Tanzania bado ni salama sana na tunapaswa kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama

Watekaji wanajiweka wazi Sasa.
Hizi ajali za barabarani zinazojitokeza kila kukicha naomba sana zianze na watu kama wewe ili tusione maandiko yako ya hovyo hapa jukwaani
 
Ni salama kwa kuwa baba yako au Mama yako au mwanao hajatekwa na kuuliwa siku ya kikufika ndio utakapo juwa kuwa sio salaama
 
Kama humuogopi Mungu basi ogopa hata kuku. Hivi unajukuta nani kutoa kauli kama hiyo? Weee ni msemqji wa jeshu la polisi?

Nakushauri ufanye kazi za kukuingizia kipato kwa bidii zaidi na maarifa pamoja na uaminifu. Kama Mungu amepanga upate nafasi ya kisiasa utapata. Usiwafanye wazazi wako watukanwe kwasababu yako Kwasababu unachofanya sio uzalendo, ni uchawa na watu Kama nyie mkipewa nafasi za kisiasa ndio inafanya vijana wengine waharibike, waache kuwa true kwa Mungu na kwa nafsi zao, waanze kazi ya kusifu na kuabudu Miungu watu coz wanajua kazi hiyo inalipa.

Kwakweli sipendezwi na tabia zako za kuwa chawa zaidi ya kunguni
 
Kuwa mwanachama wa chama flani hakukutoi akili na hofu ya Mungu. Watu kama wewe 10 wanaweza kuzamisha hili taifa. Jikite kwenye kukosoa kwa staha, toa ushauri na ubunifu na kutetea haki kila eneo. Hayo mapambia achia kazi itajitangaza
 
Acha uchawa, mmemuua binti wa mika 18 tena akiwa ndani kwao, aibu kubwa.
mtakipata mnachokitafuta.
Poleni familia, mama anasema ni binti pekee ( form four) ambaye ndiye msomi mtegemewa na mboni ya familia ila katoweka kwa udhaifu wa jeshi letu la police.
 
Ukiwa na ugomvi na serikalini utaona nchi haina usalama ila ukiwa raia mwema nchi mbona ina amani tele
 
Mmmm! Mi nilikuwa najua kuwa, ni mimi tu ambaye huwa sisomi MAANDIKO yake. Heading, yaweza kunivutia, lakini nikilisoma jina lake kuwa ndiye mwandishi, sisumbuki kusoma!
Huyu mpumbavu kila nikiona jina ni la kwake naishia kusoma heading tuu
 
Ukiwa kama raia mwema Jenga nchi Yako kwa kupongeza panapostahili. Sema kweli panapostahili, kosoa panapostahili, shauri inavyostahili. Usilete furaha/kejeri kwenye msiba(wa raia mwema), leta huzuni. KIFO hugusa hisia za watu wote, aliyetekwa na kukutwa kafariki ni kiumbe chenye thamani kubwa. Wakati tulionao sasa ingefaa ushauri nini kifanyike kutokomeza utekaji na kuuawa watu, kuliko kupongeza au kupamba sifa kwa mamlaka ya ulinzi na usalama.
 
Why tupongeze failure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…