasa ,watu wenye ujuzi wa kila aina pamoja na kamera kila kona,lakini Dunia nzima kwa macho yake ilishuhudia mgombea Urais na Rais wake mstaafu Donald Trump akipigwa Risasi ya sikioni akiwa jukwaani.

Nchi Kama Tanzania yenye watu zaidi ya Millioni 61 na yenye kuzungukwa na nchi takribani 7 na ikaendelea kuwa katika usalama kama huu tunao ushuhudia pasipo matukio makubwa yenye sura ya kigaidi au wahalifu kuvuka mipaka na kuja kufanya matukio hapa nchni ,ni lazma tuvipongeze sana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kuwalinda watanzania na mali zao pamoja na mipaka ya Nchi yetu.

Ni lazima tufahamu kuwa hali ipo hivyo kwa kuwa vyombo vyetu vipo macho saa 24 usiku na mchana,doria zinapigwa muda wote.ni kwa kuwa wapo askari wetu waliojitoa sadaka ya damu yao kwa ajili yetu watanzania ili tuishi kwa amani.ni kwa kuwa wapo askari wetu wanatokwa jasho ,machozi na damu kupambana na kila aina ya uharamia na uhalifu .

Tuwapeni moyo na kuwaunga mkono askari wetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.tusiwakatishe tamaa wala kuwatukana matusi wala kuwatolea maneno machafu.haya matukio machache ya watu kupotea naamini kuwa na sote tuamini ya kuwa vyombo vyetu vipo kazini kufanya upelelezi ili wote wapatikane wakiwa hai kabisa .kikubwa tutoe ushirikiano na tujue sote ni walinzi wa Taifa letu.

Tambua ya kuwa wewe ukiwa umelala usingizi chumbani kwako na mkeo au mume wako vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinakuwa macho kukulinda wewe na mali zako.ndio maana unaamka ukiwa salama wewe na mali zako.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Siku yakikufika ndiyo akili itaelewa somo lililopo ubaoni
 
Usalama uko wapi we kiande???
Watu kila siku wanapote na kukutwa wamekufa vifo vya kikatili. Wakati mwingine punguza kutukanwa hasira na matusi unayopata humu ni laana hiyo.
 
Wewe jishaue tu kujifanya msemaji wa watekaji na wauaji ipo siku yatakukuta
 
Umesahau kuweka namba ya simu
 
Usalama uko wapi we kiande???
Watu kila siku wanapote na kukutwa wamekufa vifo vya kikatili. Wakati mwingine punguza kutukanwa hasira na matusi unayopata humu ni laana hiyo.
Unafahamu nchi isiyo na usalama?
 
Tunawapongeza huku tukibubujikwa na machozi ,watu wetu wanakufa na kutekwa😭😭
 
Kwa sababu hayakuumizi hayo yanayowafika watu.
 
Back
Top Bottom